Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 13 - Biblia

  KATIKA Maandiko Matakatifu maelfu ya vito vya thamani vya ukweli vimesetirika visionekane kwa mtafutaji wa juu juu. Shimo mnamochimbwa ukweli kamwe halimaliziki. Kadiri mnavyozidi kuyachunguza Maandiko Matakatifu kwa moyo mnyenyekevu, ndivyo mtakavyozidi kupendezwa, na kuzidi kuona moyoni mseme pamoja na Paulo: “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!” (Warumi 11:33).KN 99.1

  Kristo na Neno lake hupatana kabisa. Wakilipokea na kulisikia, hufungua njia imara kwa miguu ya wote ambao hupenda kuenenda katika nuru kama Kristo alivyo katika nuru. Kama watu wa Mangu wangelithamini Neno lake, tungekuwa na mbingu kanisani hapa chini. Wakristo watake sana, na kuwa na njaa, ya kulichunguza Neno hili. Washughulike wakati mwingine kulinganisha andiko moja na andiko lingine na kutafakari juu ya neno hili. Watamani zaidi nuru ya Neno hili kuliko magazeti ya kila siku asubuhi, au vitabu vya hadithi zisizo za kweli. Kitu ambacho wangalikitamani sana kingekuwa kula mwili na kunywa damu ya Mwana wa Mungu. Na matokeo yake yangekuwa kubadilishwa maisha yao ili yapatane na kanuni na ahadi za Neno la uzima. Lingekuwa ndani yao kisima cha maji, yakibubujikia uzima wa milele. Manyunyu ya neema yenye kuburudisha yangeburudisha na kuirudishia nguvu roho, ikiwafanya wasahau taabu yote na uchovu. Wangetiwa nguvu na moyo kwa maneno haya ya uongozi wa roho. 18T 193;KN 99.2

  Katika namna na mafundisno yake mbalimbali, Biblia inacho kitu cha kumpendeza kila mtu akilini na kuvuta moyo wa kila mmoja. Katika kurasa zake hupatikana historia ya zamani sana; maandiko ya habari za kweli kabisa za maisha ya mtu; kanuni za serikali kwa ajili ya kuitawala nchi, na kawaida za watu wa nyumbani,-kawaida ambazo kamwe hazilingani na hekima ya binadamu. Biblia ina elimu ya maana sana, utenzi mtamu kabisa na bora sana, wa kuingia moyoni na wa kutia huruma sana. Thamani ya maandiko ya Biblia ambayo haiwezi kupimika inaipa thamani kuu yakifikiriwa juu ya uhusiano wao na wazo lenye maana na lililo kubwa. Yakifikiriwa kwa wazo hili, kila kiini cha habari zake huwa chenye maana mpya. Katika maneno yaliyoelezwa kwa urahisi sana ya kweli kuna mafundisho yenye kimo kilichokwenda juu kama vile mbingu zilivyo nayo huenea hata milele. 2Ed. 125; KN 99.3

  Yawapasa kujifunza kitu fulani kipya kutoka kwa Maandiko Matakatifu. Yachunguzeni kama hazina lliyositirika, maana yana ndani yake maneno ya uzima wa milele. Mwombeni Mungu hekima na akili kuyafahamu haya Maandiko Matakatifu. Kama mtafanya hivi mtaona utukufu mpya katika neno la Mungu; mtaona moyoni mambo mbalimbali yahusianayo na ukweli; Maandiko Matakatifu yangethaminiwa upya kwenu. 35T 266;KN 100.1

  Maneno ya kweli ya Biblia, yakipokewa yatuinua moyo wa mtu kutoka katika hali yake ya kidunia na ubaya wake. Kama neno la Mungu lingethaminiwa kama ipasavyo, vijana na wazee pia wangekuwa na unyofu wa moyo, nguvu za mafundisho ambayo ingewezesha kuyapinga majaribu. 48T 319;KN 100.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents