Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuzeni Upendo wa Mambo ya Kiroho

  Usalama tu kwa vijana ni kukesha kila wakati na kuomba kwa moyo mnyenyekevu. Wasijidanganye kwamba wanaweza kuwa Wakristo bila mambo hayo. Shetani huficha majaribu na hali zake na kuwafunika kwa nuru kama alivyofanya alipomshawishi Kristo jangwani. Alionekana kama mmojawapo wa malaika wa mbinguni. Yule adui wa roho zetu atujia kama mgeni wa mbinguni, na mtume atoa shauri kuwa kiasi na kukesha ndiyo tu salama yetu. Vijana ambao hujitayarisha kwa anasa bila kujali, na wasiofanya wajibu uwapasao Wakristo, daima huanguka katika majaribu ya adui, badala ya kushinda kama Kristo alivyoshinda. 23T 374;KN 213.1

  Wengi hudai kuwa upande wa Bwana, lakini sivyo; uzito wa matendo yao yote umo upande wa Shetani. Kwa njia gani tutaweza kuyakinisha tuko upande gani? Ni nani mwenye moyo? Mawazo yetu ni juu ya nani, na nguvu zetu? Ikiwa tuko upande wa Bwana, mawazo yetu ni kwake, na mafikara yetu bora ni juu yake. Hatuna urafiki na ulimwengu, tumetoa wakfu vyote tulivyo navyo, ni vyake. Twatamani kuwa na sura yake, na kumpendeza katika mambo yote. 32T 262, 266KN 213.2

  Elimu ya kweli ni uwezo wa kutumia akili zetu makusudi kupata matokeo yenye faida. Mbona basi dini tunaifikiria kidogo hivi huku mambo ya ulimwengu yakiwa na nguvu ubongoni, mifupani, na kwenye misuli? Sababu ni kwamba nguvu zote za mwili wetu zimeelekezwa upande huo. Tumejizoeza kushughulika kwa bidii na nguvu katika mambo ya kidunia mpaka imekuwa vyepesi kuwa Mungu ametujalia vipawa vikuu vyenye thamani. Ametupa nuru na ujuzi wa mapenzi yake, hata hatuna sababu ya kufanya kosa wala kutembea gizani. Kupimwa katika mizani na kuonekana kuwa umepungua siku ile ya kukatwa shauri la mwisho na kutolewa ijara litakuwa jambo la kutisha, kosa baya sana lisiloweza kusahihishwa tena. Vijana rafiki zangu, je majina yenu hayatapatikana katika kitabu cha Mungu? 42T 266, 267;KN 213.3

  Mungu amewapa kazi ya kumfanyia ambayo itawafanva ninyi kuwa watenda kazi pamoja naye. Pande zote kuwazunguka kuna roho za watu zinazotaka kuokolewa. Wako wale mwenzao huwatia nguvu na kuwafanya kuwa wenye hali ya heri kwa jitihada zetu. Mwaweza kuziongoa roho za watu kwenye haki kutoka dhambini. Mkijua wajibu wenu kwa Mungu mtaona moyoni mwenu haja ya uamimfu katika kuomba na uaminifu katika kukesha msiingie kwenye majaribu ya Shetani. Ikiwa ninyi ni Wakristo kwa kweli, mtapenda zaidi moyoni kuhuzunikia giza la mambo matakatifu52T 267, 268; badala ya kujifurahisha kwa anasa na kiburi cha bure cha mavazi. Mtakuwa miongoni mwa wale wenye kupiga kite na kulia juu ya machukizo yatendwayo nchini. Mtayapinga majaribu ya Shetani msiingie kwenye majivuno na kujipamba kwa mapambo mengi ya fahari. Ubongo hudhoofishwa na akili hudunishwa ikiridhishwa na mambo hafifu na kutojali wajibu ulio bora. 63T 368-370KN 213.4

  Vijana siku hizi huweza kuwa watenda kazi pamoja na Kristo wakipenda, na wakitenda kazi, imani yao itatiwa nguvu na ujuzi wao wa mambo matakatifu utaongezeka.. Kila kusudi la kweli na kila tendo la haki litaandikwa katika kitabu cha uzima. Laiti ningeweza kuwaamsha vijana kuona na kusikia moyoni hali ya dhambi ya kuishi kwa kujifurahisha wenyewe kwa anasa na kudumaza akili zao katika mambo hafifu, yasiyo na maana ya maisha haya. Kama wangeinua mawazo na maneno yao juu zaidi ya mivuto hafifu ya ulimwengu huu na kuwa na kusudi la kumtukuza Mungu, amani yake, ipitayo ufahamu wote, wangeipata. 73T 370, 371;KN 214.1

  Mungu ataka vijana kuwa watu wenye mioyo hodari, kutayarishwa kuitenda kazi yake bora, na kufanywa wafae kuchukua madaraka. Mungu awaita vijana wenye mioyo safi, wenye nguvu na hodari, na wenye kukusudia kupigana kiume katika vita vilivyo mbele yao, ili wapate kumtukuza Mungu, na kuwanufaisha wanadamu. Ikiwa vijana wangeifanya Biblia kuwa somo lao, wangeweza kutuliza tamaa zao mbaya, na kuisikiliza sauti ya Muumbaji wao, licha ya kuwa na amam na Mungu, hata wangejiona kuwa wameadilishwa na kuzidishwa hadhi.KN 214.2

  Chukua nuru po pote uendako; onyesha kuwa unalo kusudi lenye nguvu, kwamba hu mtu wa mashaka, mwenye kupelekwa huko na huko na vishawishi vya marafiki wabaya. Usikubali kwa urahisi mashauri ya wale wenye kumdharau Mungu, lakini jaribu kuongoa, ongoza vema, na kuokoa roho za watu toka maovuni.KN 214.3

  Rudia kuomba, ongoza kwa upole na unyenyekevu wa moyo wale wanajipinga wenyewe. Roho ya mtu mmoja anayeokoka kutoka katika kutenda mabaya, na kuletwa chini ya bendera ya Kristo italeta furaha mbinguni, na kutia nyota ya furaha tajini mwako. Mtu aliyeokolewa, kwa njia ya mvuto wake mwema, ataleta watu wengine kuujua wokovu, na kwa hiyo kazi hii itazidi, na mafunuo tu ya siku ile ya hukumu ndiyo yatakayodhihirishwa jinsi kazi hiyo ilivyoenea.KN 214.4

  Usisite kumtumikia Bwana kwa uaminifu; maana Mungu atafanya kazi na jitihadi zako. Ataliandika jina lako katika kitabu cha uzima kama mwenye kustahili kuingia katika furaha ya Bwana. 8MYP 21 -23.KN 214.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents