Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mungu ataka Sana Kutoa Kipawa cha Roho Mtakatifu

  Jitihada maalumu zinapofanywa na watenda kazi wenye ujuzi mwingi katika mtaa wakaapo watu wetu waumini wenyewe wa mahali hapo wana wajibu mkubwa sana kufanya yote wawezayo kufungua njia kwa ajili ya Bwana kufanya kazi. Yawapasa kuchunguza mioyo yao kwa kuomba kwa bidii na kusafisha njia kuu ya Mfalme kwa kuondoa kila dhambi ambayo ingewazuia wasishirikiane na Mungu pamoja na ndugu zao.KN 76.1

  Katika njozi za usiku, maelezo yalipitishwa mbele yangu, ya matengenezo miongoni mwa watu wa Mungu. Wengi walikuwa wanamsifu Mungu. Wagonjwa waliponywa, na miujiza mingine ikafanywa. Roho ya maombezi ikaonekana, kama ilivyodhihirishwa mbele ya siku kuu ya Pentekoste. Mamia na maelfu wakaonekana wakizuru watu wa nyumba mbalimbali na kuwafunulia Neno la Mungu. Mioyo ikasadikishwa hatia ya dhambi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, na moyo wa uongofu wa kweli ukadhihirishwa. Kila upande milango ikafunguliwa kwa ajili ya kuhubiriwa Neno la Mungu. Ulimwengu ukaonekana kana kwamba uliangazwa kwa mvuto wa mbinguni na unyenyekevu wa moyo. Nikasikia sauti za shukrani na sifa, na ikaonekana kuwa kama yale matengenezo tuliyoona mwaka 1844. 6 9T 125, 126;KN 76.2

  Mungu anataka sana kuwaburudisha watu wake kwa kipawa cha Roho Mtakatifu, akiwabatiza upya katika pendo lake. Hakuna sababu ya ukosefu wa Roho kanisam. Baada ya kupaa kwa Kristo, Roho Mtakatifu aliwashukia wale wanafunzi waliokuwa wakingojea, wakisali, na kuamini kwa uwingi na nguvu hata kuufikia kila moyo. Wakati ujao dunia haina budi kuangazwa kwa utukufu wa Mungu. Mvuto mtakatifu hauna budi kutoka kuwaendea walimwengu kutoka kwa wale ambao wametakaswa kwa kweli. Dunia haina budi kuzungukwa na mambo yavutayo mtu kuona neema. Roho Mtakatifu hana budi kufanya kazi moyoni mwa wanadamu, akitwaa mambo ya Mungu na kuyaonyesha kwa wanadamu. 7 9T40:KN 76.3

  Mungu anapenda kufanya kazi kubwa kwa ajili ya wote wanaomwamini kwa kweli. Kama washiriki wa kanisa wasio watenda kazi walipwao mshahara wataondoka na kufanya kazi wawezayo kufanya, wakienda vitani kwa gharama zao wenyewe kila mmoja akiona kiasi awezacho kufanya katika kuongoza roho za watu kwa Yesu, tutaona wengi wakiacha kazi ya uaskari wa Shetani ili kusimama chini ya bendera ya Kristo. Kama watu wetu wataendesha nuru ambayo imetolewa kwa maneno haya machache ya mafundisho, (Yohana 15:8), yamkini tutaona wokovu wa Mungu. Uamsho wa ajabu utafuata. Wenye dhambi wataongoka na roho za wengi zitaongezwa kanisani. Tukiingiza mioyo yetu kwenye umoja na Kristo, na kuyapatanisha maisha yetu na kazi yake, roho iliyowashukia wale wanafunzi siku ya Pentekoste itatushukia. 8 8T246;KN 76.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents