Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kujiweka Tayari Kumlaki Kristo

    WAADVENTISTA Wasabato wote hutazamia sana wakati Yesu atakapokuja kuwaehukua kwenda kwenye makao mazuri ambayo amekwenda kuwaandalia. Katika yale makao ya mbinguni hapatakuwapo dhambi tena, wala huzuni, wala njaa, wala umaskini, wala ugonjwa, wala mauti. Mtume Yohana alipofikiri juu ya majaliwa haya yanayowangojea waaminifu hakuweza kujizuia kusema: “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu Sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye.” - (1 Yohana 3:1, 2.)KN 8.1

    Kufanana na Yesu katika tabia ndilo kusudi la Mungu kwa watu wake. Tangu mwanzo ulikuwa mpango wa Mungu kwamba wanadamu, walioumbwa kwa sura yake, wakuze tabia zinazofanana na tabia yake Mungu. Ili kulitimiza hili, wazazi wetu wa kwanza katika Edeni walipaswa kupokea mafundisho kutoka kwa Kristo na malaika kwa kuongea nao uso kwa uso. Lakini baada ya mwanadamu kutenda dhambi hakuweza tena kuzungumza kama apendavyo na malaika kwa jinsi hii.KN 8.2

    Kusudi mwanadamu asiachwe pasipo mwongozo, Mungu alichagua njia zingine za kufunua mapenzi yake kwa watu wake, ambazo mojawapo na iliyo kuu ni njia ya manabii - wanaume na wanawake ambao wamepokea na kupeleka mbele ya watu wa Mungu ujumbe aliopenda wauchukue. Mungu aliwaeleza Waisraeli, “Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, mtajifunua kwake katika maono, nitasema naye katika ndoto.” - (Hesabu 12:6.)KN 8.3

    Ni kusudi la Mungu kuwa watu wake wawe wajuzi na waongofu, wakijua na kufahamu licha ya nvakati wanamoishi, bali hata zile zijazo. “Hakika Bwana Mungu natafanya neno lo lote, Bila kuwafunulia utumishi wake manabii siri yake.” (Amosi 3:7) Hili huwatofautisha watu wa Mungu “wana wa nuru”, (1 The. 5:5). Na watu wa ulimwengu huu.KN 8.4

    Kazi ya nabii siyo kutabiri tu. Musa, nabii wa Mungu aliyeandika vitabu sita vya Biblia, aliandika maneno machache ya wakati ujao. Kazi yake imeelezwa na Hosea dhahiri zaidi, “Na kwa nabii Bwana alimtoa Israeli katika Misri, na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.” (Hosea 12:13).KN 8.5

    Nabii si mtu anayewekwa na wanadamu wenzake, wala si mtu anayejiweka mwenyewe. Uchaguzi wa mtu ambaye hana budi kuwa nabii uko mikononi mwa Mungu tu,ambaye peke yake aweza kuona na kujua moyo wa mwanadamu. Ni jambo la maana kwamba katika historia ya watu wa Mungu, wanaume kwa wanawake pia mara nyingi wamechaguliwa na Mungu kusema badala yake.KN 8.6

    Manabii hawa, wanaume na wanawake waliochaguliwa na Mungu wawe njia ya kutuletea habari za Mungu, wamenena na kuandika mambo ambayo Mungu amewafunulia katika njozi takatifu. Neno la Mungu lenye thamani lina ujumbe wao. Kwa njia ya manabii hawa wanadamu wameongozwa kufahamu vita ambayo inaendelea kwa ajili ya roho za watu, vita baina ya Kristo na malaika zake na Shetani na malaika zake. Tunaongozwa kuifahamu vita hii katika siku za mwisho za dunia, na njia zilizotolewa na Mungu kuihifadhi kazi yake na kuzikamilisha tabia za washiriki ambao watakuwa lile kundi la wanaume na wanawake wanaongojea kumlaki Bwana wao.KN 9.1

    Mitume, waandishi wa mwisho wa Biblia wametupa maelezo dhahiri ya matukio ya siku za mwisho. Paulo aliandika juu ya “nyakati za hatari”, na Petro ameonya juu ya “watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, wakiuliza, “Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake?” Kanisa wakati huu halina budi kuwa vitani maana Yohana alimwona Shetani “akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia.”KN 9.2

    Hawa waandishi wa Biblia waliona kuwa lilikuwa kusudi la Mungu kutoa nuru ya pekee na msaada kwa watu wake kabla ya Yesu kuja.KN 9.3

    Paulo asema kuwa kanisa lenye kutarajia na kungojea kuja kwa Kristo - Kanisa la Waadventista Wasabato Sabato - halitapungukiwa na karama iwayo yote (1 Wakor. 1:7, 8). Litakuwa lenye umoja, hai, na lenye uongozi kama mitume, manabii, wainjilisti, wacnugaji na walimu. (Waefeso 4:11).KN 9.4

    Mtume Yohana huwatambulisha washiriki wa kanisa la siku za mwisho, “kanisa la masalio”, kama wale “wazishikao amri za Mungu” (Ufunuo 12:17). Pia kanisa hili litakuwa lenye “ushuhuda wa Yesu”, ambao ni “Roho ya Unabii”. (Ufunuo 19:10).KN 9.5

    Basi ni dhahiri kuwa kwa mpango wa Mungu kanisa la Waadventista Wasabato - kanisa la unabii, lilipoanza kuwako, lilikuwa na Roho ya Unabii miongoni mwake. Lilikuwa jambo la kufaa kama nini kwa Mungu kusema na watu wake duniani siku za mwisho za dunia kama alivyokuwa amesema na watu wake nyakati za haja maalum kame nyingi zamani.KN 9.6

    Na kanisa hili la unabii - kanisa la Waadventista Wasabato - lilipoanza wakati huo huo hasa liliainishwa na unabii, wa miaka mia moja na zaidi kidogo sauti ikasikika miongoni mwetu, ikisema, “Mungu amenionyesha katika njozi takatifu.”KN 9.7

    Haya si maneno ya kujisifu, bali usemi wa kijana mwanamke mwenye umri wa miaka kumi-na-saba ambaye alikuwa ameitwa kusema kwa ajili ya Mungu. Katika muda wote wa miaka sabini ya kazi yake ya uaminifu sauti ile ilisikika miongoni mwetu, ikiongoza, ikisahihisha, ikifundisha. Na sauti ile ingali ikisikika hata leo kwa njia ya kurasa maelfu zilizotufikia za maandishi ya mjumbe aliyechaguliwa na Mungu, Ellen G White.KN 9.8

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents