Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maisha ya Aina Mbili, Sura ya 117

    Ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 1 Yohana 1:3.Mar 125.1

    Hakuna kitu kinachohitajika katika kazi yetu kama matokeo ya wazi ya ushirika wetu na Mungu. Tunapaswa kuonesha katika maisha yetu ya kila siku kwamba tuna amani na pumziko ndani ya Mwokozi. Amani yake ndani ya mioyo yetu itaangaza uso. . . Ushirika na Mungu utaboresha tabia na maisha yetu. Watu watajua kwamba tumekuwa pamoja na Yesu kama ilivyokuwa kwa wale wanafunzi wa kwanza. Jambo hili litampatia mtendakazi nguvu ambayo kitu kingine cho chote hakiwezi kumpatia. Hapaswi kukubali apokonywe nguvu hiyo. Tunapaswa kuishi maisha ya aina mbili—maisha ya fikra na vitendo, maisha ya maombi binafsi na juhudi katika kazi.Mar 125.2

    Wale wote wanaojifunza chini ya Mungu wanahitaji muda wa kutulia kwa ajili ya kuongea na mioyo yao wenyewe, viumbe, na Mungu. .. Tunapaswa sisi wenyewe kunisikia Mungu akinena moyoni. Tukimngoja kwa utulivu wakati sauti zingine zote ziko kimya, utulivu wa moyo unaifanya sauti ya Mungu isikike zaidi. Anatusihi akisema, “Acheni, mjue kuwa Mimi ni Mungu.” Zab. 46:10. Hayo ndiyo maandalizi yenye ufanisi kwa ajili ya kazi zote za Mungu. Kati ya makundi yanayokwenda huku na huko kwa kasi, na shinikizo la shughuli nyingi za maisha, yeye anayepokea nguvu mpya kwa njia hiyo atazungukwa na nuru na amani. Atapokea nguvu mpya kimwili na kiakili. Maisha yake yatakuwa ya kupendeza na ataonesha uwezo wa Mungu utakaogusa mioyo ya watu.Mar 125.3

    Watu wengi, hata katika vipindi vyao vya tafakari, hushindwa kupokea baraka za ushirika wa kweli na Mungu. Huwa wanakuwa na haraka kupita kiasi. Hawa hupita kwa haraka katika eneo la uwepo wake, wakisimama kwa muda mfupi tu katika nyua takatifu, lakini hawakai kwa ajili ya ushauri. Hawana muda w a kukaa pamoja na yule Mwalimu toka mbinguni. Hurejea katika kazi zao wakiwa na mizigo yao.Mar 125.4

    Watenda kazi hawa hawataweza kufikia kiwango cha juu kabisa cha mafanikio wasipojifunza siri na kuwa na nguvu. Wanapaswa kutafuta muda wa kufikiri, kuomba, kumngoja Mungu ili awapatie uwezo mpya wa kimwili, kiakili na kiroho. Wanahitaji kuwa na nguvu ya Roho wake iwezayo kuinua. Wakiipokea hiyo, watahuishwa.Mar 125.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents