Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kristo Huwapa Wanadamu Uwezo wa Kufanyika Watoto wa Mungu

    Hebu tuyachunguze maneno yale Kristo aliyosema ghorofani usiku kabla ya kusulibiwa kwake. Alikuwa akiikaribia saa yake ya jaribio naye alijaribu kuwafariji wanafunzi wake, ambao iliwabidi kujaribiwa sana.KN 88.1

    Wale wanafunzi walikuwa hawajayafahamu maneno ya Kristo juu ya uhusiano wake na Mungu. Mengi miongoni mwa mafundisho yake yalikuwa yangali giza kwao. Walikuwa wameuliza maswali mengi yaliyoonyesha kutojua kwao uhusiano wao na Mungu na juu ya rikra zao za mambo ya sasa na yale ya baadaye. Kristo alitaka sana wawe na ujuzi dhahiri zaidi juu ya Mungu.KN 88.2

    Siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu alipomiminwa juu ya wanafunzi, wakafahamu maneno ya kweli ambayo Kristo alikuwa ameyasema kwa mithali. Mafundisho ambayo yalikuwa mafumbo kwao yakadhihirishwa. Ufahamu walioupata kwa kumiminwa kwa Roho uliwafanya kuona aibu juu ya mafundisho yao ya upuzi. Mawazo na maelezo yao yalikuwa upumbavu yakilinganishwa na hekima ya mambo ya mbinguni ambayo sasa waliyapokea. Waliongozwa na Roho, na nuru iliangaza ufahamu wao ambao ulikuwa gizani.KN 88.3

    Lakini wale wanafunzi walikuwa bado hawajapokea utimizaji kamili wa ahadi ya Kristo. Walipokea ujuzi wote wa Mungu ambao waliweza kustahimili, lakini utimizaji kamili wa ahadi ambayo Kristo angependa kuwaonyesha dhahiri juu ya Baba ulikuwa bado kuja. Ndivyo ilivyo leo. Ujuzi wetu juu ya Mungu ni sehemu tu na si kamili. Shindano litakapokwisha, na yule Mtu Kristo Yesu akiwakiri mbele za Baba watenda kazi wake waaminifu, ambao, katika ulimwengu wa dhambi, wamemshuhudia kwa kweli, watafahamu dhahiri mambo ambayo hivi sasa ni mafumbo kwao.KN 88.4

    Kristo alichukua mbinguni ubinadamu wake uliotukuzwa. Huwapa wale wanaompokea, uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ili mwishowe Mungu apate kuwapokea kama walio wake, kukaa pamoja naye milele. Kama, katika maisha haya, ni waaminifu kwa Mungu, hatimaye “watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao” (Ufunuo 22:4). Ni furaha gani ya mbinguni zaidi ya kumwona Mungu? Furaha gani kuu atakayoipata mwenye dhambi aliyeokolewa kwa neema ya Kristo zaidi ya kuutazama uso wa Mungu na kumtambua kama Baba?KN 88.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents