Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mapatano na Umoja Ndiyo Ushuhuda Wetu Wenye Nguvu Sana

    Siyo upinzani wa walimwengu unaotuhatarisha zaidi; bali maovu yanayofurahiwa na kutunzwa mioyoni mwa waumini ndiyo yanayoleta maangamizi makubwa na kuzuia sana maendeleo ya kazi ya Mungu. Hakuna njia nyingine ya hakika zaidi ya kuidhoofisha hali yetu ya kiroho kuliko kuwa na wivu, kutuhumiana, kujawa na roho ya kutafutana makosa na kudhaniana maovu. “Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani” (Yakobo 3:15-18).KN 51.1

    Mapatano na umoja ukiwapo miongoni mwa watu wenye tabia mbalimbali ni ushuhuda wenye nguvu sana uwezao kuonyesha kwamba Mungu amemtuma Mwanawe ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi. Tumepewa fursa ya kutoa ushuhuda huu. Lakini, ili kufanya hili hatuna budi kujitia chini ya amri ya Kristo. Tabia zetu hazina budi kuumbwa kupatana na tabia yake, nia zapaswa kutiwa chini ya nia yake. Ndipo tutafanya kazi pamoja pasipo kugongana hata kidogo.KN 51.2

    Tofauti ndogo zinazopong’ang’aniwa sana huleta vitendo ambavyo huharibu ushirika wa Kikristo. Tusikubali kumnufaisha adui kwa udhaifu wetu huu. Tuzidi kumkaribia Mungu zaidi na kukaribiana sisi kwa sisi. Ndipo tutakuwa kama miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, na kunyweshwa na mto wa maji ya uzima. Nasi tutakuwa wenye kuzaa matunda kwa wingi ajabu iliyoje! Je Kristo hakusema: “Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana” (Yohana 15:8).KN 51.3

    Sala ya Kristo ikisadikiwa kabisa, mafundisho yake yakiingizwa katika maisha ya kila siku ya watu wa Mungu, umoja wa utendaji utaonekana katika watu wa ngazi zote. Ndugu atafungamanishwa na ndugu kwa vifungo vizuri vya thamani vya upendo wa Kristo. Roho wa Mungu peke yake ndiye awezaye kuleta umoja huu. Yeye aliyejitakasa aweza kuwatakasa wanafunzi wake. Wakiwa na umoja naye, watakuwa na umoja wao kwa wao katika imani takatifu sana. Tukijitahidi kwa ajili ya umoja huu kama Mungu anavyotaka sana kujitahidi kwa ajili yake, tutaupata. 33T 242,243;KN 51.4

    Siyo wingi wa sheria, majengo makubwa na kujionyesha kwa nje ambavyo Mungu anavihitaji bali utendaji kwa moyo wa maelewano wa watu wa pekee, watu wa thamani waliochaguliwa na Bwana waliungana wao kwa wao, ambao uzima wao umefichwa pamoja na Kristo kwa Mungu. Kila mtu anapaswa mwenyewe kusimama mahali pake, akitoa mvuto mzuri katika wazo, neno; na tendo. Watenda kazi wote wa Mungu wakifanya hili, na mpaka hapo tu, ndipo kazi yake itakamilika, na yote kuwa sawa. 48T183;KN 52.1

    Mungu anahitaji watu wa imani kamili na akili bora wenye kutofautisha dhahiri kati ya kweli na uwongo. Kila mmoja anapaswa kujihadhari, akijifunza na kuyatumia mafundisho yaliyotolewa katika sura ya kumi na saba ya Yohana, na kulinda imani yenye nguvu katika ukweli wa wakati huu. Tunahitaji kujitawala ambako kutatuwezesha kuenenda sawasawa na ombi la Kristo. 58T 239;KN 52.2

    Moyo wa Mwokozi hufikiri juu ya wafuasi wake kutimiza kusudi la Mungu lote, kimo na kina chake pia. Yawapasa kuwa na umoja katika Yeye, ijapokuwa wametawanyika ulimwenguni. Lakini Mungu hawezi kuwafanya kuwa wamoja katika Kristo isipokuwa kama watakubali kuachana na njia yao wenyewe na kuifuata njia ya njia Kristo. 68T 243;KN 52.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents