Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shuhuda na Msomaji

  Kwa muda wa miaka sabini Ellen G. White alisema na kuandika habari za mambo ambayo Mungu alikuwa amemfunulia. Mara nyingi maonyo yalikuwa yametolewa kuwasahihisha wale ambao walipotoka kutoka katika ukweli wa Biblia. Mara nyingi walionyesha njia ambayo Mungu angependa watu wake waifuate. Wakati mwingine Shunuda hizi zilikuwa juu ya mwenendo wa maisha, nyumbani, na kanisani. Washiriki wa kanisa waliupokeaje ujumbe huu?KN 32.4

  Tangu mwanzo wa kazi yake, viongozi wakubwa waliipima kazi yake wapate kuhakikisha kuwa mafunuo ya kipawa cha unabii yalikuwa ya kweli. Mtume Paulo aonya, “Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema,” (lThe. 5:20, 21). Kipimo cha Biblia cha kumpima nabii kilitumika kuithibitisha kazi ya Ellen White. Na hivi ndivyo alivyopenda iwe, maana ameandika:KN 32.5

  “Kazi hii ni ya Mungu, au sivyo. Mungu hafanyi shirika lo lote na Shetani. Kazi yangu kwa miaka thelathini iliyopita inao ama muhuri wa Mungu ama muhuri wa yule adui. Haiwezi kuwa nusunusu kwa jambo hili.” Biblia inatoa majaribio manne ambayo kwayo nabii hana budi kupimwa. Kazi ya Ellen White imeshinda katika kila kipimo.KN 32.6

  1. Ujumbe wa nabii wa kweli hauna budi kupatana na sheria ya Mungu na maneno ya ujumbe wa manabii, (Isa. 8:20).KN 33.1

  Maandishi ya Ellen G. White huiheshimu sheria ya Mungu na kuwaongoza daima wanaume na wanawake kwenye Biblia nzima. Anaelekeza kwenye Biblia kama kanuni ya imani na ibada na kama nuru kuu ambapo maandishi yake “nuru ndogo,” huwaelekeza wote wasomao.KN 33.2

  2. Unabii wa kweli hauna budi kutimia. (Yer. 28:20). Huku kazi ya Ellen White ikiwa imefanana na ile ya Musa katika kuwaongoza watu, lakini yeye aliandika kwa njia ya kutabiri matukio mengi. Mwanzoni mwa kazi yetu ya kuchapisha vitabu na magazeti mnamo mwaka 1848, alisema jinsi ambavyo ingalikua na kueneza nuru ulimwenguni. Leo Waadventista Wasabato huchapisha vitabu na magazeti katika lugha 200 ambavyo vina thamani zaidi ya Shs. 140,000,000 kwa mwaka.KN 33.3

  Mwaka 1890, walimwengu walipotangaza kuwa hapatakuwako na vita tena na ya kwamba muda wa miaka elfu ulikuwa karibu kuanza, Ellen G. White aliandika: “Dhoruba inakuja, nasiKN 33.4

  yatupasa kujiweka tayari kuzikabili nguvu zake Tutaona matataKN 33.5

  pande zote. Maelfu ya meli zitatupwa kwa nguvu vilindini mwa bahari. Manowari zitazama, na watu mamilioni watapoteza maisha yao.” Hili lilitimia katika Vita Kuu ya I na ya II.KN 33.6

  3. Nabii wa kweli atakiri kuwa Yesu Kristo amekuja katika mwili, na ya kuwa Mungu alifanyika mtu halisi. (1 Yohana 4:2). Kusoma Tumaini la Vizazi Vyote hudhihirisha kuwa kazi ya Ellen G. White hulenga katika kipimo hiki. Tazama maneno haya:KN 33.7

  “Yesu angaliweza kuendelea kukaa karibu na Baba. Angaliweza kushikilia ule utukufu wa mbinguni, na kupewa heshima na malaika. Lakini alichagua kuiweka enzi na utukufu wake mikononi mwa Baba yake, na kushuka kutoka katika kiti cha enzi cha mbinguni na kuja duniani ili kuwaletea nuru wale walio gizani, na uzima kwa wale wanaopotea.KN 33.8

  “Yapata miaka elfu mbili iliyopita, sauti ya maana ajabu ilisikika mbinguni kutoka katika kile kiti cha enzi cha Mungu ikisema, ‘Tazama, nimekuja’. Dhabihu na toleo hukutaka, lakini Mwili uliniwekea tayari Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) niyafanye mapenzi yako, Mungu.’ (Waebrania 10:57). Kwa maneno haya umetangazwa utimizo wa kusudi lililokuwa limefichwa tangu zamani. Kristo alikuwa karibu kuuzuru ulimwengu wetu, na kufanyika mtu halisi Machoni pa walimwengu nakuwa na uzuri hata wamtamani; lakini, alikuwa Mungu aliyefanyika mtu halisi, nuru ya mbinguni na duniani. Utukufu wake ulifichwa. Ukuu na utukufu wake ulisetiriwa ili apate kuwakaribia wanadamu wenye huzuni na waliojaribiwa.”KN 33.9

  4. Pengine kipimo muhimu sana cha nabii wa kweli hupatikana katika maisha yake, kazi yake, na mvuto wa mafundisho yake. Kristo alinena wazi jambo hili katika Mathayo 7:15, 16: “Mtawatambua kwa matunda yao.” Tukiyapima maisha ya Ellen G. White hatuna budi kusema kuwa aliishi maisha mema ya Kikristo yanayopatana na mafundisho yake, na kushika kile tunachoweza kumtazamia nabii. Tukiyaangalia matunda kama yalivyodhihirishwa maishani mwa wale ambao wameyafuata maonyo ya Roho ya Unabii, twaona kuwa ni mema. Shuhuda hizi zimezaa matunda mema. Tukilitazama Kanisa, tukijua kuwa tumeongozwa katika kazi za namna nyingi mbalimbali kwa mashauri haya, hatuna budi kukiri kuwa kazi ya Ellen White inashinda kipimo hiki. Hali ya umoja wa mafundisho yaliyo katika maandishi yaliyoandikwa kwa kalamu ya wino kwa muda mrefu zaidi ya miaka 70 pia hushuhudia hakika ukamilifu wa kipawa hiki.KN 34.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents