Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kufanza Tabia Ifananayo na Ile ya Kristo

  Dini ya Kristo kamwe haimwondolei heshima mwenye kuipokea; kamwe haimfanyi duni au asiye na adabu, mwenye dharau au mwenye kujivuna, mwepesi wa hasira au mkali, asiye na huruma. Kinyume cha hayo, huifanya tamaa iwe safi, huziadilisha akili za kuchagua vema, na kuyasafisha na kuyaongoza vema mafikara, ikiwateka nyara kwa Kristo. Wazo la Mungu kwa ajili ya watoto wake ni bora kupita wazo lililo bora sana la binadamu. Ametia katika sheria yake takatifu nakala ya tabia yake.KN 90.5

  Kipeo cha tabia ya Mkristo ni tabia ya Kikristo. Pamefunguliwa mbele yetu njia ya maendeleo ya daima. Tunao mradi wa kujipatia, kipimo cha kukifikia, hicho ni pamoja na kila kitu kizuri na safi na adili na bora. Daima yapasa pawepo kujitahidi kufanya maendeleo mbele na juu kwenye ukamilifu wa tabia. 28T 63, 64:KN 90.6

  Tutakua kila mmoja wetu, kwa muda na kwa milele, vile mazoea yetu yatufanyavyo. Maisha ya wale wenye kufanya mazoea mema, na walio waaminifu katika kufanya kila kazi, watafanana na mianga yenye kutupa mionzi ya nuru juu ya njia ya wengine; lakini mazoea ya kutokuwa na uaminifu yakipendelewa, kama mazoea mabaya ya ulegevu, uvivu, na uzembe yakiachwa kuwa na nguvu, wingu jeusi kuliko giza la usiku wa manane litakaa imara juu ya maelekeo ya maisha haya na yale ya milele kumzuia mtu asiupate uzima wa wakati ujao. 34T 452;KN 91.1

  Heri mtu yule ayasikiaye maneno ya uzima wa milele. Akiwa ameongozwa na “Roho wa kweli” kwenye kweli yote. Hatapendwa, hataheshimiwa, wala kusifiwa na walimwengu; lakini atakuwa mwenye thamani kuu machoni pa Mungu. “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu hatutambui, kwa kuwa haukumtambua, yeye” (1 Yohana 3:4). 45T 439;KN 91.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents