Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujumbe Ambao Uliyaongoa Maisha

  Mwinjilist mmoja alifanya mikutano Bushnell, Michigan; lakini, mara baada ya ubatizo, akaondoka akawaacha watu bila kuwaweka imara waumini katika ujumbe huu. Pole pole watu wakakata tamaa na baadhi yao wakaanza tena mazoea yao mabaya. Mwishowe kanisa likawa dogo sana hata washiriki 10 au 12 waliosalia wakaamua kwamba haikuwa na maana kuendelea. Mara walipokwisha kutawanyika kutoka kwa mkutano walioudhania kuwa wa mwisho, wakapata barua kutoka posta na miongoni mwa barua ilikuwapo Review and Herald. Katika sehemu ya utaratibu wa mambo ya safari palikuwa na tangazo kuwa Mchungaji na Bibi White hawana budi kufika Bushnell kwa mikutano tarehe 20, Julai 1867. Tarehe hiyo ilikuwa baada ya juma moja tu. Watoto wakatumwa kuwaita watu warudi ambao walikuwa njiani kwenda zao nyumbani. Ikaamuriwa kwamba mtu mmoja anapaswa kutayarisha mahali penye miti na ya kuwa wote wamepaswa kuwaalika majirani zao, hasa washiriki waliorudi nyuma na kuiacha imani.KN 25.1

  Siku ya Sabato asubuhi, Julai 20, Mchungaji na Bibi White wakafika mahali hapa penye miti walimokusanyika watu sitini. Mchungaji White akahutubu asubuhi. Alasiri Ellen White akasimama kusema, lakini alipokwisha kusoma fungu lake, akaonekana anafadhaishwa na tatizo. Bila maneno ya kueleza zaidi akaifunga Biblia yake na kuanza kuzungumza nao kwa njia ya pekee sana.KN 25.2

  “Nikisimama mbele yenu alasiri hii, nazitazama nyuso za wale nilioonyeshwa katika njozi miaka miwili iliyopita. Nikiziangalia nyuso zenu mambo yenu nayakumbuka vizun, nami nina ujumbe kwenu kutoka kwa Mungu.KN 25.3

  “Kuna ndugu huyu karibu na huu msunobari. Siwezi kulitaja jina lako maana sikujulishwa, lakini uso wako naujua, na mambo ya maisha yako ya dhaniri mbele yangu.” Kisha akasema na ndugu huyu juu ya kuacha dini kwake na kuyarudia mazoea mabaya. Akamtia nguvu kurudi na kutembea pamoja na watu wa Mungu. Kisha akamgeukia mwanamke mmoja katika sehemu nyingine ya makutano, akasema, “Dada huyu mwenye kuketi karibu na Bibi Myanard wa kanisa la Greenville-Siwezi kulitaja jina lako kwa sababu sikuambiwa ni jina gani-lakini, miaka miwili iliyopita nalionyeshwa mashauri juu yako katika njozi, na mambo ya maisha yako nayajua.” Ndipo Mama White akamtia moyo mwanamke nuyu.KN 25.4

  “Tena kuna ndugu kule nyuma karibu na mti Ulaya (Muoki). Siwezi kukutaja jina lako pia, kwa kuwa sijakutana nawe bado, lakini mashauri yako ni dhahiri kwangu.” Kisha akasema habari za ndugu huyu, akimfunulia kila mmoja aliye kuwako pale mawazo yake ya moyoni na kumwambia mambo ya maisha yake.KN 25.5

  Na kutoka kwa mtu mmoja hata kwa mwingine aliwageukia makutano, akiwaambia mambo aliyoonyeshwa miaka miwili iliyokuwa umepita katika njozi. Ellen White alipokuwa amemaliza mahubiri yake, ambayo yalihusisha maneno ya kukaripia na hata maneno ya kutia moyo, akaketi. Mmoja miongoni mwa makutano akasimama, akasema, “Nataka kujua kama mambo ambayo Ellen V/hite ametuambia alasiri hii ni kweli. Mchungaji na Mama White hawayajui hata majina ya wengi wetu, lakini amefika hapa alasiri hii na kutwambia kuwa miaka miwili iliyopita alipewa njozi ambayo kwayo alionyeshwa mashauri yetu, tena akasema nasi kila mmoja mambo hayo moja moja, akimfunulia kila mmoja aliyeko hapa mwenendo wetu na mawazo yetu ya moyoni. Mambo haya ndivyo yalivyo kwa kweli kwa kila mmoja? Au Ellen White amekosea? Nataka kujua.”KN 26.1

  Watu mmoja mmoja wakasimama. Yule mtu aliyekuwa karibu na msunobari akasimama, na kusema Ellen White alikuwa ameeleza mashauri yake vizuri zaidi kuliko yeye mwenyewe angalivyoweza kuyaeleza. Akaungama upotovu wake. Akaonyesha nia yake karibu na kuenenda na watu wa Mungu. Mwanamke aliyeketi karibu na Bibi Maynard kutoka kanisa la Greenville pia alitoa ushuhuda. Akasema kuwa Ellen White amesimulia mambo ya maisha yake vizuri kuliko yeye mwenyewe angalivyoweza kuyasimulia. Yule mwanamume karibu na mti Ulaya, ambaye Ellen White alimkaripia na kumwambia maneno ya kumtia moyo akasema kwamba Ellen White alikuwa ameyaeleza mashauri yake vizuri kuliko yeye mwenyewe angalivyoweza kuyaeleza. Maungamo yakafanywa Dhambi zikaachwa. Roho wa Mungu akaingia, na pakawa na uamsho Bushnell.KN 26.2

  Mchungaji na Mama White wakarudi tena Sabato nyingine iliyofuata, na pakafanywa ubatizo, na kanisa la Bushnell likaimarishwa vizuri na likawa na nguvu.KN 26.3

  Mungu aliwapenda watu wake wa Bushnell kama awapendavyo wale wote wanaomtazamia. Lile Neno lisemalo “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu” (Ufu. 3:19), halina budi kuwa neno lililowaingia moyoni baadhi ya wale waliokuwako. Watu walipojiona mioyoni mwao wenyewe kama Bwana alivyowaona, wakafahamu hali yao halisi na kutamani uongofu maishani mwao. Hili ni kusudi halisi la njozi nyingi alizopewa huyu Ellen White.KN 26.4

  Mara baada ya kufa kwa Mchungaji White, Mama White akakaa karibu na Healdsburg College. Wasichana kadha wa kadha wakawa wanakaa nyumbani mwake walipokuwa wakihudhuria Chuo. Ilikuwa desturi wakati ule kuvaa wavu mwepesi juu ya nywele ili kuziweka vizuri kwa taratibu mchana kutwa. Siku moja mmoja wa wasichana hawa alipokuwa akipita chumbani mwa Mama White akauona wavu wa nywele uliokuwa umetengenezwa vizuri ambao aliutaka. Akidhani kuwa hautahitajika, akautwaa na kuuweka ndani ya sanduku lake. Baadaye kidogo Mama White alipokuwa akivaa ili atoke, akaukosa wavu wake na ikambidi kwenda bila kuwa nao. Jioni watu wa nyumbani mwake walipokuwa pamoja, Mama White akauliza juu ya wavu wake uliopotea, lakini nakuna hata mmoja aliyeonyesha kuwa anajua ulipo.KN 26.5

  Siku moja baadaye Bibi White alipokuwa akipita chumbani mwa wasichana hawa, sauti fulani ikamwambia, “Fungua sanduku lile.” Kwa sababu sanduku hili halikuwa lake, hakupenda kufanya hivyo. Alipoamriwa mara ya pili akaitambua ile sauti kuwa ni ya yule malaika. Alipoinua kifuniko akaona sababu iliyomfanya yule malaika aseme, maana pale palikuwa na ule wavu wake. Watu wa nyumbani mwake walipokutanika tena Mama White akauliza tena juu ya wavu huu, akisema kuwa usingeweza kutoweka wenyewe. Hakuna aliyesema neno hivyo Mama White akaacha shauri hili.KN 27.1

  Siku chache baadaye Mama White alipokuwa anapumzika kutoka katika kuandika akapewa njozi fupi sana. Akauona mkono wa msichana ukishusha wavu wa nywele kwenye taa inayotumia mafuta. Wavu huo ulipogusa mwali wa moto ukatoweka ghafula motoni. Huu ukawa ndio mwisho wa njozi hii.KN 27.2

  Watu wa nyumbani mwake walipokutanika tena Mama White akakaza shauri lile la kupotea kwa ule wavu wa nywele tena, lakini hata hivyo hapakuwako na ungamo lo lote wala hakuna mtu ye yote aliyeelekea kujua ulipo. Ndipo baadaye kidogo Mama White akamwita kando msichana huyu akamwambia habari za ile sauti, na kile alichoona ndani ya sanduku na akamwambia habari za ile njozi fupi ambayo kwayo aliona wavu wa nywele ukiteketea juu ya taa. Akiwa na habari zote hizi mbele yake, yule msichana akaungama kuwa aliuchukua wavu huu, na kuuchoma moto asije akagundulika. Akakiri kosa lake na kulisawazisha shauri lake na Mama White na Mungu pia.KN 27.3

  Pengine tutafikiri kuwa hili ni jambo dogo sana kwa Mungu kulihangaikia-wavu tu wa nywele. Lakini lilikuwa jambo la maana sana kuliko thamani ya kitu chenyewe kilichoibiwa. Hapa alikuwako msichana, mshiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato. Aliyejiona moyoni mwake kuwa yu salama, lakini hakuziona hitilafu katika tabia yake mwenyewe, hakuona moyo wa kujichunguza nafsi, wala si wengine, ambao ulimwongoza kuiba na kudanganya. Sasa alipofahamu jinsi mambo yalivyo na maana-kwamba Mungu angempa njozi mjumbe wake mwenye kazi nyingi hapa duniani kwa ajili ya wavu wa nywele tu-huyu msichana akaanza kufahamu jinsi mambo yalivyo hasa. Jambo hili likawa la kumbadilisha maishani mwake, naye akaishi maisha ya raha, ya Mkristo mnyofu.KN 27.4

  Hiyo ndiyo sababu ya Mama White kupewa njozi. Ijapokuwa maneno mengi ya shuhuda yaliyoandikwa na Mama Wnite yalikuwa kwa ajili ya kueleza au kudhihirisha mambo maalumu sana Lakini, yanaonyesha kanuni zinazotimiza haja za Kanisa hili katika kila nchi ulimwenguni. Mama White amedhihirisha kusudi na mahali pa shuhuda hizi kwa maneno haya:KN 28.1

  “Shuhuda hizi zilizoandikwa si za kutoa nuru mpya, bali za kuyakaza mioyoni maneno ya kweli yaliyotolewa kwa uongozi wa Roho wa Mungu ambayo yamekwisna kufunuliwa tayari. Wajibu mkubwa kwa Mungu na kwa wanadamu wenzake umpasao mtu umedhihirishwa katika Neno la Mungu; walakini ni wachache wenu tu wenye kuitii nuru iliyotolewa. Hapakutolewa neno la kweli lingine zaidi, bali Mungu kwa njia ya shuhuda hizi ameyarahisisha maneno ya kweli yaliyokwisha kutolewa tayari Shuhuda hizi hazipaswi kupunguza ukuu wa Neno la Mungu, bali kulikuza, na kuivuta mioyo ya watu kwalo, ili wepesi mzuri wa ukweli upate kuwaingia wote moyoni.”KN 28.2

  Katika maisha yake yote Mama White alilishika Neno la Mungu mbele ya watu. Kitabu chake cha kwanza kabisa alikifunga kwa wazo hili. Alisema:KN 28.3

  “Nakupa shauri, msomaji mpendwa, Neno la Mungu ni kanuni ya imani yako na ibada. Kwa Neno hilo hatuna budi kuhukumiwa. Mungu, katika Neno hilo, ameahidi kutoa njozi “Siku za mwisho”; si kwa ajili ya kanuni mpya ya imani, bali kwa ajili ya faraja ya watu wake, na kutoa makosa ya wale wanaopotoka katika ukweli wa Biblia.”KN 28.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents