Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kujionesha kwa Mamlaka za Kidunia, Sura ya 132

  “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti.” 2 Timotheo 4:3.Mar 140.1

  Kwa haraka watu wanajipanga wenyewe chini ya bendera ambayo wameichagua, wakingojea na kutazama mienendo ya viongozi wao kwa wasiwasi mkubwa. Wapo wale ambao wanakesha na kungojea na kufanya kazi kwa ajili ya kuja kwa Bwana wetu; huku kundi lingine likijiunga chini ya mamlaka ya yule mwasi mkuu. Wanamtafuta Mungu katika wanadamu, na Shetani anajifanya kuwa kama ndiye huyo wanayemtafuta. Watu wengi watadanganyika kutokana na kuukataa ukweli, na hivyo watakikubali kile cha bandia. Binadamu watatukuzwa kama Mungu.Mar 140.2

  Kadiri tunavyokaribia mwisho wa wakati, kutakuwa na maonesho makubwa na makubwa zaidi ya mamlaka za kidunia, miungu ya kidunia itadhihirisha ishara za uwezo wao, na itajionesha hadharani mbele ya miji mikubwa ya ulimwengu; na tayari udhihirisho huu wa wazi umeanza kutimia. Kwa kutumia mifano mingi, Bwana Yesu alimwonesha Yohana uovu na mvuto wa udanganyifu wa wale ambao wamejipambanua kwa kuwatesa watu wa Mungu. Wote wanahitaji hekima ili kuchunguza kwa uangalifu ile siri ya uasi ambayo inaonekana sana katika kufungwa kwa historia ya dunia hii. . . Katika saa hii tunayoishi, Bwana amewaita watu wake na amewapatia ujumbe wa kutangaza. Amewaita ili kuweka wazi uovu wa yule mtu wa kuasi ambaye ameifanya sheria ya Jumapili kuwa ni alama ya mamlaka yake, yule ambaye aliazimu kubadili majira na sheria, na kuwadhulumu watu wa Mungu ambao wamesimama imara ili kumheshimu Yeye kwa kuishika Sabato ya kweli pekee, Sabato ya uumbaji. . .Mar 140.3

  Hatari za siku za mwisho zinatukabili, na katika kazi yetu tunapaswa kuwaonya watu juu ya hatari waliyomo. Hebu matukio mazito ambayo unabii umeyafunua yawekwe wazi kwa watu. Kama watu wangekuwa wameamka hata kwa nusu tu, kama wangetambua jinsi ambavyo yale matukio yaliyotabiriwa katika kitabu cha Ufunuo yamekaribia, basi matengenezo yangefanyika katika makanisa yetu, na watu wengi zaidi wangeuamini ujumbe. Hatuna muda wa kupoteza; Mungu anatuita ili tukeshe kwa ajili ya roho kama watu tutakaotakiwa kutoa hesabu.Mar 140.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents