Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Usilinajisi Hekalu la Mungu

  Kuzitawala akili za moyoni mwa vijana, kuyaharibu mawazo na kuamsha tamaa mbaya ndiyo kazi kubwa ya Shetani siku hizi za mwisho; maana anajua kuwa kwa kufanya hivi aweza kuwaongoza kutenda mabaya, na hivyo uelekevu wote ulio bora hautakuwa na thamani iwayo yote, naye aweza kuwatawala apendavyo mwenyewe. 5CG 440;KN 125.1

  Roho yangu yawasikitikia vijana wanaoziendeleza tabia zao katika kizazi hiki kilichopotoka. Naogopa na kutetemeka kwa ajili ya wazazi wao pia; maana nimeonyeshwa kwamba kwa kawaida nawafahamu wajibu wao kuwalea watoto wao katika njia iwapasayo. Mila na desturi zinashamirishwa, na mara watoto hujifunza kuvutwa nazo nao wakaharibika; huku wazazi wao wema wakiwa wao wenyewe wametiwa ganzi na kulala bila kujali hatari yao. Lakini ni vijana wachache sana wasio na mazoea mabaya. Wengi huruhusiwa sana kutofanya mazoezi ya viungo vya mwili kwa kuogopa kwamba watafanya kazi kupita kiasi. Wazazi hubeba mzigo wenyewe ambao watoto wao wangeuchukua.KN 125.2

  Kufanya kazi kupita kiasi ni vibaya lakini matokeo yaletwayo na uvivu ni mabaya na yapasayo kuogopwa zaidi. Uvivu huleta mazoea mabaya ya kujifurahisha kwa anasa. Kufanya kazi kwa bidii hakuchoshi wala kumaliza hata sehemu tano kwa moja ya nguvu kama mazoea mabaya. Kama kazi nyepesi iliyopangwa vizuri huwachosha watoto wenu, jueni hakika, wazazi, kuwa kuna kitu fulani kingine, siyo kazi yao, ambacho hudhoofisha miili yao na kuleta uchovu wa daima. Wapeni watoto wenu kazi ya juhudi, ambayo itaitumikisha misuli. Uchovu unaotokana na kazi ya namna hii utapunguza tamaa yao kujifurahisha na anasa na mazoea mabaya. 62T 348, 349;KN 125.3

  Epuka kusoma au kuona mambo ambayo yataleta fikira mbaya. Kuza tabia ya uadilifu na uelekevu. 72T 410;KN 125.4

  Licha Mungu kutaka kuyatawala mawazo yako, hata hutaka kutawala tamaa na mapenzi yako. Wokovu wako hutegemea juu kutawala tamaa na mapenzi yako. Wokovu kutegemea juu ya kujitawala kwako katika mambo haya. Tamaa na upendo ni njia zenye nguvu. Kama zikitumiwa vibaya, kama zikitiwa kazini kwa nia mbaya, kama zikitumiwa mahali pasipostahili, zinaweza kukuletea uharibifu na kukuacha katika hali mbaya, pasipo Mungu na bila tumaini.KN 125.5

  Kama unazoea kujifurahisha kwa tamaa za bure, na kuuruhusu moyo wako kufikiri mambo yasiyo safi, unayo hatia kubwa mbele za Mungu kana kwamba mawazo yako yalikwisha kutimizwa kwa vitendo nasa. Kile kinachozuia kutimiza tendo ni kukosa nafasi. Mawazo ya mchana na usiku ni mabaya na mazoea mabaya ya hatari mno. Yakiisha kufanyiwa kazi, karibu haiwezekani tena kuyavunja mazoea ya namna hiyo, na kuyaongoa mafikira kwenye mambo safi, matakatifu, na yaliyo bora. Itakubidi kuwa askari mwaminifu wa kulinda macho yako, masikio, na milango yako yote ya maarifa kama ukitaka kuutawala moyo wako na kuyazuia mawazo mabaya yasiyo na maana yasiiharibu roho yako. Uwezo wa neema peke yake ndio uwezao kazi hii muhimu sana. 82T 561;KN 126.1

  Kujifunza kupita kiasi, kwa kuifanya damu nyingi iende ubongoni huleta hali mbaya ya fadhaa ambayo huelekea kupunguza uwezo wa kujitawala, na mara nyingi huchochea tamaa au tamaa. Hivyo mlango huwa wazi kwa ucham. Kutumia vibaya au kutokutumia kabisa nguvu za mwili ni asili ya upotovu mwmgi unaoenea mahali pengi ulimwenguni. “Kiburi, na kushiba, na kufanikiwa,” ni maadui wakubwa wa maendeleo ya wanadamu katika kizazi hiki kama yalivyokuwa asili ya uharibifu wa Sodoma. 9Ed. 209;KN 126.2

  Uzoefu wa kujifurahisa na tamaa mbaya zaidi utawafanya wengi kuyafumba macho yao wasiione nuru, maana huogopa kuwa wataziona dhambi ambazo hawapendi kuziacha Wote waweza kuona kama wakipenda. Kama wakichagua giza badala ya nuru, uhalifu wa sheria utakuwa ni ule ule, wala hakuna tofauti. 102T 352;KN 126.3

  Kufa ni bora kuliko kuivunja au kuiasi sheria ya Mungu, hili ndilo lingekuwa neno la hekima (kaulimbiu ya) kila Mkristo, Kama watu wanaojidai kuwa waongozi, wanaoyathamini maneno matakatifu sana, ya kweli, yanayotakasa ya Neno la Mungu, hatuna budi kukiinua kipimo juu zaidi ya mahali kilipo hivi sasa. Dhambi na wenye dhambi kanisani yawapasa kufanyiwa mashauri yao mara bila kukawia, ili wengine wasije wakaambukizwa. Ukweli na usafi huhitaji tufanye kazi kamili kuisafisha kambi na kuwaondoa akina Akani. Basi wale wenye madaraka wasikubali dhambi kuwapo kwa ndugu. Mwonyesheni kuwa hana budi kuacha dhambi zake ama sivyo. Atengwe kanisani. 115T 147;KN 126.4

  Vijana waweza kuwa na kanuni thabiti sana hata majaribu makubwa ya Shetani yasiweze kuwapotosha, na kuwafanya waasi. Samweli alikuwa mtoto aliyezungukwa na mivuto mibaya sana. Aliona na kusikia mambo ambayo yaliisikitisha roho yake. Wana wa Eli, waliohudumu katika kazi takatifu walitawaliwa na Shetani. Watu hawa walichafua tabia yote iliyowazunguka. Wanaume na wanawake kila siku walishindwa na dhambi na mabaya, lakini, Samweli alienenda bila mawaa. Mavazi yake ya tabia yalikuwa safi yasiyo na doa. Hakushiriki, wala kupendezwa na dhambi zilizowajaza Waisraeli wote ripoti mbaya ya kutisha sana. Samweli alimpenda Mungu; aliuweka moyo wake karibu na Mungu hata malaika akatumwa kuzungumza naye kwa habari ya dhambi za wana wa Eli ambazo zilikuwa zikiharibu Israeli. 123T 472-474;KN 126.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents