Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Walimu Chini ya Mungu

    Bwana hutenda kazi pamoja na mwalimu aliyejitoa wakfu; na ni kwa faida ya mwalimu mwenyewe kulifahamu neno hili. Walimu ambao wako chini ya utawala wa Mungu hupokea neema na kweli na nuru kwa njia ya roho Mtakatifu kuipitisha kwa watoto. Wako chini ya Mwalimu mkuu kabisa aliyepata kuwako ulimwenguni, na ingekuwa vibaya kama nini wakiwa na roho isiyo njema, sauti kali, na kujawa na chuki! Kwa jambo hili wangedumisha makosa yao wenyewe kwa watoto wao.KN 233.1

    Mungu atazungumza na roho ya mtu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Omba unapokuwa ukijifunza, “Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zab. 119:18). Mwalimu atakapomtegemea Mungu kwa maombi, Roho ya Kristo itamshukia, na Mungu atafanya kazi kwa njia yake kwa Roho Mtakatifu kwenye akili za mwanafunzi. Roho Mtakatifu huzijaza akili tumaini na moyo mkuu na maneno ya Biblia, ambayo yatapitishwa kwa mwanafunzi. Maneno ya kweli yataendelea kuwa na maana, nayo yatapanuka na kupata ukamilifu wa maana ambayo kamwe hajaota habari zake. Uzuri na sifa ya neno la Mungu vina mvuto unaoongoa akili na tabia; macheche ya upendo wa mbinguni yataanguka juu ya mioyo ya watoto kama maongozi ya Mungu Twaweza kuleta mamia na maelfu ya watoto kwa Kristo kama tukitende kazi ya kuwavuta kuja kwake. 15CT.171,172;KN 233.2

    Kabla watu hawajaweza kuwa na akili hasa, yawapasa kufahamu tegemeo lao kwa Mungu, na kujazwa na hekima yake. Mungu ndiye chimbuko la akili na nguvu za kiroho pia. Watu mashuhuri amoao wamefikia vyeo vya juu sana vya elimu, kama waonavyo, hawawezi kulinganishwa na Yohana, mwanafunzi mpendwa wa Yesu wala mtume Paulo. Akili na nguvu za kiroho zikiunganishwa ndipo cheo cha juu sana maishani kinapoweza kufikiwa. Wale wafanyao hivi, Mungu atawakubali kama watenda kazi pamoja naye katika kuwaelimisha wengine. 16CT.66 ;KN 233.3

    “Kazi kubwa sana ya jamii ya shule zetu wakati huu ni kuwaonyesha walimwengu kielelezo chema ambacho humtukuza Mungu. Malaika watakatifu huiongoza na kuisimamia kazi hiyo kwa njia ya wanadamu, na kila idara ya kazi hiyo haina budi kuwa na alama ya ubora mtakatifu. 17CT.57 ;KN 233.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents