Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hatari Katika Kuwapeleka Watoto Shuleni Wakiwa Wangali Wadogo Sana

  Kama wale waliokaa Edeni walivyojifunza kutoka kwa viumbe vya asili, kama Musa alivyouona mwandiko wa Mungu juu ya tambarare na milima ya Arabia, na kama Mtoto Yesu alivyoona juu ya mitelemko ya vilima vya Nazareti, ndivyo siku hizi wawezavyo kuona na kujifunza habari za Mungu. Mambo yale yasiyoonekana hufafanuliwa na yale yanayoonekana.KN 236.1

  Basi, kadiri iwezekanavyo, mtoto awekwe tokea utotoni kabisa mahali ambapo kitabu hiki cha ajabu cha mafundisho kinweza kufunuliwa mbele yake. 28ED.100,101 ;KN 236.2

  Msiwapeleke watoto wenu shuleni mapema mno. Yafaa mama aangalie sana jinsi anavyomwamini mtu mwingine kumfundisha mtoto wake mchanga, na kukuza tabia yake. Yawapasa wawe walimu bora kabisa wa watoto wao mpaka watoto wafikishapo umri wa miaka minane au kumi. Chumba chao cha kusomea kingekuwa nje, katika maua na ndege, na kitabu cha mafundisho yao kingekuwa viumbe wa asili. Mara wawezapo kufahamu kwa akili zao wenyewe, wazazi wawafunulie kitabu hiki kikubwa cha Mungu cha viumbe. Mafundisho haya yatolewayo mahali pa namna hii hayatasahaulika upesi. 29FE.156,157KN 236.3

  Licha ya afya ya mwili na ya akili ya watoto kuhatarishwa kwa kupelekwa shuleni mapema sana, hata wamekuwa wenye kupatwa na hasara katika mambo ya tabia ya uadilifu. Wanakuwa na nafasi kufahamiana na watoto waliokuwa washenzi kwa tabia zao wanatupwa katika jamii ya washenzi wasio na adabu, wasemao uongo, watukanaji, wevi, na wadanganyifu, na wenye kufurahia kuyashirikisha mafundisho yao maovu kwa wale walio wadogo kuliko wao wenyewe. Watoto wadogo, kama wakiachwa peke yao, hujifunza mabaya upesi zaidi ya mema. Mazoea mabaya hupatana sana na moyo wa asili, na mambo wanayoyaona na kuyasikia utotoni wakiwa wangali wachanga hukazwa akilini mwao; na mbegu mbaya iliyopandwa katika mioyo yao michanga itatia mzizi nayo itakuwa miiba mikali yenye kuijeruhi mioyo ya wazazi wao. 30CG.302;KN 236.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents