Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shirika za Biashara na Walimwengu

  Wengine hawana werevu wo wote wa mambo ya ulimwengu. Hawana sifa zitakikanazo, na Shetani huwafaidi. Mambo yakiwa hivi, watu kama hawa hawataendelea kukosa kujua kazi yao. Yawapasa wawe wanyenyekevu kiasi cha kutosha kushauriana na ndugu zao, ambao huutumainia uamuzi wao, kabla ya kutimiza mipango. Naliongozwa kwa fungu hili la Biblia: “Mchukuliane mizigo na kutimiza hivyo sheria ya Kristo.” (Wagalatia 6:2). Wengine si wanyenyekevu kiasi cha kuwaacha wale wenye busara kuwafikiria mambo hata wamefuata mipango yao wenyewe, na wamejitia shidani wenyewe. Ndipo huona haja ya kupata shauri na uamuzi wa ndugu zao; lakini mzigo huu huwa mzito jinsi gani zaidi ya hapo kwanza. Ndugu wasiende kushtaki katika baraza la hukumu kama ikiwezekana waepuke kufanya hivyo; maana kwa kufanya hivi humpa adui nafasi kubwa kuwatega na kuwatatiza. Ingekuwa heri kufanya mapatano ijapokuwa pawepo hasara.KN 97.3

  Naliona kuwa alichukizwa na watu wake kuwa wadhamini wa wale wasioamini. Naliongozwa kwa mafungu haya ya Biblia: Mithali 22:26: “Usiwe mmoja wao wapanao mikono, au walio wadhamini kwa deni za watu.” Mithali 11:15: “Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; achukiaye mambo ya dhamana yu salama.” Mawakili wasio waaminifu! Huwekea dhamana kile ambacho ni mali ya mwingine-Baba yao aliye mbinguni-na Shetani husimama tayari kuwasaidia watoto wake kuwavuta ghafula kwa nguvu kutoka mikononi mwa watu wa Mungu. Yawapasa waishikao Sabato wasishirikiane na wale wasioamini. Watu wa Mungu wanayaamini sana maneno ya wale wasio waaminifu, na huuliza shauri la msaada mawakili wake, na huwatumia kuwatatiza na kuwanyang’anya watu wa Mungu. 71T 200, 201.KN 98.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents