Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hatari ya Malezi Makali Mno

    Kuna watoto wa nyumba nyingi ambao huonekana kuwa wamepata malezi bora nyumbani; wakiwa bado chini ya malezi hayo; lakini jambo linalowaweka chini ya amri likivunjika, huelekea kwamba hawawezi kufikiri, kutenda, na kuamua mambo vizuri wao wenyewe.KN 218.1

    Malezi makali ya vijana bila ya kuwafundisha kufikiri na kutenda wao wenyewe kadiri ya uwezo wao na nia yao ilivyo, ili kwa njia hiyo waweze kukua mawazoni, na kuwa na maoni ya kujiheshimu nafsi, na kutumaini kutenda kwa uwezo wao wenyewe, yatazaa siku zote jamii ya watu walio dhaifu wa akili na wa tabia ya moyoni. Nao wakisimama ulimwenguni kutenda mambo kwa faida yao watadhihirisha ukweli kwamba walilelewa kama wanyama, wala hawakufundishwa. Nia zao, badala ya kuongozwa, zilishurutishwa kutii kwa utawala mkali wa wazazi na walimu. Hawa wazazi na walimu wanaojisifu kwamba wanao utawala kamili wa akili na nia za watoto walio chini yao wangeacha kujisifu kama wangeweza kuona maisha ya siku zijazo ya watoto hao ambao wametiishwa kwa nguvu ama kwa hofu. Hao karibu wote si tayari kushiriki kazi ngumu za madaraka za maisha. Walimu wa aina hiyo wanaoridhika kuwa wana karibu utawala kamili wa nia za wanafunzi wao si walimu wenye kufaulu sana, ijapokuwa mambo yanavyoonekana kwa muda mfupi yaweza kuwa yenye kusifiwa kuliko inavyostashili.KN 218.2

    Mara nyingi hunyamaza kimya, na kutumia madaraka yao kwa ukali, bila huruma; njia ambayo haiwezi kuipata mioyo ya watoto na wanafunzi wao. Ikiwa wangewakusanya watoto karibu nao, na kuonyesha kuwa wanawapenda, na kudhihirisha kupendezwa kwao katika bidii zote za watoto hata katika michezo yao na hata wakati mwingine kujifanya mtoto miongoni mwa watoto wangewafurahisha sana watoto na wangepata upendo wao na kuwafanya wawatumainie. Mara watoto wangeyaheshimu na kuyapenda madaraka ya wazazi na walimu wao.KN 218.3

    Pili haifai kuwaacha vijana kufikiri na kutenda kama wapendavyo wenyewe, bila kutegemea maoni ya wazazi na walimu wao. Yafaa watoto wafundishwe kuheshimu maamuzi ya wenye maarifa na kuongozwa na wazazi na walimu wao. Yawapasa wafundishwe ili nia zao zipate kuungana na nia za wazazi na walimu wao, na kuongozwa ili wapate kuona uzuri wa kulitii shauri lao. Ndipo wakitoka na kuachana na mkono wa kuwaongoza wa wazazi na walimu wao, tabia zao hazitakuwa kama unyasi utikiswao na upepo. 113T 132-135KN 218.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents