Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Urafiki na Mazoea Mema

  Vijana wanaotupwa au kuachwa kwenye jamii wao kwa wao huweza kufanya urafiki wao kuwa mbaraka au laana. Huweza kuadilisha, kuneemesha, na kutiana nguvu, kuendelea vizuri katika mwenendo, katika tabia, katika maarifa; au, kwa kukubali kuwa wazembe na kutokuwa waaminifu, waweza kutoa tu mvuto wa upotevu.KN 184.5

  Yesu atakuwa msaada wa wote wanaomtumainia. Wale wenye uhusiano na Kristo wanaweza kufurahi wapendavyo. Huifuata njia ambayo mwokozi huwaongoza, kwa ajili yake kuisulibisha nafsi pamoja na anasa na tamaa mbaya za mwili. Watu hao wanayo matumaini juu ya Kristo, na dhoruba za dunia hazina nguvu kuwaondoa kwenye msingi imara.KN 184.6

  Ni juu yenu, vijana wa kiume na wa kike kama mkipenda kuwa watu wa kuamimwa, wema na wa kufaa hasa. Yafaa mwe tayari na kukusudia kusimama imara kuitetea kweli kwa hali iwayo yote. Mazoea yetu mabaya hayawezi kutwaliwa mbinguni pamoja nasi, na tusipoyashinda hapa, yatatufungia nje ya makao ya wenye haki. Mazoea mabaya yakipingwa, yatakuwa na ugumu; lakini kama vita ikifululizwa kwa nguvu na bidii, yanaweza kushindwa.KN 184.7

  Ili kuwa na mazoea mema, yatupasa kutafuta marafiki wenye tabia ya uadilifu na mvuto wa dini. 104T 655;KN 184.8

  Ikiwa vijana wangeweza kuvutwa kufanya urafiki na kuwa waangalifu na wenye tabia nzuri, matokeo yangekuwa mazuri sana. Kama ukifanywa uchaguzi wa marafiki wamchao Bwana, mvuto huo utaongoza katika ukweli, wajibu, na utakatifu. Maisha ya Kikristo ni uwezo kwa mema. Lakini, kwa upande mwingine, wale wafanyao urafiki na wanaume na wanawake wenye tabia za mashaka watakuwa wenye mashaka pia; mwenye kuchagua marafiki waovu bila shaka atakuwa mwovu. Kwenda katika shauri la wasio haki ni hatua ya kwanza kabla ya kusimama katika njia ya wakosaji na kuketi barazani pa wenye mizaha.KN 185.1

  Hebu wote wapendao kufanya tabia njema wachague marafiki wenye akili na busara na ambao hupenda mambo ya dini. Wale ambao wamehesabu gharama wanaotaka kujenga kwa ajili ya uzima wa milele wanapaswa kutia vifaa bora kwenye jengo lao. Kama wakikubali mbao zilizooza, kama wakiridhika na upungufu wa tabia, jengo litaangamia. Watu waangalie jinsi wajengavyo. Dhoruba ya majaribu italipitia jengo hilo, na kama halikujengwa imara na kwa uaminifu halitasahimili jaribio.KN 185.2

  Sifa njema ni yenye thamani kushinda dhahabu. Vijana wanayo maelekeo ya kushirikiana na wale wenye nia na tabia mbaya. Ni furaha gani hasa kijana awezayo kuitazamia kwa kujiunga kwa hiari yake na watu wenye mawazo, maoni, na mwenendo mbovu, usio na maana? Wengine wamepotoka kwa tamaa na ni wenye mazoea mabaya, na wote wachaguao marafiki wa namna hii watakifuatta kielelezo chao. 114T 587; 588;KN 185.3

  Pengine huwezi kuona hatari hasa katika kuchukua hatua ya kwanza ya upuzi na kujitafutia anasa nawe wafikiri kuwa utakapotaka kubadili mwenendo wako, utaweza kufanya mema kwa urahisi tu kama ilivyokuwa zamani kabla hujashindwa na mabaya. Lakini hili ni kosa. Kwa kuchagua rafiki wabaya wengi wamepotoshwa hatua kwa hatua kuiacha njia ya sifa njema na kuingizwa katika kutokutii na upotevuni, ambapo wakati mwingine waweza kuzama ndani yake. 12CT 224;KN 185.4

  Msidhani kwamba Mungu anataka tuache kila kitu ambacho ni cha maana kwa raha yetu hapa. Atakacho tukiache ni kile ambacho hakitatunufaisha wala kuidumisha furaha yetu. 13AH 502; Pumziko Kamili na KujifurahishaKN 185.5

  Vijana wangekumbuka kuwa wanapaswa kutoa habari za majaliwa yote ambayo wamefaidi, na kwa kutumia kwa faida wakati wao, na kwa kutumia vizuri uwezo wao. Pengine watauliza, Je, tusiwe na michezo wala maburudisho? Tufanye kazi tu kila mara bila kuwa na badiliko? 14CT 337;KN 185.6

  Kubadili kazi ya juhudi ambayo imezitumikisha nguvu za mwili kupita kiasi pengine italazimu sana kwa muda, ili wapate kushughulika tena na kazi kwa bidii na kufaulu vizuri zaidi.KN 185.7

  Lakini kupumzika kabisa huenda hakutalazimu au hata hakutakuwa na matokeo mazuri baadaye kwa habari za nguvu zao za mwilini. Hawana sababu, hata wakichoka na kazi ya aina moja, kupoteza bure dakika zao zenye thamani. Pengine watataka kufanya kitu kingine ambacho hakiwachoshi hivyo, lakini kitakachowaletea mama na dada zao furaha. Katika kuyapunguza masumbuko yao kwa kujitwika wenyewe mizigo migumu kabisa wapaswayo kuibeba, wataweza kupata maburudisho ambayo hutokana na tabia na ambayo yatawapa furaha kamili, na wakati wao hautakuwa wa kupotezwa bure kwa mambo yasiyo na maana wala kwa kujipendeza nafsi wenyewe, kwa anasa. Wakati wao daima waweza kutumiwa kwa faida, wakiburudishwa kwa mambo mbalimbali, huku wakiukomboa wakati kusudi kila dakika iwe na faida kwa mtu fulani. 153T 223;KN 186.1

  Wengi hudai kwamba inalazimu kwa ajili ya kuhifadhi afya ya mwili kujifurahisha kwa machezo. Ni kweli kwamba kubadili kunatakikana kwa faida ya maendeleo ya mwili, maana akili na mwili huburudishwa na kutiwa nguvu na badiliko; lakini kusudi hili halitimizwi kwa kujifurahisha kwa anasa zisizo na maana, kwa kuacha kazi za kila siku ambazo vijana wangetakiwa kuzitenda. 16AH( 1) KN 186.2

  Jumba la maonyesho (theater) ni mojawapo ya mahali penye hatari sana pa anasa. Badala ya kuwa shule ya tabia ya uadilifu na sifa njema kama inavyosemekana kila mara, ni mahali pa maovu hasa. Maozoea mabaya na mwelekeo wa dhambi hutiwa nguvu na kuimarishwa kwa michezo hiyo. Nyimbo za ovyo, ufisadi wa matendo, maneno, na moyo huharibu akili na kushusha tabia. Kila kijana mwenye mazoea ya kwenda mahali pa maonyesho ya jinsi hii ataharibika tabia. Hakuna mvuto nchini mwetu wenye nguvu kutia akili sumu, kuharibu maoni ya ndani, na kupunguza nguvu za kupendezwa na starehe na utulivu halisi wa maisha zaidi ya michezo ya sinema. Kuyapenda mambo haya huzidisha kila anasa sawa na tamaa ya kileo inavyotiwa nguvu kwa kukitumia. Njia tu ya salama ni kuepukana na jumba la maonyesho(theater), kiwanja cha tamsha, na kila pahali pa machezo hiyo isiyofaa. 17CT 334, 335;KN 186.3

  Kucheza kwa Daudi kwa moyo wa kicho mbele za Mungu kumetajwa na wale wapendao anasa, lakini hoja ya namna hii haina maana. Siku hizi kucheza dansi kumeungana na upuzi na kujifurahisha usiku wa manane. Afya na tabia ya uadilifu hutupwa makusudi kujifurahisha na anasa. Kwa wazoefu wa chumba cha dansi Mungu siye awazwaye wala kuheshimiwa; maombi au nyimbo za kumsifu Mungu zingeonekana kuwa hazifai kwenye ngoma zao. Yapasa jaribio hili liwe la kukata maneno. Michezo ambayo huelekea kudhoofisha upendo wa mambo matakatifu na kupunguza furaha yetu kazini mwa Mungu haifai kutafutwa na Wakristo. Muziki na kucheza kwa furaha na kumsifu Mungu wakati wa kuhamisha sanduku la agano haukuwa na namna yo yote ya ufisadi wa dansi ya siku hizi. Ile ilikusudiwa kwa ukumbusho wa Mungu na kulitukuza jina lake takatifu. Lakini hii ya siku hizi ni hila ya Shetani kuwafanya watu wamsahau Mungu na kumdharau. 18PP 707;KN 186.4

  Vijana kwa kawaida huenenda kama kwamba saa za thamani kuu za muda wa majaribio kama wanafaa au hawafai, pindi wakati rehema ikiendelea, ni sikukuu kubwa walizoruhusiwa kupumzika, nao wamewekwa ulimwenguni humu kwa michezo yao wenyewe na kujifurahisha kwa anasa daima. Shetani amekuwa akijitahidi kuwaongoza kutafuta furaha katika michezo ya kidunia na kujihalalisha kwa kujaribu kuonyesha kuwa michezo hiyo haina madnara, ni safi, halali, tena yenye maana kwa afya. 19IT 501;KN 187.1

  Wengi wanashiriki sana micnezo ya kidunia, inayoharibu tabia ambayo Neno la Mungu laikataza. Hivyo hufarakana na Mungu na kujiweka pamoja na wale wapendao anasa za dunia. Dhambi zile zilizowaangamiza watu walioshi zamani kabla ya gharika na ile miji ya uwandani zaonekana siku hizi-siyo katika nchi za washenzi tu, wala siyo miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya dini ya Kikristo ipendwayo na wengi, bali miongoni mwa wale wanaokiri kuwa wanatazamia kuja kwa Mwana wa Adamu. Ikiwa Mungu angeziweka dhambi hizi mbele yako kama zionekanavyo machoni mwake, ungejawa na aibu na hofu. 205T 218;KN 187.2

  Tamaa ya tamasha na michezo ya kupendeza ni jaribu na mtego kwa watu wa Mungu na hasa kwa vijana. Shetani hutayarisha daima vishawishi kuivuta mioyo ipotoke na kuacha kazi takatifu ya matayarisho ya mambo ambayo hayako mbali, wakati ujao. Kwa njia ya watu wapendao anasa za dunia huyadumisha mambo ya kusisimua ili kuwashawishi wale wasiojihadhari kushiriki anasa za dunia. Pana maonyesho, hotuba, na michezo mbalimbali isiyo na mwisho ambayo imekusudiwa kuwaongoza watu kuipenda dunia; na kwa njia ya ushirika huu na walimwengu imani hudhoofishwa.KN 187.3

  Mungu hamhesabu mwenye kutafuta anasa kama yu mfuasi wake. Wale tu wanaojikana nafsi wenyewe, wenye kiasi, unyenyekevu, na utakatifu maishani mwao hao ndio wafuasi wa kweli wa Yesu. Hao hawawezi kufurahia mazungumzo ya ovyo, yasiyo na maana, ya wapendao anasa za dunia. 21 CT 325, 328; KN 187.4

  Kama kwa kweli u mtu wa Kristo, utakuwa na nafasi kumshuhudia. Utaalikwa kuhudhuria mahali penye starehe nawe utakuwa na nafasi kumshuhudia Bwana wako. Kama u mwaminifu kwa Kristo, basi, hutajaribu kutoa udhuru kwa kukosa kufika, bali utasema wazi tena kwa makini kwamba u mtoto wa Mungu, na kanuni zinazoyaongoza maisha yako hazikuruhusu uwepo ingawa kwa safari moja mahali ambapo huwezi kumwalika Bwana wako kuwapo. 22AH 519; KN 187.5

  Kutakuwako na tofauti kubwa baina ya jumuia ya wafuasi wa Kristo kwa ajili ya maburudisho na mkusanyiko wa ngoma ya kidunia kwa ajili ya anasa na michezo. Badala ya sala na kumtaja Kristo na mambo matakatifu itasikika kutoka midomoni mwa hao wapendao anasa za dunia vicheko vya ovyo na mazungumzo yasiyo na maana. Wazo lao ni kuwa na sikukuu tu. Michezo yao huanza kwa mambo ya upuzi na kumalizika kwa mambo ya ovyo, yasiyo na maana. 23 AH 512.KN 188.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents