Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maburudisho Yawezayo Kuwapendeza Matajiri na Maskini Pia

  Vijana hawawezi kufanywa kuwa watulivu na wazito kama wazee, au mtoto afanywe mwenye busara wala mtaratibu kama bwana. Huku anasa za dhambi zikilaumiwa, kama ipasavyo, hebu wazazi, walimu na walezi wa vijana wawapatie badala yake furaha za halali ambazo hazitaharibu tabia za uadilifu. Msiwalazimishe vijana kutii amri kali ambazo zitawafanya wajione kuwa wanadhulumiwa hata iwafanye kuasi na kuzifuata njia za upotovu. Kwa mkono imara, mpole, na wa huruma shikeni madaraka mkiongoza na kuzitawala akili na makusudi:yao, walakini kwa upole, kwa busara, kwa upendo, ili wajue kuwa mnawafikiria na mnawatakia mema. 4CT 335;KN 183.4

  Ziko namna za maburudisho ambazo zina faida kubwa akilini na mwilini pia. Akili yenye busara itapata njia ya kufurahi na mwilini pia. Akili yenye busara itapata njia ya kufurahishwa na kupumzishwa, siyo katika mambo yaliyo halali tu, bali yanayovutia pia. Michezo ya nje, kuzitafakari kazi za Mungu katika viumbe vya asili, yatakuwa mambo ya faida kabisa. 54T 653;KN 183.5

  Hakuna maburudisho yatakayowanufaisha sana watoto na vijana kama yale yanayowafanya wawasaidie wengine, kuliko nafsi zao wenyewe. Kwa kawaida vijana ni wepesi kushauriwa. 6Ed. 212;KN 183.6

  Mungu ameruzuku kwa ajili ya furaha ya kila mmoja kile awezacho kufaidi tajiri na maskini pia-furaha ipatikanayo kwa kukuza usafi wa mawazo na matendo ya fadhila; furaha iletwayo na kusema maneno ya huruma na kutenda matendo mema. Nuru ya Kristo hung’aa kwa wale watendao huduma ya namna hii ili kuyatia nuru maisha yaliyotiwa giza na huzuni nyingi. 797 57;KN 184.1

  Kuna mambo mengi ya muhimu, na manufaa yapasayo kutendwa ulimwenguni humu ambayo yangeifanya michezo ya kujifurahisha isilazimu sana. Ubongo, mifupa na misuli vitaimarika na kupata nguvu kwa kutumika kwa kusudi la kufanya mema, kufikiri sana, na kufanya mashauri kwa akili ambako kutavizoezesha viungo hivyo kuwa na uwezo wa akili na nguvu za mwilini zitakazotumika kwa manufaa ya talanta walizopewa na Mungu ambazo kwazo vyaweza kumtukuza Mungu. 8AH 509;KN 184.2

  Sikatazi mazoezi mepesi ya kucheza mpira; lakini haya, ijapokuwa yawe mepesi pengine huwa ya kuchosna.KN 184.3

  Naogopa siku zote matokeo ambayo hufuata mara baada ya hiyo michezo. Huleta matumizi ya fedha ambayo ingetumiwa kuwaletea nuru ya ukweli watu wanaopotea nje ya Kristo. Anasa na matumizi ya mali kwa kujipendeza nafsi mwenyewe, ambayo hupeleka kidogo kidogo kwenye kujitukuza, na kujizoeza katika michezo hii kwa ajili ya raha ama anasa tu huleta upendo na tamaa ya mambo yasiyofaa katika tabia kamilifu ya Mkristo. 9AH 499;KN 184.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents