Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Matokeo ya Elimu ya Kikristo

  Kadiri watoto walivyoimba hekaluni, “Hosana; ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana” (Markol 1:90), ndivyo siku hizi za mwisho sauti za watoto zitakavyopaswa kuutoa ujumbe wa mwisho wa onyo kwa ulimwengu unaopotea. Wale wenye akili mbinguni watakapoona kuwa watu hawaruhusiwi tena kulitoa Neno la Mungu, Roho wa Mungu atawajilia watoto, nao watafanya kazi ya kulihubiri Neno la Mungu, kazi ambayo watenda kazi wazee hawawezi kuifanya, kwa sababu njia yao itafungwa.KN 239.2

  Shule zetu za Kanisa zimeamuriwa na Mungu ziwepo kuwatayarisha watoto kwa kazi hiyo kubwa. Hapa watoto wanapaswa wafundishwe maneno ya utume. Yawapasa kujiandikisha katika jeshi la watenda kazi kuwasaidia wagonjwa na wenye shida. Watoto huweza kushiriki katika utume kwa kazi ya utabibu, na kwa mambo yao madogo madogo huweza kuiendesha. Matoleo yao huenda yakawa madogo lakini kila kidogo husaidia, na kwa jitihada zao roho za watu wengi zitaletwa kwenye ukweli. Kwa njia yao ujumbe wa Mungu na nguvu zake za kuokoa utatangazwa kwa mataifa yote. Basi Kanisa na lichukue mzigo kwa ajili ya wanakondoo wa kundi hili. Watoto wafundishwe na kuzoezwa kumtumikia Mungu, maana wao ndio urithi wa Bwana.KN 239.3

  Zikiendeshwa vizuri, shule za Kanisa zitakuwa njia ya kuinua hali ya ukweli mahali ambapo zinajengwa; kwa kuwa watoto wanaopokea elimu ya Kikristo watakuwa mashahidi wa Kristo. Kama Yesu hekalum alivyoeleza siri ambazo makuhani na wakuu walikuwa hawajazifahamu, ndivyo katika kazi ya mwisho wa dunia hii watoto ambao wamefundishwa vizuri watakavyofanya kwa maneno yao mepesi ambayo yatawashangaza watu ambao sasa husema juu ya “elimu ya juu zaidi.” 416T.202,203;KN 239.4

  Nalionyeshwa kuwa “Chuo Kikuu chetu” kilikusudiwa na Mungu kuitekeleza kazi hii kubwa ya kuokoa roho za watu. Ni hapo tu talanta za mtu zitakapowekwa chini ya mamlaka ya Roho wa Mungu na kutawaliwa naye ambapo zitatolewa zitumike kwa faida kamili. Mafundisho na kanuni za dini ni hatua za kwanza katika kupata elimu bora, na kuwa na msingi hasa wa elimu ya kweli. Maarifa na elimu havina budi kutiwa nguvu na Roho wa Mungu kusudi kufaa kwa makusudi bora sana. Mkristo peke yake ndiye awezaye kuitumia vema elimu. Ili elimu ithaminiwe kabisa, haina budi iangaliwe na kupimwa kwa upande wa dini. Moyo ambao umeadilishwa na neema ya Mungu nufahamu vizuri thamani halisi ya elimu. Sifa za Mungu, kama zionekanavyo katika kazi zake za kuumba, huweza tu kuthaminiwa kama tukimfahamu Muumbaji. Kusudi kuwaelekeza vijana kwenye chemchemi ya kweli, MwanaKondoo wa Mungu azichukuaye dhambi za ulimwengu, walimu hawana budi kuwa na elimu ya hakika juu ya njia takatifu. Elimu ina nguvu kama ikiunganishwa na kumcha Mungu kwa kweli. 424T432-435.KN 240.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents