Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Onyo kwa Wale Watafutao Ahadi ya Kukubaliwa na Mungu

    Wawezaje kujua kuwa umekubaliwa na Mungu? Jifunze neno lake kwa kuomba kwa bidii. Usiliweke kando kwa ajili ya kitabu kingine. Kitabu hiki huhakikisha hatia ya dhambi. Huidhihirisna wazi njia ya wokovu. Hufunua ijara yenye utukufu ung’aao. Hukufunulia Mwokozi kamili, na kukufundisha kuwa kwa njia ya rehema zake zisizo na kikomo pekee waweza kuutazamia wokovu.KN 64.3

    Usipuuzie maombi ya faragha, kwa kuwa ni moyo wa dini. Kwa kusali kwa bidii, daima, omba usafi wa moyo. Omba kwa bidii, omba sana, kama ambavyo ungefanya iwapo ungekuwa hatarini kufa. Dumu mbele za Mungu mpaka shauku lfanywe ndani yako kutamani wokovu, na ushahidi uwepo ndani yako kuwa umesamehewa dhambi. 141T 163;KN 64.4

    Yesu hakukuacha kushangazwa na taabu na shida unazokutana nazo. Amekwisha kukuambia habari zake zote, na amekwambia pia usiangushwe chini na kulemewa taabu zikupatapo. Mtazame Yesu, Mkombozi wako, ufurahi na kushangilia. Taabu kubwa mno za kustahimili ni zile zitokazo kwa ndugu zetu, rafiki zetu wenyewe; lakini hata taabu hizi twaweza kuzistahimili kwa uvumilivu. Yesu halali ndani ya lile kaburi jipya la Yusufu. Amefufuka naye amepaa juu mbinguni, huko ili kutuombea. Tunaye Mwokozi aliyetupenda sana hata akatufilia, ili kwa njia yake tupate kuwa na matumaini na nguvu na moyo, na nafasi, ya kukaa pamoja naye juu ya kiti chake cha enzi. Aweza na anapenda kukusaidia umwitapo.KN 64.5

    Je, unaona moyoni upungufu wako kwa cheo cha kazi ya madaraka uliyoaminiwa? Mshukuru Mungu kwa ajili hiyo. Kadiri uzidivyo kuuona udhaifu wako, ndivyo utakavyoelekea kutafuta msaidizi. “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.” Yesu anataka mwe wenye furaha, mwe wachangamfu. Anawataka mfanye mwezavyo kwa uwezo na Mungu, kisha mmwamini Bwana kuwasaidia na kuwainua wale ambao watakuwa wasaidizi wenu katika kuichukua mizigo.KN 64.6

    Maneno makali ya watu yasikutie uchungu. Je, watu hawakusema maneno makali juu ya Yesu? Unakosea, na wakati mwingine unatoa nafasi kwa maneno yasiyofaa. Usitazamie fungu zuri zaidi maisha haya kuliko lile Mfalme wa fahari alilokuwa nalo. Maadui zako wakiona kuwa wanaweza kukutia uchungu, watafurahi, na Shetani atafurahi. Mtazame Yesu, na kufanya kazi kwa nia moja ukiuangalia utukufu wake. Ulinde moyo wako katika upendo wa Mungu. 158T 128, 129;KN 65.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents