Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Pambano Muhimu Sana Lililo Mbele Yetu, Sura ya 123

  Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Matendo 5:29.Mar 131.1

  Bahama kuu inawajia watu wa Mungu. Zahama inaijia dunia. Pambano la muhimu sana kuliko mapambano ya zama zote liko mbele yetu.... Suala la kushurutisha ushikaji wa Jumapili limeonekana kuwa bora na kupendwa kitaifa. Tutajua matokeo ya msukumo huu yatakavyokuwa. Lakini je, tupo tayari kwa tamko? Je, tumefanya kwa uaminifu wajibu aliotupa Mungu wa kutoa onyo kwa watu kuhusu hatari iliyo mbele yao?. . .Mar 131.2

  Wapo wengi ambao hawajatofautisha kati ya madai ya Sabato ya Biblia na msingi wa uongo ambapo hoja ya Jumapili imesimikwa. Mfumo wowote unaopatana na kutungwa kwa sheria hiyo ni hakika unapatana na upapa, ambao kwa muda mrefu sana umekuwa katika mapambano dhidi ya uhuru wa dhamiri. Kile kinachodaiwa kuanzishwa na “Ukristo” ambacho ni uadhimishaji wa Jumapili kinatokana na “siri ya kuasi”; na kutekelezwa kwake kutakuwa ni hatua ya kutambua kanuni ambazo hakika ni jiwe la msingi la Kirumi. Kwa kitendo cha taifa letu kukana kanuni za serikali yake kiasi cha kupitisha sheria ya Jumapili, Uprotestanti utakuwa umeshikana mikono na upapa; na maana halisi ya hatua hii itakuwa nr kuupa nguvu udhalimu ambao kwa muda mrefu na kwa shauku umekuwa ukitafuta fursa ya kuinuka tena na kutawala .Mar 131.3

  Kama upapa au kanuni zake vitapewa tena mamlaka kisheria, moto wa mateso utawashwa upya dhidi ya wale ambao hawatakabidhi dhamiri na kuuacha ukweli ili kuridhia makosa ya wengi. Uovu huu upo katika hatua ya kudhihirika.Mar 131.4

  Kama Mungu ametupatia nuru akituonesha hatari zilizo mbele yetu, tunawezaje kusimama tukiwa safi mbele zake kama tumedharau kuweka jitihada zetu zote zilizo katika uwezo wetu ili kuileta nuru hiyo mbele za watu? Je, tunaridhika kuwaacha wakutane na jambo hili kubwa bila kuwaonya?. . .Mar 131.5

  Wakati sheria za watawala wa kidunia zitakapowekwa kupingana na sheria za Mtawala wa juu wa Ulimwengu wote, ndipo wale walio wa Mungu watakuwa wakweli kwake.Mar 131.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents