Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Usidharau Mahitaji ya Akilini

  fslimeonyeshwa kuwa huku wazazi wanaomcha Mungu daima wakiwazuia watoto wao, wangejifunza tabia na moyo wao, na kujaribu kutimiza mahitaji yao. Wazazi wengine hushughulikia mahitaji ya muda ya watoto wao kwa uangalifu sana; huwauguza kwa huruma na uaminifu wanapoumwa, kisha hufikiri kwamba wametimiza wajibu wao. Hapa hufanya kosa. Kazi yao ndipo imeanza tu. Mahitaji ya moyoni yangeangaliwa. Inatakikana akili kutumia dawa ya kufaa kuponya akili za moyoni ambazo zimejeruhiwa.KN 222.2

  Watoto wanazo shida ngumu kuchukua uzito katika tabia sawa na zile za watu wazima kwa umri. Wazazi wenyewe hawaoni hivyo saa zote. Akili zao mara nyingi hutatizwa. Hufanya kazi wakiwa na maoni yaliopotoka. Shetani hushindana nao, nao hushindwa na majaribu yake, husema kwa ghadhabu, na kwa njia ya kuichochea hasira kwa watoto wao, na wakati mwingine ni wakali na wenye kunung’unika. Watoto hao, maskini, huambukizwa moyo huo huo, na wazazi hawako tayari kuwasaidia, maana wao ndio asili ya taabu hiyo. Wakati mwingine kila jambo huelekea kwenda vibaya. Kuna uchungu pande zote, na wote wana hali mbaya sana, na taabu. Wazazi huwalaumu watoto wao na kuwadhania kuwa ni wahalifu na wakaidi sana, watoto wabaya kabisa ulimwenguni, hali asili ya fujo hiyo ni wao wenyewe.KN 222.3

  Wazazi wengine huleta machafuko mengi kwa kukosa kuizuia hasira. Badala ya kuwauliza watoto kwa upole, kufanya hili au lile, huwaamuru kwa ukali, na mara hiyo kutoa midomoni mwao lawama na makaripio ambayo watoto hawakuyastahili. Wazazi, njia ya namna hiyo ikiruatwa kwa watoto wenu huharibu uchangamfu na nia yao ya kuendelea. Wanatimiza agizo lenu siyo kutokana na upendo, bali kwa sababu hawana la kufanya ila tu kulitimiza. Moyo wao haumo katika shauri hilo. Ni kazi ngumu isiyowapendeza, badala ya kuwa kitu cha kuwapendeza,. na hilo mara nyingi huwafanya kusahau kuyafuata maongozi yenu yote; hilo ni jambo lenye kuwaongezea uchungu, na kulifanya kuwa baya zaidi kwa. watoto. Lawama hurudiwa, na mwenendo wao mbaya kuwekwa mbele yao.KN 222.4

  Msiache watoto wenu kuwatazama kwa ghadhabu. Kama wakishindwa na majaribu, na baadaye kuona na kutubu kosa lao, wasameheni kwa urahisi kama mnavyotumaini kusamehewa na Baba yenu aliye mbinguni. Wafundisheni kwa wema, na kuwafungamanisha kwenye mioyo yenu. Ni wakati wa hatari kwa watoto. Mivuto itaenezwa kuwazunguka ili kuwafanya waachane nanyi, jambo ambalo hamna budi Kushindana nalo. Wafundisheni kuwafanya ninyi kuwa tuamini lao. Hebu wanong’one sikioni mwenu shida na furaha zao. Kwa kulitia nguvu jambo hilo mtawaepusha na mitego mingi ambayo Shetani ameiwekea tayari miguu yao isiyojua kitu. Msiwatendee watoto wenu kwa ukali tu, na kusanau utoto wenu ninyi wenyewe, na kukosa kukumbuka kwamba wao ni.watoto tu. Msiwatazamie kuwa wakamilifu wala kujaribu kuwafanya wanaume wazima au wanawake wazima kwa matendo yao mara moja. Kwa kufanya hivyo mtafunga mlango wa kuingilia ambao pengine mngeweza kuwa nao kwao, na kuwalazimisha kufungulia mlango mivuto yenye madhara, na kuacha wengine kutia sumu akili zao changa kabla ya ninyi kuamka na kuiona hatari yao. 231T 384 - 387;KN 223.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents