Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 38 - Mwito wa Kuwa na Kiasi Maishani

  AFYA ni mbaraka mkubwa mno, na ni yenye uhusiano sana na dhamiri ya moyoni na dini kuliko wengi wanavyojua. Inahusiana sana na uwezo wa mtu kazini, nayo yafaa kulindwa kwa kicho kama tabia; maana kadiri afya izidivyo kuwa kamili, ndivyo juhudi zetu zitakavyozidi kukamilika kwa ajili ya maendeleo ya kazi ya Mungu na kwa ajili ya mbaraka kwa wanadamu. 1CT 294;KN 242.1

  Mnamo Desemba 10, 1871, nalionyeshwa tena kwamba kuwa na kiasi ni mojawapo ya kazi kuu ambayo itawafanya watu wafae kwa kuja kwa Bwana. Inahusiana sana na ujumbe wa malaika watatu kama vile mkono unavyohusiana na mwili. Amri Kumi za Mungu zimedharauliwa na mwanadamu, lakini Bwana hapendi kuja kuwaadhibu waasi wa hiyo sheria bila kuwapelekea kwanza ujumbe wa onyo. Malaika wa tatu anahubiri ujumbe huo. Watu wangalitii hiyo sheria ya amri Kumi, na kutimiza maishani mwao kanuni za maagizo hayo, laana ya magonjwa yanayojaa sasa ulimwenguni isingalikuwako.KN 242.2

  Wanaume kwa wanawake hawawezi kuiasi sheria ya asili kwa kuiridhisha tamaa ya chakula iliyopotoka pamoja na tamaa mbaya za mwili, bila kuasi sheria ya Mungu. Kwa hiyo, Mungu ameruhusu nuru ya matengenezo ya kuwa na kiasi kutuzukia, kusudi tuweze kuona dhambi yetu katika kuziasi sheria ambazo ameziweka mwilini mwetu. Furaha au huzuni yetu yote yaweza kuonekana kwamba hutokana na utii ama uasi wa sheria ya asili. Baba yetu aliye mbinguni huona hali mbaya ya kusikitisha ya watu ambao wengine kwa makusudi lakini, wengi bila kujua, huishi kwa kuziasi sheria zilizowekwa na Mungu. Na kwa kuwapenda na kuwahurumia wanadamu, ameifanya nuru iangaze kwenye kanuni bora za matengenezo ya afya. Aitangaza sheria yake na adhabu ambayo itafuata kwa kuiasi, ili wote wapate kujifunza na kuwa waangalifu kuitii sheria ya asili. Ametangaza sheria yake wazi kabisa na kuitukuza hata imekuwa kama mji ulio juu ya mlima. Watu wote wanaohusika waweze kuifahamu kama wakitaka. Wajinga hawatakuwa na hatia kuidhihirisha sheria hii ya asili, na kusisitiza kuitii, ndiyo kazi inayofuatana na ujumbe wa malaika wa tatu kuwatayarisha watu kwa ajili ya kuja kwa Bwana. 23T 161;KN 242.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents