Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 3 - Jiweke Tayari Kukutana na Bwana

    NALIONA kuwa haitupasi kuahirisha kuja kwa Bwana. Malaika amesema: “Jitayarisheni, kwa kile kinachoujia ulimwengu. Hebu matendo yenu yapatane na imani yenu.” Nikaona kuwa moyo hauna budi kukazwa kwa Mungu, na ya kuwa mvuto wetu wapaswa kuonyesha habari za Mungu, na za Neno lake la kweli. Hatuwezi kumheshimu Bwana tukiwa ovyo, tusiojali. Hatuwezi kumtukuza tukiwa tunakata tamaa. Hatuna budi kufanya bidii kwa ajili ya wokovu wa roho zetu, na kuwaongoa wengine. Jambo hili halina budi kupewa umuhimu wa kwanza ndipo mambo mengine yafuate.KN 46.1

    Naliona uzuri wa mbinguni. Naliwasikia malaika wakiimba nyimbo zao za furaha, wakimpa Yesu sifa, heshima, na utukufu. Ndipo nikatambua kitu juu ya upendo wa ajabu wa Mwana wa Mungu. Aliacha utukufu na heshima yote aliyokuwa nayo mbinguni, naye alipenda sana kutuokoa hata kwa uvumilivu na upole akastahimili aibu na dharau ambayo wanadamu walimtwisha. Alijeruhiwa, akapigwa, na kuchubuliwa; aliwambwa msalabani Kalwari na kupatwa na kifo cha maumivu makuu ili kutuokoa na mauti, kusudi tupate kuoshwa katika damu yake na kuinuliwa kukaa pamoja naye katika makao anayotuandalia, kufurahishwa na nuru na utukufu wa mbinguni, kuwasikia malaika wakiimba, na kuimba pamoja nao.KN 46.2

    Nikaona kuwa mbingu yote inapendezwa na habari za wokovu wetu; je sisi tunaohitaji wokovu tusijali? Je, tuidharau dhabihu ambayo imetolewa kwa ajili yetu? Wengine wamefanya jambo hili. Wamepuuza neema iliyotolewa, na ghadhabu ya Mungu inawakalia. Roho wa Mungu hatahuzunishwa daima. Ataondoka kama akizidi kusikitishwa. Baada ya kuyatenda yote ambayo Mungu angeweza kufanya kuwaokoa wanadamu, kama wakionyesha kwa mienendo yao kuwa wanaidharau rehema ya Yesu iliyotolewa, mauti itakuwa ndio fungu lao, nayo itanunuliwa kwa bei kubwa. Itakuwa mauti ya kutisha sana; kwa kuwa itawabidi kupata maumivu yale yaliyompata Kristo msalabani kuwanunulia ukombozi walioukataa. Ndipo watafahamu kile ambacho wamepoteza-uzima wa milele na urithi wa milele. Dhabihu kuu ambayo imetolewa kwa ajili ya roho zetu hutuonyesha thamani yake. Roho iliyo ya thamani kuu ikipotea, imepotea milele.KN 46.3

    Nimemwona malaika akisimama na mizani mikononi mwake akiyapima mawazo na mioyo ya watu wa Mungu, hasa vijana. Upande mmoja wa mizani palikuwa na mawazo na moyo uelekeao mbinguni; Upande mwingine palikuwa na mawazo na moyo uelekeao duniani. Na katika mizani hii palitupwa vitabu vyote vya hadithi vya kusoma, mawazo ya mavazi na umalidadi, majivuno, kiburi, na kadhalika. Ni wasaa wa kutisha kama nini! Malaika wa Mungu wakisimama na mizani, wakipima mawazo ya watoto wanaojidai kuwa wake Mungu-wenye kujidai kuwa wamezifia anasa za duniani ili kuishi kwa Mungu. Mizani iliyojaa mawazo ya kidunia, kiburi na majivuno mara ikashuka chini, ijapokuwa uzito wa vitu kimoja kimoja ulikuwa ukimwagika kutoka mizani hiyo. Ile yenye mawazo na moyo wa kuelekea mbinguni ikapanda juu kadin upande mwingine wa mizani ulivyoshuka, ulikuwa mwepesi kama nini! Naweza kueleza neno hili kama nilivyoona; lakini kamwe siwezi kutoa maoni kamili yaliyoniingia moyoni mwangu, nikiona malaika akiwa na mizani akiyapima mawazo na mioyo ya watu wa Mungu. Malaika akasema: “Je hawa waweza kuingia mbinguni? La, hasha, kamwe hawawezi. Waambie matumaini waliyo nayo sasa ni bure, na kama hawatatubu haraka, na kupata wokovu, lazima watapotea.”KN 46.4

    Mfano wa utauwa nauwezi kumwokoa ye yote. Wote hawana budi kuwa na uzoefu wa uhusiano wa karibu sana na Yesu. Hili tu ndilo litakalowaokoa wakati wa taabu. Ndipo kazi yao itajaribiwa na kuonekana ni ya aina gani; na kama ni dhahabu, fedha, na vito vya thamani, watasitiriwa mahali pa siri pa hema ya Bwana, Lakini kama kazi yao ni mti, majani makavu, na mabua, hakuna cho chote kiwezacho kuwakinga wasipatwe na ukali wa ghadhabu ya Yehova.KN 47.1

    Naliona kuwa wengi walijipima wao kwa wao, na kuyalinganisha maisha yao na maisha ya wengine. Haipaswi kuwa hivyo. Hakuna mwingine ila Kristo tuliyepewa awe kielelezo. Ndiye Kielelezo chetu halisi, na kila mmoja apaswa kufanya bidii sana kumwiga Kristo. Tu watenda kazi pamoja na Kristo, kama sivyo, tu watenda kazi pamoja na yule adui. Tunakusanya pamoja na Kristo ama tunatawanya. Tu Wakristo wema, wanyofu, ama sisi si Wakristo hata kidogo. Kristo anasema: “Hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu” (Ufunuo 3:15, 16).KN 47.2

    Naliona kuwa wengine walikuwa hawajajua maana ya kujikana nafsi au kujinyima, au maana ya kuteseka kwa ajili ya neno la kweli. Lakini hakuna atakayeingia mbinguni pasipo kujinyima. Moyo wa kujikana nafsi na kujinyima wapasa kuthaminiwa. Wengine hawajitoi dhabihu miili yao wenyewe, madhabahuni mwa Mungu. Wanajifurahisha kwa moyo wa kigeugeu, mara kushika mara kuacha, na kuziridhisha tamaa zao za chakula, na kutimiza mapenzi yao wenyewe, bila kuijali kazi ya Mungu. Wale wenye kukubali kujinyima kitu kiwacho chote kwa ajili ya uzima wa milele wataupata; nao utakuwa kitu kistahilicho kuumia ili kukipata, cha kustahili kuiisulibisha nafsi kwa ajili yake, na kuacha miungu yote kwa ajili yake. Utukufu mwingi mno wa milele humeza kila kitu na kushinda anasa zote za dunia (IT 123-126).KN 48.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents