Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 17 - Usafi wa Moyo na Maisha

  MUNGU amewapa makao kuyatunza na kuyahifadhi katika hali bora kwa ajili ya kazi na utukufu wake Mungu. Miili yenu si mali yenu wenyewe. “Au hamjuia ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu.” “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi,“ 12T 352, 353;KN 124.1

  Katika zama hizi za uharibifu wakati adui yetu Shetani kama simba aungurumaye atembeapo huko na huko akitafuta mtu apate kumla, naona inavyolazimu kuipaza sauti ya onyo. “Kesneni muombe, msije mkaingia majaribuni” (Marko 14:38). Kuna wengi walio na talanta nzuri ambao kwa uovu huzitoa zitumike kwa kazi ya Shetani. Onyo gani ambalo naweza kuwapa watu hawa ambao nujidai kuwa wametoka kwa walimwengu na kuachana na kazi zao za giza na ambao Mungu amewafanya ghala za kuwekea sheria yake, lakini huku kama mtini wa fahari, huonyesha wazi wazi mbele za Mwenyezi Mungu, matawi yao yanayositawi, lakini hayazai matunda kwa utukufu wa Mungu? Wengi wao huyafurahia, mafikara yasiyo safi, mawazo mabaya, mapenzi yasiyo matakatifu, na tamaa mbaya. Mungu huyachukia matunda yanayozaliwa na mti wa namna hii. Malaika, wema na watakatifu huuchukia sana mwenendo wa namna hii, huku Shetani akiufurahia. Aha, laiti wanaume na wanawake wangefikiri kile ambacho hakina budi kupatikana kwa kuiasi sheria ya Mungu! Kwa hali iwayo yote, uasi ni fedheha kwa Mungu na laana kwa mwanadamu. Yatupasa kuuhesabu hivi, si neno uwe unaoonekana kuwa haki namna gani, na ijapokuwa utendwe na mtu gani awaye yote. 25T 146;KN 124.2

  Wenye moyo safi watamwona Mungu. Kila wazo lisilo safi huinajisi rono, huchafua akili za moyoni, na kuelekea kufutilia mbali mivuto ya Roho Mtakatifu. Hutia giza maono ya kiroho, ili mtu asiweze kumwona Mungu. Bwana aweza naye humsamehe mwenye dhambi atubuye; lakini ajapokuwa amesamehewa moyo utabaki na kovu. Uchafu wote wa maneno au wa mawazo hauna budi kuepukwa na mtu ambaye angependa kuwa na akili safi za kweli ya kiroho. 3DA 302;KN 124.3

  Wengine wataukiri uovu wa anasa za dhambi, lakini watatoa udhuru kwa kusema kuwa hawawezi kuzishinda tamaa zao mbaya. Hili ni ungamo lililo baya kabisa kwa mtu awaye yote kulifanya ambaye hulitaja jina la Kristo. “Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu” (2 Timotheo 2:19). Kwa nini kuna udhaifu kama huu? Ni kwa sababu tamaa za kinyama zimetiwa nguvu kwa kuzitumia mpaka zimepata nguvu kuutawala uwezo ulio bora zaidi. Wanaume na wanawake hawana kanuni inayoyaongoza maisha. Wanakufa kiroho kwa sababu wamejilisha vyakula vitamu muda mrefu hata uwezo wao wa kujitawala unaelekea kama kwamba haupo. Tamaa duni za mwili wao zinatawala, na uwezo ule ambao ungepasa kutawala umekuwa mtumwa wa tamaa mbaya. Roho imeshikwa katika kifungo duni kabisa. Tamaa ya mwili imezima moyo wa kutafuta utakatifu na kupozesha mafanikio ya kiroho. 42T 348;KN 124.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents