Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uwakfu wa Kazi ya Mama

    Yampasa mwanamke kushika madaraka ambayo Mungu alimwekea tangu zamani, sawa na yale ya mumewe. Ulimwengu una hitaji akina mama ambao ni mama siyo kwa jina tu, bali kwa kweli kama ilivyo maana ya neno lenyewe. Twaweza kusema kuwa kazi zimhusuzo mwanamke ni takatifu zaidi ya zile za mwanamume. Basi, mwanamke na afahamu uwakfu wa kazi yake na kwa nguvu na kicho cha Mungu ashike kazi yake ya maisha. Hebu awafundishe watoto wake kwa ajili ya manufaa katika ulimwengu huu na kwa ajili ya makao katika ule ulimwengu bora zaidi.KN 163.2

    Mke na mama asingetoa nguvu zake na kukubali uwezo wake kutotumika, na kumtegemea kabisa mumewe. Nafsi yake haiwezi kuchanganyika ndani ya nafsi ya mumewe. Yampasa kuona kuwa ana haki sawa na mumewe-kusimama karibu naye, akiwa mwaminifu kwa kazi na wajibu umpasao. Kazi yake katika mafundisho ya watoto wake ni yenye kukuza hali kwa kila jambo na yenye kuadilisha sawa na kazi iwayo yote awezayo kufanya mumewe, hata kama kazi yenyewe iwe ya cheo cha iaji mkuu wa nchi nzima.KN 163.3

    Mfalme penye kiti chake cha enzi hana kazi ya cheo kikubwa zaidi ya ile aliyo nayo mama. Mama ni malkia kwa watu wa nyumba yake. Anao uwezo wa kuzikuza tabia za watoto wake, kusudi wapate kufanywa wafae kwa maisha bora, ya milele. Malaika asingeweza kuomba kazi ya cheo kikubwa zaidi ya hiyo; maana kwa kufanya kazi hii (mama) humtumikia Mungu. Basi, na afahamu ubora wa kazi zake na kuvaa silaha zote za Mungu, ili apate kuyapinga mashawishi ya kukifuata kipimo cha walimwengu. Kazi yake ni ya wakati huu na ya umilele pia.KN 163.4

    Kama waume huenda zao kazini, na kuwaacha wake zao kuwatunza watoto nyumbani, mke na mama hufanya kazi kubwa na ya maana sawa sawa kabisa na kazi ile afanyayo mume na baba. Ingawa mmoja yuko nje mahali pa kazi ya umishenari mwingine ni mmishenari nyumbani, ambaye shughuli zake na mashaka na mizigo yake mara nyingi hupita sana ile ya mume na baba. Kazi yake ni nzito na yenye maana. Mumewe nje kazini aliko aweza kupata heshima na sifa za watu, huku (mke) mwenye kutaabika nyumbani akiwa pengine asiyepata sifa yo yote ya kidunia kwa kazi yake. Lakini ikiwa hufanya kazi hii kwa faida ya jamaa yake, akitafuta kuziendeleza tabia zao zifanane na Kielelezo Kitakatifu, malaika mwenye kuandika kumbukumbu huliandika jina lake kama mmojawapo wa wamishenari wakubwa ulimwenguni. Mungu huona mambo vingine, tofauti na macho ya mwanadamu yenye kikomo yaonavyo.KN 163.5

    Ulimwengu umejaa mivuto mibaya. Mitindo na mila hutoa mvuto wa nguvu juu ya vijana. Ikiwa mama anakosa kazini mwake kuwafundisna, kuwaongoza, na kuwashika watoto wake, kwa urahisi watayakubali mabaya na kuyaasi mema. Hebu kila mama amwendee Mwokozi wake kwa sala hii, “Tufundishe jinsi itupasavyo kumwamuru mtoto, na jinsi ya kumtendea.” Hebu na aangalie mafundisho ambayo Mungu ametoa katika neno lake, naye atapewa hekima kadiri anavyohitaji.KN 164.1

    Kila mama na aone kuwa dakika zake zina thamani isiyohesabika; kazi yake itajaribiwa siku ile kuu ya kutoa hesabu. Ndipo itaonekana kuwa makosa na uhalifu wa wanaume kwa wanawake wengi hutokana na ujinga na dharau za wale ambao kazi ingekuwa kuwaongoza watoto katika njia nyofu. Tena itaonekana kuwa wengi walionufaisha ulimwengu kwa nuru halisi na kweli na utakatifu ni kwa sababu ya mafundisho ambayo yalikuwa chanzo cha mvuto wao na kufaulu kwa mama Mkristo mwenye kuomba kwa bidii.KN 164.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents