Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Tabia ya Mbinguni Haina Budi Kupatikana Duniani

    Msidanganyike. Mungu hadhihakiwi. Utakatifu tu, wala si kitu kingine, ndio utakaowafanya kuwa tayari kwenda mbinguni. Unyofu na uchaji wa hakika katika mambo ya maisha peke yake ndio uwezo wa kuwapa tabia safi, bora, na kuwawezesha kumgia mbele za Mungu akaaye penye nuru isiyoweza kukaribiwa. Tabia ya mbinguni haina budi kupatikana hapa duniani, ama sivyo kamwe naipatikani tena. Basi, anza mara moja. Usijidanganyike kuwa utafika wakati uwezapo kujitahidi kwa urahisi kuliko sasa, Kila siku huzidisha umbali wako kutoka kwa Mungu. Jitayarishe kwa ajili ya uzima wa milele. Zoeza mawazo ya moyo wako kuipenda Biblia, kuupenda mkutano wa maombi, kupenda saa ya kumtafakari Mungu, na, zaidi ya yote, saa ambayo roho hushirikiana na Mungu. Uwe mwenye kufikiri mambo ya mbinguni ukipenda kuungana, na lile kundi la waimbaji wa mbinguni katika makao ya juu.KN 207.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents