Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Arusi Isiwe na Mambo Mengi, Bali iwe Wakati wa Furaha

    Upendo mtakatifu utokao kwa Kristo kamwe hauharibu upendo wa kibinadamu, bali unakuwa nao ndani yake. Kwa njia ya upendo huo mtakatifu, upendo wa kibinadamu hutakaswa na kusafishwa, kukuzwa vizuri na kuadilishwa. Kamwe upendo wa kibinadamu hauwezi kuzaa matunda yake mazuri mpaka kwanza uwe umeunganishwa na tabia takatifu na kufundishwa kukua kuelekea juu mbinguni. Yesu ataka kuona ndoa za furaha, na nyumba zenye furaha.KN 144.4

    Maandiko Matakatifu yasema kuwa Yesu na wanafunzi wake walialikwa katika karamu hii ya arusi (Kana). Kristo hakuwaruhusu Wakristo kusema wakati wanapoalikwa arusini, . Haitupasi kuwepo mahali penye sherehe ya namna hiyo. Kwa kuihudhuria yeye mwenyewe karamu hii Kristo aliifundisha kuwa angependa tufurahi pamoja na wale wanaofurahi tukiyashika maagizo yake. Kamwe hapingi sherehe za wanadamu ambazo hazifanywi kinyume cha shena ya Mungu. Mkutano ule ambao Kristo aliutukuza kwa kuwako yeye mwenyewe, ni halali kwamba wafuasi wake wamepaswa kuuhudhuria. Baada ya kufika kwenye karamu hii, Kristo alihudhuria zingine nyingine nyingi, akizihalalisha kwa kuwako yeye mwenyewe na kwa mafundisho pia.KN 144.5

    Hatuna sababu ya kufanya maandamano makubwa ama sherehe kubwa sana, hata kama jamii ya watu karamuni wakiwa hali moja kabisa.KN 145.1

    Kila mara huwa jambo lisilonipendeza kuona pakiwako na vicheko na shangwe za vigelegele ama mambo ya jinsi hiyo. La, hili ni agizo la Mungu, lipasalo kuheshimiwa kabisa kwa moyo wa kicho. Kadiri unyumba unavyofanywa hapa chini, hauna budi kuonyesha namna watu wa nyumba hiyo watakavyokuwa watu wa nyumba ya mbinguni juu. Daima utukufu wa Mungu hauna budi kufanywa kuwa jambo la Kwanza. 1 AH 99-101;KN 145.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents