Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Watenda Kazi wa Kufundisha Washiriki wa Kanisa

  Ni dhahiri kuwa mahubiri yote ambayo yamehubiriwa hayakukuza jamii kubwa ya watenda kazi wenye kujikana nafsi. Somo hili lapasa kufikiriwa kuwa ni la muhimu sana na lenye matokeo makubwa sana. Mustakabali wetu wa uzima wa milele umo hatarini. Makanisa yanafifia kwa sababu wamekosa kutumia talanta zao kueneza nuru. Mashauri ya uangalifu yapaswa kutolewa ambayo yatakuwa mafundisho kutoka kwa Bwana, kusudi wote wapate kuitumia nuru yao kwa njia ya kufaa. Wale ambao wanayasimamia makanisa wangechagua washiriki wenye uwezo na kuwapa kazi za madaraka, na wakati huo huo wakiwapa mashauri mema juu ya jinsi wawezavyo kuwatumikia na kuwafaidia wengine. 14 67431;KN 79.1

  Mafundi wa mashine, wanasheria, wafanyabiashara, watu wa namna zote za kazi na uchumi, hujielimisha ili wapate kuwa wajuzi stadi wa kazi zao. Je, yawapasa wafuasi wa Kristo kupungua akili, huku wakiwa wanadai kuwa wanamtumikia kazini mwake wasijue njia za kutumia? Uhodari wa kujipatia uzima wa milele ni jambo kubwa kuliko inavyoweza kudhaniwa duniani. Ili kuwaongoza watu kwa Yesu inalazimu pawepo ujuzi wa hali ya binadamu ya asili na kujifunza moyo wa mwanadamu. Mawazo yanayofikiriwa kwa uangalifu mwingi na kuomba daima hutakikana lli kujua jinsi ya kuwaendea wanaume na wanawake juu ya somo kuu la Neno la Mungu. 15 4T 67;KN 79.2

  Mara kanisa liishapo kuanzishwa, mchungaji na aweke washiriki kazini. Watahitaji kufundishwa namna ya kufanya kazi vizuri. Mchungaji na atumie saa zake nyingi zaidi katika kufundisha kuliko katika kuhubiri. Na awafundisne watu jinsi ya kuwapa wengine ujuzi waliopokea. Huku waongofu wapya wakipaswa kufundishwa kutaka shauri jema kutoka kwa wale wenye maarifa mengi kazini, hawana budi pia kufundishwa kutomweka mchungaji mahali pa Mungu.KN 79.3

  Msaada mkuu kabisa wawezao kupewa watu wetu ni kuwa-fundisha kumtumikia Mungu, na kumtegemea, wala si kuwategemea wachungaji. Hebu wajifunze kufanya kazi kama Kristo alivyofanya kazi. Nawajiunge na jeshi lake la watenda kazi na kumtumikia kwa uaminifu. 16 77 19, 20;KN 80.1

  Walimu wanaonyesha njia katika kufanya kazi miongoni mwa watu, na wengine, wakiungana nao, watajifunza kwa kielelezo chao. Kielelezo kimoja chafaa zaidi ya mafundisho mengi. 17 MH 149;KN 80.2

  Wale wenye kulisimamia kanisa kwa mambo ya kiroho yawapasa kuvumbua njia ambazo kwazo nafasi yaweza kutolewa kwa kila mshiriki wa kanisa kushiriki kazini mwa Mungu. Hili si jambo lililofanywa siku zote zamani? Mipango haikutimizwa kabisa ambayo kwayo talanta za wote zaweza kutumiwa jeshini. Wengi hawafahamu hasara ambayo imepatikana kwa sababu ya jambo hili.KN 80.3

  Katika kila kanisa kuna talanta, ambayo kwa kazi nzuri, yaweza kukuzwa kuwa msaada mkubwa katika kazi hii. Yapasa pawepo mpango mzuri kwa kuwaajiri watenda kazi kuyatembelea makanisa yetu yote, makubwa na madogo, kuwafundisha washiriki wa kanisa kufanya kazi kwa ajili ya kulijenga kanisa, na pia kwa ajili ya wale wasioamini. Mafunzo, elimu, ndiyo inayotakiwa. Hebu wote wanuie moyoni mwao na akilini mwao kuwa wenye akili kwa habari za kazi ya wakati huu, wakijistahilisha kufanya kile ambacho ni chenye kufaa vizuri kukitenda.KN 80.4

  Kinachohitajika sasa kwa ajili ya kuyajenga makanisa yetu ni kazi nzuri ya watenda kazi wenye busara kuona na kukuza talanta kanisani-talanta ambayo huweza kukuzwa na kuongozwa vizuri kwa ajili ya kazi ya Bwana. Wale ambao watafanya kazi ya kuyatembelea makanisa wangewapa ndugu na dada mashauri ya njia za kufaa za kuifanya kazi ya utume. Hebu pawepo na darasa la mafundisho kwa vijana pia. Vijana wa kiume na wa kike wanapaswa kufundishwa kuwa watenda kazi nyumbani, jirani na kwao, na kanisani. 18 An Appeal to Ministers and Church Officers;KN 80.5

  Malaika wa mbinguni wamekuwa wakingojea muda mrefu mawakili wanadamu-wasniriki wa kanisakushirikiana nao katika kazi hii kuu inayohitajika kufanywa. Wanakungojea. Mahali pa kazi ni pakubwa sana, na azimio lake lina mambo mengi pia, hata kila moyo uliotakaswa utavutwa kuingia kazini kama chombo cha uwezo wa Mungu. 19 97 46, 47;KN 80.6

  Kama Wakristo wangetenda mambo kwa umoja, wakisonga mbele kama mtu mmoja, chini ya maongozi ya Uwezo mmoja, kwa ajili ya kutimiza kusudi moja, wangetingisha ulimwengu. 2097221;KN 80.7

  Mwito wa kutolewa katika “njia kuu” hauna budi kutangazwa kwa wote wenye sehemu ya kutenda katika kazi ulimwenguni humu, kwa walimu na kwa viongozi wa watu. Wale wenye kazi za madaraka makubwa katika maisha ya watu-madaktari na walimu, wanasheria na mahakimu maafisa wa mambo ya serikali na wafanyabiashara wanapaswa kupewa ujumbe dhahiri. “Itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?” (Marko 8:36, 37).KN 80.8

  Tunazungumza na kuandika mengi juu ya maskini waliotupwa; je, haipasi kuangalia pia matajiri waliotupwa? Wengi huwanesabu watu wa jamii hii kama wasio na matumaini, nao hufanya kiasi kidogo tu kuyafumbua macho ya wale ambao, kwa kupofushwa na kupumbazwa na nguvu za Shetani, wamepotewa na uzima wa milele katika hesabu yao. Maelfu ya matajiri wamekufa na kwenda makaburini mwao bila kuonywa kwa sababu wamepimwa kwa umbo la nje na kupitwa kando kama watu wasio na matumaini. Lakini, kinyume cha wanavyoonekana, nimeonyeshwa kuwa wengi wa watu wa jamii hii ni wenye kulemewa rohoni. Kuna maelfu ya matajiri wanaoumia kwa kukosa chakula cha kiroho. Wengi katika maisna yao ya kila siku huona haja yao ya kitu wasicho nacho. Wengi wao hawaendi kanisani, maana huona kwamba hawapati faida. Mafundisho wanayoyasikia hayagusi moyo. Je, tusijitanidi kwa ajili yao?KN 81.1

  Wengine watauliza: Hatuwezi kuwafikia kwa vitabu na magazeti? Kuna wengi wasioweza kufikiwa kwa njia hii. Wanahitaji kuendewa. Je wafe bila kupewa onyo maalum? La, sivyo ilivyokuwa zamani za kale. Watumisni wa Mungu walitumwa kuwaambia wale walio na vyeo kwamba wangeweza kupata amani na raha kwa Bwana Yesu Kristo tu.KN 81.2

  Mfalme wa mbinguni alikuja ulimwenguni mwetu kuokoa wanadamu waliopotea, na waliotenda dhambi. Kazi yake haikuwa kwa wale waliotupwa tu bali pia kwa wale wenye madaraka na heshima. Kwa akili alifanya kazi kupata njia ya kuzifikia roho za watu wa vyeo vikubwa wasiomjua Mungu na wasiozishika amri zake.KN 81.3

  Kazi ile ile ilipaswa kuendelea baada ya kufa kwa Kristo. Moyo wangu umeumizwa sana nikisoma mambo yaliyofunuliwa na Bwana kwa Komelio. Komelio alikuwa mtu mwenye kazi ya madaraka, afisa katika jeshi la askari la Kirumi, lakini alikuwa akienenda kwa kuifuata sana num yote aliyokuwa ameipokea. Mungu akampelekea ujumbe maalum kutoka mbinguni, na kwa ujumbe mwingine uliomwongoza Petro kufika kwake na kumpa num. Lapaswa kuwa jambo kubwa la kututia moyo kazini mwetu kufikiri juu ya humma na upendo wa Mungu kwa wale ambao wanatafuta na kumwomba Mungu nuru.KN 81.4

  Wako wengi ambao nimewaonyeshwa wenye kufanana na Komelio, watu ambao Mungu anataka sana wajiunge na kanisa lake. Humma zao ni juu ya watu wazishikao amri za Mungu. Lakini nyuzi zinazowarunga kwa ulimwengu huwashika imara. Hawana moyo wa adili kutwaa mahali pao pamoja na wanyenyekevu wa moyo. Yatupasa kufanya bidii maalum kwa ajili ya roho za watu hawa, ambao wanahitaji kazi maalum kwa sababu ya madaraka yao na majaribu.KN 81.5

  Kwa nuru niliyopewa, nimeonyeshwa ya kuwa hata watu wenye madaraka, walio viongozi duniani, wanapaswa kuambiwa dhaniri lile neno la “Ndivyo asemavyo Bwana.” Ni mawakili ambao Mungu amewakabidhi amana kubwa. Kama watauitikia mwito wake, Mungu atawatumia kazini mwake KN 82.1

  Kuna wengine ambao hufaa hasa kwa kazi kwa jamii za watu wakubwa. Hawa imewapasa kumtafuta Mungu kila siku, kulifanya jambo la kujifunza kujua jinsi ya kuwafikia watu hawa, siyo mazungumzo ya kubahatisha tu kujuana nao bali kuwashikilia kwa mahubiri na kwa imani yenye nguvu, yenye kuonyesha upendo mwingi kwa ajili ya roho zao, kutia nia hasa ili wapate ujuzi wa kweli kama ilivyo katika Neno la Mungu. 216778 - 81.KN 82.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents