Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wafuasi wa Kweli wa Kristo Watamshuhudia

    Kama kila mmoja wenu angekuwa mmishenari mwenye nguvu, ujumbe wa wakati huu ungehubiriwa kwa nguvu sana katika nchi zote, kwa kila taifa, na kabila na lugha. 66T 438;KN 68.2

    Wote wapendao kuingia mji wa Mungu hawana budi katika maisha yao hapa duniani kumtangaza Kristo katika shughuli zao. Hili ndilo linalowafanya wajumbe wa Kristo, mashahidi wake. Wamepaswa kutoa ushuhuda dhahiri, wa nguvu kuipinga mivuto yote mibaya, wakiwaelekeza wenye dhambi kwa Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu. Huwapa wote wanaompokea, uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Uongofu ni njia tu ambayo kwayo twaweza kuuingia mji wa Mungu. Imesonga, na mlango tunaoingilia ni mwembamba, lakini njia hiyo ndiyo tupaswayo kuwaongoza wanaume na wanawake na watoto kupitia, tukiwafundisha kuwa, ili kuokoka, hawana budi kuwa na moyo mpya na roho mpya. Utu wa kale, tabia za kurithiwa hazina budi kushindwa. Tamaa za mwili za asili hazina budi kuongolewa. Udanganyifu wote, uongo wote, na mazungumzo yote mabaya hayana budi kuachwa. Maisha mapya, ambayo huwafanya wanaume na wanawake kufanana na Kristo, hayana budi kufuatwa. 7.KN 68.3

    Ndugu na dada, mnataka kuvunja mvuto unaowashika? Mnapenda kuamka na kutoka katika mazoea haya ya uvivu ambayo ni kama usingizi wa mauti? Nendeni mkafanye kazi, haidhuru mnajisikia au hamjisikii hivyo moyoni . Jishughulisheni na mahubiri ya Injili ninyi wenyewe kuwaleta watu kwa Yesu na katika kulijua Neno la Mungu. Katika kila kazi mtaona kichocheo na dawa ya kutia afya na nguvu zenu za kiroho zitazidi kuongezeka, ili mweze kuushughulikia wokovu wenu wenyewe vizuri zaidi. Hali ya kuzimia imewapata wengi wanaomkiri Kristo. Onya, lalama, gombeza. Ijapokuwa wanaweza kukataa kusikia, kazi yako haitakuwa ya bure. Katika kufanya bidii kuwabariki wengine roho zenu wenyewe zitabarikiwa. 85T387;KN 68.4

    Pasiwepo na mtu ye yote anayeona moyoni kuwa kwa sababu hawakuelimika, hawawezi kushiriki kazini mwa Mungu. Waweza kuyachunguza Maandiko Matakatifu wewe mwenyewe. “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga” (Zaburi 119:130). Waweza kuiombea kazi hii. Sala ya moyo mnyofu, ikiombwa kwa imani, itasikiwa mbinguni. Nanyi yawapasa kufanya kazi kadiri ya uwezo wenu mlio nao. 96T433;KN 69.1

    Malaika wa mbinguni wanangojea kushirikiana na vyombo vya kibinadamu, ili wapate kuwadhihirishia walimwengu kile wanadamu wawezacho kuwa na kile ambacho, kwa njia ya mvuto wao, waweza kukitimiza kwa ajili ya wokovu wa roho za watu ambao wako tayari kupotea.KN 69.2

    Kristo anatuita kufanya kazi kwa uvumilivu na kwa kuendelea kwa bidii kwa ajili ya maelfu wanaopotea dhambini mwao, walioenea katika nchi zote, kama mabaki ya vitu vilivyoharibika ukingoni mwa jangwa. Wale wanaoushiriki utukufu wa Kristo hawana budi kushiriki pia kazini mwake, kuwasaidia wadhaifu, maskini, na waliokata tamaa. 10 9T30, 31;KN 69.3

    Kila muumini anapaswa kuwa na upendo kamili kwa kanisa. Mafanikio ya kanisa yapaswa kuwa jambo lake la kwanza linalompendeza. Kanisa lisipofaidika na ushirika wake ingekuwa heri asingekuwapo mshiriki maana hapo kanisa lingesaidiwa kwa kutokuwa na mzigo wa bure. Ni hiari ya wote kufanya kitu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Wako wale ambao hutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa anasa zisizo na maana; wanajiridhisha tamaa zao, lakini huona kuwa ni mzigo mkubwa sana kutoa mali kulisaidia kanisa. Wanapenda kupokea manufaa yote ya majaliwa ya kanisa, lakini hupendelea kuwaacha wengine kulipa fedha. 1118;KN 69.4

    Kanisa la Kristo laweza kufananishwa vyema na jeshi. Maisha ya kila askari yamejaa taabu, shida, na hatari. Kila upande, wako maadui walio macho, wenye kuongozwa na mkuu wa mamlaka za giza, ambaye kamwe hasinzii wala hatoroki na kuacha lindo lake. Mkristo aachapo kukesha zamu yake, huyu adui hodari hufanya shambulio la ghafula. Ikiwa washiriki wa kanisa hawatakuwa hodari na wenye bidii, watashindwa na hila zake.KN 69.5

    Itakuwaje kama nusu ya askari jeshini wakiwa wavivu na walegevu au wakilala wanapoamriwa kuwa kazini? Matokeo yake yatakuwa kushindwa, kutekwa, au mauti. Wakiwapo askari wo wote katika hao wanaoponyoka mikononi mwa yule adui, wangehesabiwa kuwa wenye kustahili thawabu? La; wangepokea mara hiyo hukumu ya kufa. Kadhalika ndivyo ilivyo na kamsa la Kristo likikosa uangalifu au uaminifu; madhara ya baadaye yatakuwa makubwa zaidi sana. Jeshi la Kikristo lenye kulala usingizi-jambo gani la kutisha kuliko hili! Ni maendeleo gani yangaliweza kufanywa juu ya walimwengu, ambao wako chini ya mamlaka ya mkuu wa giza? Wale wanaosimama nyuma bila kujali siku ya mapigo, kana kwamba hawayatilii maanani mambo hayo, ni heri wabadili mwenendo wao au kuacha kabisa uaskari mara moja. 125T394;KN 69.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents