Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Masomo Yanayoharibu Roho ya Mtu

    Kwa ajili ya wingi wa vitabu na magazeti vinavyomiminika daima kutoka katika mitambo ya kuchapisha wazee kwa vijana hufanya mazoea ya kusoma haraka-haraka na kwa juu juu tu, na hivyo ubongo hupoteza uwezo wake wa kupokea mawazo yaliyounganika na yenye nguvu. Juu ya hayo, sehemu kubwa ya magazeti na vitabu ambavyo, kama vyura wa Misri, vinatapakaa ncnini, sio kwamba ni vya hali ya chini tu, visivyofaa, na vyenye kudhoofisha, bali ni vichafu na vyenye kuaibisha. Matokeo yake siyo kulevya na kuharibu akili tu, bali kuchafua na kuangamiza roho. 3 Ed. 189, 190KN 192.4

    Katika mafundisho ya watoto na vijana, hekaya, hadithi za kizimwi, na hadithi za uongo sasa zinapewa nafasi kubwa. Vitabu vya namna hiyo hutumika shuleni, navyo hupatikana nyumbani mwa watu wengi. Wazazi ambao ni Wakristo huwezaje kuwaruhusu watoto wao kutumia vitabu vilivyojaa uongo jinsi hii? Watoto wakiuliza maana ya hadithi hizo ambazo ni kinyume cha mafundisho ya wazazi wao, hujibiwa kuwa hadithi hizo si za kweli; lakini hili halisaidii kuwaepusha na matokeo mabaya ya kuzitumia. Mawazo yatolewayo katika vitabu hivyo huwapotosha watoto. Huingiza maoni ya uongo ya maisha na kuzaa pamoja na kuchochea tamaa ya mambo yasiyo ya hakika, ya kuwaziwa tu.KN 192.5

    Kamwe vitabu vyenye kuipotosha kweli visiwekwe mikononi mwa watoto au vijana. Watoto wetu wanapojielimisha kwa njia hii, wasiruhusiwe kuwa na mawazo ambayo yatakuwa mbegu za dhambi. 4 CT 384, 385;KN 193.1

    Chimbuko lingine la hatari ambalo twapaswa kujihadhari nalo siku zote ni kusoma vitabu vilivyotungwa na makafiri. Vitabu vya namna hiyo huandikwa kwa uongozi wa yule adui wa ukweli, na hakuna mtu awaye yote awazaye kuvisoma bila kuihatarisha roho. Kwa kweli wengine wanaoathirika na vitabu hivyo hatimaye huweza kupona; wote wanaojituliza kwa mvuto mbaya wa vitabu hivyo hujiweka katika milki ya Shetani, nave huwafaidi sana. Wakiyakaribisha majaribu yake jinsi hiyo, hawana hekima ya kupambanua wala nguvu za kuyapinga. Kwa uwezo wa mivuto ya uzuri unaopoteza akili, kutoamini na ukafiri huimarika akilini. 5 CA 135, 136;KN 193.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents