Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kristo Katika Biblia Nzima

    Uwezo wa Kristo, Mwokozi aliyesulibiwa ambao unaweza kutoa uzima wa milele, hauna budi kutolewa kwa watu. Yatupasa kuwaonyesha kuwa Agano la Kale ni Injili kweli katika mifano na vivuli vya mambo yajayo kama Agano Jipya lilivyo katika uwezo wake ambao umefunuliwa. Agano Jipya halitoi dini mpya; Agano la Kale halitoi dini ya kubatilishwa na Agano Jipya. Agano Jipya ni mwendelezo na mafunuo tu ya Agano la Kale.KN 103.3

    Habili alikuwa mwenye kumwamini Kristo, naye kwa kweli alikuwa mwenye kuokolewa na uwezo wake Kristo kama Petro au Paulo. Henoko alikuwa mjumbe wa Kristo hakika kama alivyokuwa Yohana yule mwanafunzi mpendwa. Henoko alikwenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. Huyu alikabidhiwa ujumbe wa kuja kwa Kristo mara ya pili. “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia Bwana alikuja na watakatifu wake maelfu elfu, ili afanye hukumu juu ya wote.” (Yuda 14). Ujumbe aliohubiri Henoko na kule kutwaliwa kwake mbinguni ulikuwa hoja kubwa ya kuwasadikisha wote walioishi siku zake. Mambo haya yalikuwa hoja ambayo Methusela na Nuhu waliweza kuitumia kwa nguvu kuonyesha kuwa wenye haki huweza kuhamishwa.KN 103.4

    Yule Mungu aliyetembea pamoja na Henoko alikuwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yeye alikuwa nuru ya ulimwengu wakati ule kama alivyo sasa. Wale walioishi wakati ule hawakukosa walimu wa kuwaongoza katika njia ya uzima; maana Nuhu na Henoko walikuwa Wakristo. Injili unetolewa katika mafundisho ya Mambo ya Walawi. Utii kamili unatakiwa sasa, kama ulivyotakiwa wakati ule. Ni jambo muhimu kama nini kwamba tunaufahamu ukubwa wa neno hili!KN 104.1

    Swali ni kwamba: Asili ya upungufu kanisani ni nini? Jibu ni hili: “Tunaacha akili zetu kupotoshwa kutoka kwa Neno hili. Kama Neno la Mungu lingeliwa kama chakula cha rohoni kama lingeelezwa kwa heshima na unyenyekevu, pasingelazimu kuwa na shuhuda nyingi ambazo hutolewa mara kwa mara. Mahubiri mepesi ya Biblia yangepokewa na kufuatwa. 146T 392, 393KN 104.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents