Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maisha na Kazi ya Ellen E.G. White

    Ellen G. Harmon na dada yake pacha walizaliwa Novemba 26, 1827, Gorham, Maine, mashariki ya kaskazini mwa Marekani (United States). Alipokuwa na umri wa miaka tisa, Ellen alipatwa na ajali ambayo jiwe lililotupwa na mwanafunzi mwenzake mzembe lilimpiga. Jeraha hili la usoni lilikuwa karibu kumwua. nalo lilimtia uahaifu mwilini hata hakuweza kuendelea na masomo.KN 17.5

    Alipokuwa na umri wa miaka kumi na mmoja alimpa Mungu moyo wake na si muda mrefu baada ya hapo akabatizwa kwa kuzamishwa majini baharini na akapokewa kama mshiriki wa Kanisa la Methodist. Pamoja na watu wengine wa jamaa yake, Ellen alihudhuria mikutano ya Kiadventista Portland, Maine, naye akayaamini mafundisho juu ya kukaribia kuja kwa Kristo mara ya pili, kulikoonyeshwa na William Miller na wenzake, na kwa matumaini mengi akatazamia marejeo ya Mwokozi.KN 17.6

    Siku moja asubuhi Desemba, 1844, alipokuwa akisali pamoja na wanawake wengine wanne, uwezo wa Mungu ulimsnukia. Kwanza alihamishwa kimawazo kutoka duniani; kisha katika ufunuo wa mfano aliona safari za Waadventista kwenda kwenye mii wa Mungu, na ijara ya wale waliokuwa waaminifu. Kwa hofu na kutetemeka msichana huyu mwenye umri wa miaka kumi na saba alisimulia neno hili na njozi za baadaye kwa waumini wenzake wa Portland. Kisha kadiri alivyopata nafasi, akahubiri njozi hii kwa makundi ya Waadventista wa Maine na katika nchi jirani.KN 18.1

    Agosti, 1846, Ellen Harmon akaoana na James White, mhubiri kijana Mwadventista. Katika miaka yote thelathini na mitano iliyofuata maisha ya Ellen White yaliungana kabisa na yale ya mumewe katika kazi ya Injili kwa junudi, mpaka kifo cha mumewe, Agosti 6, 1881. Walisafiri mahah pengi katika Marekani, wakihubiri na kuandika, wakipanda mbegu na kujenga, wakipanga mambo na kuamuru.KN 18.2

    Muda na jaribio vimethibitisha jinsi misingi ambayo Mchungaji na Ellen White na wenzao waliiweka ilivyo mipana na imara, na jinsi walivyojenga vizuri kwa busara. Waliongoza miongoni mwa Waadventista wenye kuishika Sabato na kuanzisha kazi ya kuchapisha vitabu na magazeti mnamo mwaka 1849 na 1850, na kukuza utaratibu wa Kanisa kwa mipango mizuri ya habari za fedha katika miaka mingine baada ya 1850. Jambo hili lilikamilishwa na kupangwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Waadventista wa Sabato’ mnamo mwaka 1863. Miaka iliyofuata mwaka huo ukawa ni mwanzo wa kazi yetu ya uganga, na, kazi yetu kuu ya elimu ya madhehebu kuanzishwa mara baada ya mwaka wa 1870. Mpango wa kufanya mikutano ya makambi ya kila mwaka ulikuzwa mnamo mwaka 1868, na mwaka 1874 Waadventista Wasabato walituma wamishenari wao wa kwanza.KN 18.3

    Maendeleo haya yote yaliongozwa na maonyo mengi yaliyosemwa na kuandikwa ambayo Mungu aliwapa hawa kwa njia ya Ellen G. White.KN 18.4

    Habari nyingi za mwanzoni ziliandikwa kwa njia ya barua za mtu mwenyewe, au kwa njia ya habari katika Present Truth(Ukweli wa Leo), gazeti letu la kwanza kuchapishwa. Mpaka mwaka 1851 ndipo Ellen White alipotoa kitabu chake cha kwanza cha kurasa 64, kilichoitwa A Sketch of the Christian Experience and View of Ellen G. White. KN 18.5

    Kuanzia mwaka 1855 aina kadha wa kadha za magazeti zilichapishwa, kila moja likiwa na jina la Testimony of the Church(ushuhuda wa Kanisa) . Haya yalitoa ujumbe wa kufaa wa mafundisho na maonyo ambayo mara kwa mara Mungu alichagua kuyapeleka kuwabariki, kuwakaripia, na kuwaongoza watu wake. Ili kuitimiza haja ya daima ya mafundisho maonyo haya, yalichapishwa mara ya pili mnamo mwaka 1885 katika vitabu vinne, na pamoja na ongezeko la vijitabu vingine, ambavyo vilichapishwa kati ya mwaka 1889-1909, na kufanya jumla ya vitabu tisa vya Testimonies for the Church(Shuhuda kwa Kanisa).KN 18.6

    Bwana na Bibi White walizaa watoto wanne. Mtoto mkubwa wa kiume, Henry, aliishi akawa na umri wa miaka kumi na sita; mvulana mdogo kuliko wote, Herbert, alifariki akiwa na umri wa miezi mitatu. Watoto wa kiume wawili wa katikati, Edson na William, wakaishi hata wakawa watu wazima na kila mmoja akafanya kwa bidii kazi ya Kanisa la Waadventista Wasabato.KN 19.1

    Kwa kuitikia mwito wa Halmashauri Kuu ya Kanisa,Ellen White alikwenda Ulaya wakati wa kiangazi mwaka 1885. Huko alitumia miaka miwili akiwatia nguvu na kuanzisha kazi mpya kwenye Bara hilo. Akiishi Basle, Switzerland, alisafiri mahali pengine kusini, katikati na kaskazini ya Ulaya, akihudhuria mikutano mikubwa ya Kanisa hili na kukutana na waumini katika mikutano yao.KN 19.2

    Baada ya miaka minne alipokwisha kurejea Marekani Ellen White akiwa mwenye umri wa miaka 63, kwa kuitikia mwito wa Halmashauri kuu alisafiri baharini kwenda Australia. Kule alikaa kwa muda wa miaka tisa, akisaidia kuanzisha na kukuza kazi, hasa upande wa kazi ya elimu na utabibu. Ellen White alirejea mwaka 1900 kufanya makao yake upande wa magharibi mwa Marekani, katika St. Helena, California, Mahali alipokaa mpaka kufa kwake mwaka 1915.KN 19.3

    Katika kazi ya Ellen White ya muda mrefu wa miaka 60 Marekani na miaka 10 katika nchi za kigeni, alipewa njozi karibu 2,0 ambazo kwa bidii zake nyingi katika kuwashauri watu mmoja mmoja, makanisa, mikutano ya watu kwa jumla, na hata wakati wa kikao kikuu cha Halmashauri kuu aliongoza maendeleo ya kanisa hili. Kazi ngumu ya kuwapa wote wahusikanao ujumbe aliopewa na Mungu hakuchoka kuifanya.KN 19.4

    Maandishi yake yalikuwa zaidi ya kurasa mia moja elfu, Ujumbe aliouandika uliwafikia watu kwa kuwapelekea habari mwenyewe, na kwa makala za juma kwa juma katika magazeti ya madhehebu yetu na katika vitabu vyake vingi. Mafundisho hayo yalihusiana sana na historia ya Biblia, maisha ya Kikristo ya kila siku, afya, elimu, uinjilisti na mambo mengine makubwa ya kufaa. Vitabu kadha wa kadha miongoni mwa vitabu vyake arobaini na sita vimechapishwa katika lugha kuu ulimwenguni na nakala milioni nyingi zimeuzwa.KN 19.5

    Alipokuwa mwenye umri wa miaka 81 Ellen White alivuka bara la (Marekani) kwa mara yake ya mwisho kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu cha mwaka 1909. Miaka 6 ya maisha yake iliyokuwa imesalia aliitumia kumaliza kazi yake ya vitabu. Karibu na mwisho wa maisha yake Ellen White aliandika maneno haya: “Kama maisha yangu yakiachwa yazidi kuendelea, vema, ama sivyo, maandishi yangu yatasema daima, na kazi yake itasonga mbele mpaka siku ya mwisho.”KN 19.6

    Kwa moyo usio na hofu kwa matumaini kamili kwa Mkombozi wake, akafa nyumbani kwake Julai 16, 1915, na akazikwa kando ya mumewe na watoto katika Oak Hill Cemetery, Battle Creek, Michigan.KN 20.1

    Ellen White alithaminiwa na kuheshimiwa na watenda kazi wenzake, Kanisa, na watu wa nyumbani mwake, kama mama mcha Mungu na mtu mwaminifu, mkarimu, mtenda kazi hodari wa kidini. Kamwe hakushika kazi ya afisa wa Kanisa. Ilijulikana na Kanisa na yeye mwenyewe kwamba alikuwa “mjumbe” mwenye ujumbe kutoka kwa Mungu kwa watu wa Mungu. Kamwe hakuwataka watu kumtazama, wala hakutumia kipawa chake kujinufaisha kwa habari za fedha au ili kupendwa na wengi. Maisha yake na vyote alivyokuwa navyo vilitolewa wakfu kwa kazi ya Mungu.KN 20.2

    Wakati wa kufa kwake mchapishaji wa gazeti lililopendwa sana na watu wengi, la kila juma, The Independent, katika toleo la Agosti 23, 1915, aliandika maneno yake yanayoelezea juu ya maisha ya Ellen White kwa kusema haya: “Alikuwa mwaminifu kabisa katika imani yake katika mafunuo yake. Maisha yake yalistahili. Hakuonyesha kiburi cho chote cha mambo ya kiroho, naye hakutafuta faida inayopatikana kwa njia mbaya. Aliishi na kutenda kazi ya kustahili nabii mwanamke.”KN 20.3

    Miaka kadha wa kadha kabla ya kufa kwake, Ellen White alibuni Bodi ya Wadhamini, watu mashuhuri wa Kanisa alimoacha maandishi yake na agizo kuwa ni iuu yao kuyatunza na kuendelea kuyachapisha . Ikiwa na ofisi yake kwenye makao makuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato Marekani, Bodi hii hukuza na kuendelea kutoa vitabu vya Ellen G. White katika lugha ya Kiingereza na kusaidia kutolewa ama vitabu vizima ama kwa sehemu katika lugha zingine. Pia wametoa vitabu kadha wa kadha kwa kutumia nakala za magazeti na maandishi yake. Kitabu hiki kimetolewa kwa idhini ya Bodi hiyo.KN 20.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents