Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 42 - Uaminifu Katika Kutunza Afya

    ANGALIA: Ujumbe huu wenye kutaja mara nyingine mambo makuu katika matengenezo ya afya ulitolewa na Mama White kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu mnamo mwaka 1909. Mkutano wa mwisho wa aina hiyo aliopata kuhudhuria.KN 263.1

    Nimeamuriwa kutoa ujumbe kwa watu wetu wote juu ya somo hili la matengenezo ya afya maana wengi wameasi na kuacna utii wao wa kwanza wa kanuni za matengenezo ya afya bora.KN 263.2

    Kusudi la Mungu kwa watoto wake ni ya kuwa waweze kukua hata kuufikia utu uzima wa wanaume na wanawake kwa Kristo. Kusudi kulitimiza hilo, hawana budi kutumia vizuri kila uwezo wa akili, na mwili. Hasara wawezayo kuipata kwa kutupa ovyo nguvu za akili ama za mwili ni kubwa mno.KN 263.3

    Swali juu ya jinsi ya kuitunza afya ni kubwa na la maana sana. Tunapolichunguza swali hili kwa kicho cha Mungu tutajifunza kuwa ni bora, kwa ajili ya maendeleo yetu ya mwili na ya roho pia, kushika kanuni za utovu wa chakula cha anasa. Basi, tulichunguze jambo hili kwa makini. Twahitaji maarifa na busara ili kuendelea kwa akili katika jambo hili. Sheria za asili si za kupingwa bali za kutiiwa.KN 263.4

    Wale ambao wamepokea mafundisho juu ya ubaya wa kutumia nyama, majani ya chai, na kahawa, pamoja na vyakula visivyofaa kwa afya, wenye kukusudia kufanya agano na Mungu kwa kujinyima, hawataendelea kuiendekeza tamaa yao ya chakula wanachojua kwamba si bora kwa afya. Mungu anadai kuwa tamaa ya chakula iwe safi, na ya kuwa kutumiwa kwa kiasi kitumiwe kwa habari ya vitu hivyo ambavyo si vizuri kwa afya. Hiyo ndiyo kazi ambayo itakuwa haina budi kutendwa kabla watu wake kuweza kusimama wakiwa wakamilifu mbele zake.KN 263.5

    Watu walio masalio wa Mungu hawana budi kuwa waongofu. Kuhubiri kwa ujumbe kumepasa kuleta uongofu na utakaso wa roho za watu. Yatupasa kuona moyoni uwezo wa roho ya Mungu katika kanisa hili. Huu ni ujumbe wa ajabu na wenye maana dhahiri; haupungui lo lote kwa mwenye kuupokea, nao hauna budi kuhubiriwa kwa sauti kuu. Yatupasa kuwa na imani ya kweli, idumuyo, ya kwamba ujumbe huu utatoka na kuzidi kuwa wenye maana mpaka mwisho.KN 263.6

    Wako wengine wanaodai kuwa ni waumini, wenye kukubali sehemu fulani tu za Shuhuda (Testimonies) hizi kama ujumbe wa Mungu, huku wakikataa sehemu zile zenye kukataza anasa zao wazipendazo. Watu kama hao wanafanya kinyume cha usitawi wao wenyewe na usitawi wa kanisa pia. Yafaa tuenende katika nuru maadam tunayo nuru. Wale wanaodai kuwa wanayaamini matengenezo ya afya, lakini wanafanya kinyume cha kanuni zake katika matendo ya maisha ya kila siku, kwa roho zao wenyewe na huacha mivuto mibaya mawazoni mwa waumini na mawazoni mwa wale wasioamini pia.KN 263.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents