Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Udanganyifu wa Shetani ulio Mkuu Kuliko Wote, Sura ya 127

  Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii. Kumbukumbu 29:29.Mar 135.1

  Ufahamu wa kibinadamu katika mambo halisi na ya kiroho ni wa juu juu na usio kamili; kwa hiyo wengi hawawezi kupatanisha mitazamo yao ya kisayansi na kauli za Maandiko. Wengi wanakubali nadharia na makisio tu kama kanuni za kisayansi, na wanadhani kuwa neno la Mungu ni la kujaribiwa kwa maandiko “ya elimu iitwayo elimu kwa uongo.” 1 Tim. 6:20. Hawamwelewi Mwumbaji na kazi zake; na kwa sababu hawawezi kuyaeleza haya kwa kanuni za asili, historia ya Biblia inaonekana kama isiyoaminika. Wale wanaotilia mashaka uaminifu wa taarifa za Agano la Kale na Jipya mara kwa mara wanakwenda mbele zaidi na kutilia mashaka uwepo wa Mungu na hivyo kufikiria kwamba uwezo huu usio wa kawaida ni sehemu tu ya viumbe asili. Hali wakiwa wameachilia nanga yao, wanaachwa wakitanga tanga juu ya miamba ya udanganyifu.Mar 135.2

  Kwa namna hiyo wengi wanakosea na kutoka katika imani na kupotoshwa na mwovu. . .Falsafa ya kibinadamu imejaribu kutafuta na kuelezea mafumbo ambayo kamwe hayatafunuliwa milele zote. Kama watu wangefanya utafiti na kuelewa kile ambacho Mungu amekiweka wazi kumhusu Yeye mwenyewe na makusudi yake, wangeweza kuona utukufu, ukuu na uweza wa Yehova kiasi kwamba wangetambua udogo wao na wangeridhika na kile ambacho kimefunuliwa. . .Mar 135.3

  Udanganyifu wa Shetani ulio wa juu kuliko wote ni huu wa kufanya mawazo ya watu yatafute na kukisia yale ambayo Mungu hajayafunua na yale ambayo hakusudii tuyaelewe. Ni kwa namna hii pia Lusifa alipoteza nafasi yake mbinguni. Hakuridhika kwa sababu hakushirikishwa katika siri zote za makusudio ya Mungu, na akadharau kabisa yale yaliyokuwa yamefunuliwa kuhusu kazi yake katika nafasi ya juu aliyokuwa amepewa. Kwa kuzua hisia hiyo hiyo ya kutoridhika ndani ya malaika waliokuwa chini yake, alisababisha kuanguka kwao. Sasa anatafuta kuingiza roho hiyo mawazoni mwa watu na kuwaongoza pia kudharau amri za Mungu zilizo wazi.Mar 135.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents