Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Anza mapema kuwafundisha watoto kutunza mavazi yao.

    Wapatie mahali pa kuweka vitu vyao na wafundishwe kukunja vizuri kila kitu na kukiweka mahali pake. Kama huwezi kuwanunulia dawati, tumia sanduku, uligawe vyumba vidogo vidogo, na kulifunika kwa kitambaa kizuri king’aacho. Kazi hii ya kufundisha usafi na utaratibu itachukua wasaa mdogo kila siku, lakini itakuwa na faida baadaye kwa watoto wenu, na mwishowe itakuokolea wakati na masumbufu mengi.KN 171.2

    Wazazi wengine huwaacha watoto wao kuwa waharibifu kutumia kwa michezo vitu ambavyo hawana haki kuvigusa. Watoto wangefundishwa kuwa hawana ruhusa kutumia mali ya watu wengine. Yawapasa kujifunza kushika kanuni za adabu kwa ajili ya raha ya jamaa nzima. Haiwaongezei watoto furaha wanaporuhusiwa kutumia kila kitu wanachoona. Kama wasipofundishwa kuwa watunzaji, watakua huku wakiwa na tabia za uharibifu wa vitu.KN 171.3

    Msiwape watoto vitu vya kuchezea vyenye kuvunjika kwa urahisi. Kufanya hivi ni kuwafundisha uharibifu. Hebu wapatie vitu vichache vya kuchezea, lakini viwe imara na vyenye kudumu siku nyingi. Mashauri ya namna hii, ingawa yaonekane kuwa madogo namna gani, yana maana sana katika malezi ya mtoto. 2CG 110,111, 102 KN 171.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents