Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hatari ya Kuzilaumu Shuhuda Hizi

  Katika ndoto ya hivi karibuni naliletwa mbele ya mkutano wa watu wengi, ambao wengine wao walikuwa wakijitahidi kuondoa maneno yenye kuchoma moyo ya ushuhuda mzito sana wa onyo ambalo nimewapa. Wakasema: “Twaziamini shuhuda za Bibi White; lakini anapotwambia mambo ambayo hakuyaona wazi katika njozi katika jambo fulani lenye kufikiriwa, maneno yake hayawi na maana zaidi kwetu kuliko maneno ya mtu awaye yote mwingine.” Roho wa Bwana, alinijia, nami nikaondoka na kuwakaribia katika jina la Bwana.KN 110.4

  Sasa kama wale ambao maonyo haya mazito yananenwa kwao, husema, “Ni mawazo yas Bibi White mwenyewe, itanibidi kufuata vile nionavyo mimi mwenyewe,” na kama wakiendelea kutenda mambo yale waliyoonywa kutoyatenda, huonyesha kuwa hulidharau shauri la Mungu, na matokeo yake ni yale tu ambayo Roho wa Mungu amenionyesha yangekuwa madhara kwa kazi ya Mungu na uharibifu kwao wao wenyewe. Wengine watakao kuimarisha hali yao wanayoyadhania kuwa yatasaidia maono yao, na watayatilia mkazo iwezekanavyo; lakini kile ambacho huhoji mwendo wao, au ambacho hakipatani na maoni yao, hukitaja kuwa ni mawazo ya Bibi White, wakikana kuwa hakikutoka mbinguni na kukisawazisha na maoni yao wenyewe.KN 110.5

  Basi, ndugu nawasihi msijitie kati yangu na watu, na kuikinga nuru ambayo Mungu apenda iwafikie. Kwa lawama zenu msiziondolee nguvu zote, maana zina uwezo wote hizi Shuhuda. Msijione moyoni kuwa mwaweza kuzichungua ili zifae mawazo yenu wenyewe, mkidai kuwa Mungu amewapa uwezo kufahamu kile kilicho nuru kutoka mbinguni na kile kilicho maneno tu ya hekima ya mwanadamu. Kama Shuhuda hizi hazisemi sawasawa na Neno la Mungu, zikataeni. Krito na Beliari hawawezi kuunganishwa. Kwa ajili ya Kristo msizitatanishe akili za watu kwa werevu na moyo wa wanadamu, wa kuonea mashaka na kuifanya kazi hii isiwe na matokeo yo yote mema ambayo Mungu ataka kufanya. Kwa kukosa busara za kiroho, usifanye hii njia ya Mungu jiwe la kujikwaza ambapo wengi watafanywa wajikwae na kuanguka, “na kunaswa na kuchukuliwa.” 105T 687-691;KN 111.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents