Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mungu Baba Amefunuliwa kwa Njia ya Kristo

  Mungu aliye nafsi ya pekee, amejifunua mwenyewe kwa njia ya Mwanawe. Yesu, mng’ao wa utukufu wa Baba, “chapa ya nafsi yake” (Waebrania 1:3), alionekana duniani katika umoo la mwanadamu. Yeye aliye Mwokozi wa pekee alikuwa ulimwenguni humu, na alipaa juu. Sasa Mwokozi huyu wa pekee huwaombea watu mbinguni. Mbele za kiti cha enzi cha Mungu huhudumu kwa ajili yetu “Mtu mfano wa Mwanadamu (Ufunuo 1:13).KN 87.2

  Kristo, Nuru ya ulimwengu, alivua utukufu wenye kutia kiwi machoni kwa mng’ao wake ambao alikuwa nao katika hali yake ya Uungu akaja kukaa kama mtu miongoni mwa wanadamu, ili wapate, pasipo kuteketezwa, kujua habari za Mwumbaji wao. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote isipokuwa kama alivyofunuliwa kwa njia ya Kristo.KN 87.3

  Kristo alikuja kuwafundisha wanadamu jambo Mungu alilotaka sana walijue. Mbinguni juu, duniani, baharini, tawaiona kazi ya mikono ya Mungu. Viumbe vyote huushuhudia uwezo wake, hekima yake, na upendo wake. Lakini hatuwezi kujifunza kutoka kwa nyota au bahari au maporomoko ya maji habari za nafsi ya Mungu kama ilivyofunuliwa kwa njia ya Kristo.KN 87.4

  Mungu aliona kuwa mafunuo dhahiri zaidi ya viumbe vya asili yalitakikana kueleza nafsi yake na tabia yake pia. Alimtuma Mwanawe ulimwenguni kufunua, kadiri ambavyo macho ya wanadamu yangaliweza kustahimili, tabia na sifa za Mungu asiyeonekana.KN 87.5

  Kama Mungu angetaka kuelezwa kana kwamba Yeye Mwenyewe hukaa katika viumbe vya asili-ndani ya ua, mti, ncha za majani, -Kristo hangewaambia neno hili wanafunzi wake alipokuwa duniani? Lakini kamwe Mungu hakunenwa hivi katika mafundisho ya Kristo. Kristo na mitume walifundisha dhahiri ukweli wa kuwako kwa Mungu wa pekee.KN 87.6

  Kristo alifunua habari zote za Mungu ambazo wanadamu wenye dhambi wangeweza kustahimili pasipo kuangamizwa. Yu Mwalimu wa mambo ya Mungu mwenye kutia nuru. Kama Mungu angetufikiria kuwa tunahitaji mafunuo mengine kuliko vale yaliyofunuliwa kwa njia ya Kristo na katika Neno lake lililoandikwa, angeweza kuyatoa.KN 87.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents