Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 36 - Malezi Bora na Mafundisho kwa Watoto Wetu

  MTAZAMO wa sasa ulimwenguni ni kuwaacha vijana kufuata nia zao wenyewe kwa kawaida. Na kama wakiwa wakaidi sana katika ujana wao, wazazi husema wataendelea vizuri baadaye kidogo wanapofikisha umri wa miaka kumi na sita au kumi na minane, watayapima mambo wenyewe, na kuacha mazoea yao mabaya, na hatimaye kuwa wanaume na wanawake wenye manufaa. Kosa gani! Kwa miaka mingi humwacha adui kupanda mbegu moyoni; huacha mafundisho mabaya kukua, na mara nyingi jitihada yote ya baadaye itakayofanywa juu ya mtu huyo haitakuwa na mafanikio yo yote.KN 215.1

  Shetani ni mwenye hila, fundi hodari, adui mkubwa. Wakati wo wote neno lisilo la akili likisemwa lenye kuwadhuru vijana, liwe kuwasifu mno wasivyostahili au kuwafanya wasichukie sana dhambi fulani, Shetani hulifaidi na kustawisha mbegu mbaya ipate kutelemsha mzizi na kuzaa mavuno mengi. Wazazi wengine wamewaacha watoto wao kuwa na mazoea mabaya, alama ambazo huweza kuonekana siku zote za maisha. Dhambi hiyo ni juu ya wazazi. Watoto hao waweza kujidai ni Wakristo, walakini, bila kazi maalumu ya neema moyoni na pasipo uongofu kamili maishani mazoea yao ya zamani yataonekana katika mambo yote ya maisha yao, na wataonyesha tabia ile ile ambayo wazazi wao waliwaacha kuwa nayo. 11T 403;KN 215.2

  Yawapasa wazazi kuwatawala watoto wao, kuzisahihisha tamaa zao, na kuwatiisha, ama sivyo Mungu atawaangamiza hao watoto siku ya hasira yake kali, na wazazi wasiowatawala watoto wao hawatakosa kuwa na hatia. Hasa ingewapasa watumishi wa Mungu kuwatawala watu wa nyumba zao wenyewe na kuwaweka chini ya utawala mzuri. Naliona kuwa hawako tayari kuhukumu wala kuamua mashauri ya kanisa, kama wasipoweza kutawala vizuri nyumba yao wenyewe. Kwanza hawana budi kuwa na utaratibu nyumbani, ndipo maamuzi yao na mvuto wao vitakuwa na matokeo kanisani. 21T 119;KN 215.3

  Kila mwana na binti angeitwa kutoa habari kama akikosekana nyumbani usiku. Yawapasa wazazi kujua marafiki za watoto wao na nyumba ya mtu wanamozitumia saa zao za jioni. 34T 651;KN 215.4

  Akili ya mwanadamu haijagundua zaidi ya kile Mungu ajuacho wala kubuni shauri bora zaiai juu ya namna ya kuwatendea watoto kuliko lile lililotolewa na Bwana wetu. Ni nani awezaye kuelewa vizuri zaidi mahitaji ya watoto kuliko Muumbaji wao?KN 215.5

  Ni nani awezaye kuyatilia moyo zaidi mambo yao kuliko Yeye aliyewanunua kwa damu yake mwenyewe? Kama neno la Mungu lingesomwa kwa uangalifu na kushikwa kwa uaminifu maumivu makuu ya roho juu ya tabia zilizopotoka za watoto waovu yangepungua.KN 216.1

  Watoto wanayo madai ambayo wazazi wao wapaswa kuyajua na kuyajali. Wana haki ya elimu na mafundisho yatakayowafanya kuwa wenye maana, wanaoheshimiwa na wenye kupendwa na watu hapa kuwapa hali ya tabia ya kufaa kwa jamii ya watu safi na watakatifu baada ya hapo. Vijana wangefundishwa kuwa hali yao ya wakati huu na lle ya wakati ujao pia hutegemea sana juu ya mazoea wanayofanya utotoni na katika siku za ujana. 4AH 306;KN 216.2

  Wanaume na wanawake wanaodai kuheshimu Biblia na kuyashika mafundisho yake hushindwa mara nyingi kutimiza masharti yake. Katika kuwafundisha watoto hufuata tabia zao wenyewe zilizopotoka badala ya mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa wazi. Kukosa kufanya wajibu huo huleta hasara kwa roho za watu maelfu. Biblia imeweka kawaida za malezi bora ya watoto. Kama masharti hayo ya Mungu yangefuatwa na wazazi, tungeona leo jamii ya vijana walio tofauti kabisa wenye kupiga hatua ya juu ya utendaji. Lakini wazazi wanaodai kuwa ni wasomaji wa Biblia na wafuasi wa Biblia wanafanya kinyume kabisa cha mafundisho yake. Tunasikia kilio cha huzuni na maumivu makuu kutoka kwa akina baba na mama wanaosikitikia tabia ya watoto wao, wasifahamu ila kidogo tu kwamba wanajiletea huzuni wao wenyewe na maumivu hayo, na kuwaharibu watoto wao waliopewa na Mungu kwa kutowazoeza watoto wao mazoea mema tokea utotoni. 54T 313;KN 216.3

  Watoto ambao ni Wakristo wataupendelea upendo na kibali cha wazazi wao wanaomcha Mungu zaidi ya mibaraka yote mingine ya duniani. Watawapenda na kuwaheshimu wazazi wao. Yafaa njia ya kuwafurahisha wazazi wao iwe mojawapo ya mambo makubwa wanayojifunza maishani mwao. Katika zama hizi za uasi, watoto hawajapata mafundisho na malezi bora, hawajui ila kidogo tu wajibu uwapasao kwa wazazi wao. Mara nyingi ndivyo ilivyo, yaani, kadiri wazazi wao wanavyowatendea mema, ndivyo wanavyozidi kutokuwa na shukrani na kutowaheshimu.KN 216.4

  Furaha ya wakati ujao ya watoto wao iko zaidi mikononi mwa wazazi. Kazi kubwa ya kuzirekebisha tabia za watoto hawa ni juu yao, mafundisho yaliyotolewa utotoni yatafuatana nao siku zote za maisha yao. Wazazi hupanda mbegu ambazo zitaota na kuzaa matunda ama kwa wema ama kwa ubaya. Huweza kuwafanya wana na mabinti zao kufaa kwa raha ama kwa hali mbaya sana. 61T 392, 393;KN 216.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents