Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shauri Jema kwa Bwana Arusi na Bibi Arusi

  Wapenzi Ndugu na Dada: Mmeungana katika agano la daima maisha yenu yote. Mafundisho yenu katika maisha ya unyumba yameanza. Mwaka wa kwanza wa maisha ya unyumba ni mwaka wenye mambo ya kupatwa nayo maishani, mwaka ambao mume na mke hujifunza tabia mbalimbali walizo nazo, kwa wao, kama vile mtoto anavyojifunza masomo shuleni. Katika mwaka huu wa kwanza wa maisha ya unyumba pasiwepo mambo yatakayoharibu furaha yenu ya wakati ujao.KN 145.3

  Kupata ufahamu bora wa unyumba ni kazi ya daima maishani. Wale wanaooana huingia shule ambayo kamwe katika maisha haya hawaihitimu ama kuimaliza. Ndugu, wakati wa mkeo na nguvu na raha sasa vimeungamanishwa pamoja na yako. Mvuto wako kwake waweza kuwa harufu ya uzima iletayo uzima au harufu ya mauti. Angalia sana usije ukayaharibu maisha yake.KN 145.4

  Dada yakupasa sana kujifunza mafundisho yako mazuri ya kwanza kwa habari za kazi na wajibu wa maisha ya unyumba. Hakikisha kuwa unajifunza mafundisho hayo kwa uaminifu siku kwa siku. Usikubali kushindwa na moyo wa kutokuridhika au kukata tamaa upesi. Usitamani maisha ya anasa na kujikalia kivivu. Daima jihadhari usishindwe na choyo ama moyo wa kujipendeza nafsi mwenyewe bila kujali wengine.KN 145.5

  Katika umoja wenu wa maisha upendano wenu hauna budi kuwa sifa yenu kila mmoja, mkifurahisnana ninyi. Kila mmoja wenu hana budi kutumikia furaha ya mwenziwe. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu. Lakini huku mkipaswa kupatana na kuwa kitu kimoja, hali halisi ye yote kati yenu kupotewa na hadhi yake kwa ajili ya mwenziwe. Nafsi yako ni mali ya Mungu. Kila mmoja na amwulize Mungu hivi, Ni jambo gani linalofaa? Ni jambo gani lisilofaa? Nawezaje kulitimiza vizuri kusudi la maisha? “Ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinuliliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” (Kwa kuwa ni hivyo, mtukuzeni Mungu kwa mwili wenu, na kwa roho yenu, ambayo ni mali ya Mungu.”-(Kiunguja) Upendo wenu kwa kile ambacho ni cha kibinadamu hauna budi kuwa pungufu kuliko upendo wenu kwa Mungu. Wingi wa upendo wenu hauna budi kufurika kwake yeye aliyeutoa uhai wake kwa ajili yenu. Kuishi kwa ajili ya Mungu, mtu hana budi kumpenda kabisa. Je, upendo wenu kwake aliyewafilia unafurika? Kama unafurika, upenao wenu ninyi kwa ninyi utatimiza agizo la Mungu.KN 145.6

  Upendo waweza kuwa safi na mzuri, lakini unaweza kuwa wa juu juu tu kwa sababu haukujaribiwa. Mfanyeni Kristo kuwa wa kwanza na wa mwisho na bora zaidi ya mambo mengine yote. Daima mtazameni, ndipo upendo wenu kwake utakavyozidi na kuwa wenye nguvu kila siku kadiri unavyotolewa upate kujaribiwa. Na kadiri upendo wenu mlio nao kwake unavyozidi kuwa mwingi, upendano wenu utaongezeka na kuwa na nguvu. “Sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tufanane na mfano uo huo toka utukufu hata utukufu.”(2 Wakorintho 3:18). Sasa mnazo kazi za kufanya ambazo kabla ya kuoana hamkuwa nazo. “Basi....jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu.” “Mkienenda katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi.” Soma kwa uangalifu maneno yafuatayo: “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa Vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanis, akajitoa kwa ajili yake.” (Wakolosai 3:12; Waefeso 5:2, 22-25).KN 146.1

  Ndoa, yaani umoja wa maisha, ni mfano wa ushirika ulio baina ya Kristo na kanisa lake. Moyo ambao Kristo alionyesha kwa kanisa ndio moyo ambao mume na mke wanapaswa kuwa nao wao kwa wao. Mume wala mke asijaribu kumtawala mwenzake kwa nguvu bila haki. Bwana ameweka kanuni ambayo imepasa kuwa kiongozi cha jambo hili. Mume apaswa kumpenda mkewe kama Kristo alipendavyo kanisa. Mke naye apaswa kumheshimu mumewe. Wote wawili wanapaswa kukuza vizuri moyo wa rehema, wakikusudia kutohuzunishana au mmoja kumdhuru mwingine.KN 146.2

  Ndugu na dada, ninyi nyote walili mnao uwezo wa nia thabiti. Mwaweza kuufanya uwezo huu kuwa mbaraka mkubwa au laana kubwa kwenu wenyewe ama kwa wale wanaokutana nanyi. Usijaribu kumlazimisha mwenzako kuyakubali mapenzi yako. Hamwezi kufanya hivi na huku mkadumu kupendana. Kuonyesha ukaidi huharibu amani na furaha ya nyumbani. Msikubali unyumba wenu kuwa wenye ugomvi. Kama mkifanya hivyo mtakosa furaha wote. Semeni kwa upole na kutenda kwa upole, mkitangulizana. Jihadharini sana na maneno yenu, maana yana mvuto wenye nguvu kwa mema ama kwa mabaya. Msikubali ukali kuwapo katika sauti zenu. Ingizeni maishani mwenu umoja wenye harufu nzuri ya tabia ya Kristo. Kabla mwanamume hajaingia umoja mkubwa kama llivyo ndoa, yampasa ajifunze jinsi ya kujitawala na jinsi ya kuwatendea wengine.KN 146.3

  Ndugu, uwe mfadhili; mwenye saburi na mvumilivu. Kumbuka kuwa mkeo alikukubali uwe mumewe, si kusudi upate kumtawala, la, bali ili uwe msaidizi wake. Usiwe mkali, mdhaiimu au mwenye kutoa amri na kushurutisha watu wa nyumbani kuzitii. Usitumie nguvu kumshurutisha mkeo kufanya upendavyo. Kumbuka kuwa anayo nia ya moyoni na ya kwamba yeye pia huweza kutaka kufanya mapenzi yake kama wewe. Pia kumbuka kuwa unayo bahati ya ujuzi mkubwa ulio nao. Kuwa mwenye huruma na mwenye staha. “Hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina unaflki.” (Yakobo 3:17).KN 147.1

  Kumbukeni, ndugu na dada zangu, ya kuwa Mungu ni Upendo na kwamba kwa neema yake mwaweza kufaulu kupendezana ninyi kwa ninyi, kama mlivyoahidi kufanya katika mapatano na ahadi ya ndoa yenu. Kwa nguvu za Mkombozi mwaongeza kutumia busara na uwezo mlio nao kuyasaidia maisha ya watu yaliyopotoka yapate kunyoka na kumwelekea Mungu. Kuna jambo gani Kristo asiloweza kufanya? Yu mkamilifu katika hekima yake, katika haki, na katika upendo. Msijitenge, ridhikeni kuonyesha upendo wenu kila mmoja kwa mwenzake. Shikeni kila nafasi kuwafurahisha majirani, mkishiriki pamoja nao upendano wenu. Maneno ya upole, nyuso za huruma, shukrani za moyoni, vingeweza kuwag awia wengi wasumbukao, walio katika nali ya upweke, kama ikombe cha maji baridi kwa mtu mwenye kiu. Neno la kutia moyo, tendo la fadhili, lingeweza hata kupunguza uzito wa mizigo inay-owalemea watu waliokwisha kucholca. Huduma ya ukarimu ndiyo yenye kuleta furaha ya kweli. Na kila neno na kila tendo la huduma ya namna hii huandikwa vitabuni mbinguni kama limetendewa Kristo. Anasema, “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.” (Mathayo 25:40).KN 147.2

  Kaeni kwenye pendo zuri la Mwokozi. Ndipo mvuto wenu utawanufaisha walimwengu. Roho ya Kristo na iwatawale. Sheria ya wema na iwe midomoni mwenu daima. Uvumilivu na ukarimu nauyaainishe maneno na matendo ya wale waliozaliwa mara ya pili, wapate kuishi maisha mapya ndani ya Kristo. 27745-50KN 147.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents