Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kitabu cha Vitabu

  Hali ya mtu ya maisha ya dini hudhihirishwa kwa aina ya vitabu anavyochagua kusoma wakati awapo na nafasi. Ili kuwa na hali njema akilini na kanuni thabiti za dini, vijana hawana budi kushirikiana na Mungu maishani kwa njia ya Neno lake. Likielekeza njia ya wokovu ipatikanayo kwa Kristo, Biblia hutuongoza kwenye maisha bora zaidi. Inayo historia ya kupendeza sana, tena yenye mafundisho mengi pamoja na maandiko ya habari za maisha ya watu wengi zaidi ya maandiko yoyote mengine. Wale ambao mawazo vao havajapotoka kwa kusoma hadithi za uongo wataona kuwa Biblia ni kitabu cha kupendeza kuliko vitabu vingine.KN 194.2

  Biblia ni kitabu cha vitabu. Kama unalipenda Neno la Mungu, na kulichunguza upatapo nafasi, ili upate hazina zake za thamani, na kutengenezwa kwa kila kazi njema, basi, uwe na hakika kuwa Yesu anakuvuta kwake. Lakini kuyasoma Maandiko Matakatifu kwa bahati, bila kutafuta kulifahamu fundisho la Kristo ili upate kuafikiana na masharti yake, hakutoshi. Kuna hazina ndani ya Neno la Mungu ambazo huweza tu kugunduliwa kwa kuchimba chini kabisa ya shimo la madini hayo ya kweli.KN 194.3

  Moyo wa tamaa za mwili hukataa ukweli; roho ya mtu aliyeondoka hupatwa na badiliko la ajabu. Kitabu kile ambacho kwanza kilikuwa hakipendezi kwa sababu kiliyafunua maneno ya kweli ambayo yalimkanusha mwenye dhambi, sasa huwa chakula cha kiroho, furaha na kitulizo cha maisha. Jua la haki huzitia nuru kurasa hizi takatifu, na Roho Mtakatifu huzitumia kusema na roho ya mtu huyo.KN 194.4

  Basi, wote wenye kuyapenda masomo hafifu, yasiyo na maana, sasa hawazielekezi akili zao kwenye neno hili lililo imara la unabii. Zitwaeni Biblia zenu, na kuanza kujifunza kwa moyo mpya Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na, Agano Jipya, kadiri mnavyosoma Biblia mara kwa mara, kwa moyo wa bidii, ndivyo itakavyozidi kuonekana kuwa nzuri, nanyi mtazidi kutopendezwa na masomo hafifu. Kazeni kitabu hiki cha thamini moyoni mwenu. Kitakuwa kwenu rafiki na kiongozi. 8 MYP 273, 274.KN 194.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents