Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Shauri Jema Juu ya Kutoa Hesabu ya Watoto

    Watoto ni urithi wa Bwana, ni juu yetu kutoa habari za namna tufanyavyo na mali yake Mungu. Kwa upendo, imani, na sala, hebu wazazi wafanye kazi kwa ajili ya watu wa nyumbani mwao, mpaka kwa furaha waweze kufika mbele za Mungu wakisema, “Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na Bwana.”KN 167.5

    Mungu angependa wazazi kutenda lcama watu wenye akili na kuishi kwa njia ambayo kila mtoto aweza kufundishwa vizuri, ili mama apate kuwa na nguvu na nafasi ya kutumia uwezo wa akili zake katika kuwapa watoto wake wadogo malezi mema kwa kushirikiana na mafaika. Yampasa awe na moyo wa kutenda vizuri wajibu wake na kufanya kazi yake kwa kicho na upendo wa Mungu, kusudi watoto wake wapate kuwa mbaraka kwa jamaa na kwa watu mtaani.KN 167.6

    Mume na baba angeyafikiria mambo haya yote ili mke na mama wa watoto wake asije akachoshwa na kulemewa kwa kukata tamaa. Apaswa kuona kuwa mama wa watoto wake hakutiwa katika shida mahali asipoweza kuwatendea haki watoto wake wengi, hata iwabidi kukua pasipo kupata malezi mazuri.KN 168.1

    Wako wazazi ambao, bila kufikiri kama waweza kuwatendea ipasavyo jamaa kubwa ama sivyo, huzijaza nyumba zao watoto hawa wadogo wasioweza kujihudumia wenyewe, wenye kuwategemea tu wazazi wao kwa matunzo na kwa mafundisho. Hili ni kosa baya, si kwa mama tu, bali kwa watoto wake na kwa jamii ya watu mtaani. Mtoto mikononi mwa mama mwaka kwa mwaka ni udhalimu mkuuu kwake. Hupunguza, na mara nyingi huharibu starehe na kuongeza uchovu wa kazi nyumbani. Huwanyang’anya watoto matunzo, elimu na furaha ambayo wazazi wangeiona kuwa ni wajibu wao kuwapa.KN 168.2

    (Wazazi) wangefikiri kwa makini riziki wawezazo kuwapatia watoto wao. Hawana haki kuzaa watoto ulimwenguni kuwa mzigo kwa wengine.KN 168.3

    Mwisho wa mtoto utakavyokuwa ni jambo lisilofikiriwa ila kidogo tu kama nini! Kuiridhisha ashiki ndilo wazo kubwa tu, na mke na mama hutwishwa mizigo ambayo hudhoofisha nguvu zake za uhai na kupoozesha uwezo wake wa kiroho. Akiwa na afya dhaifu na moyo uliokatishwa tamaa hujiona amezungukwa na kundi la watoto asiloweza kulitunza kama impasavyo. Kwa kukosa malezi mazuri yawapasayo kupata, hukua na kumdharau Mungu na kuambukiza wengine maovu ya tabia zao wenyewe, na hivyo ndivyo lipatikanavyo jeshi ambalo Shetani huweza kulitumia kama apendavyo. 6AH 159-164.KN 168.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents