Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mungu Huwapima Wale Anaowathamini

  Ukweli kwamba tumeitwa kustahimili taabu yaonyesha kuwa Bwana Yesu aona ndani yetu kitu cha thamani sana, ambacho anataka kukikuza. Kama hangeona cho chote ndani yetu ambacho kwacho aweza kutukuza jina lake asingetumia wakati wake kututakasa. Hatujisumbui kupunguzia miiba matawi. Kristo hatupi kwenye tanuru lake mawe yasiyo na thamani. Mawe ya madini ya thamani ndiyo anayoyapima. 107T214;KN 63.3

  Kwa watu ambao hukusudia washike kazi za madaraka, kwa rehema hudhihirisha makosa yao yaliyositirika, ili waweze kuona na kuchunguza mahangaiko yanayowatatiza moyoni na mashindano ya mioyom mwao, na kuona neno lililo baya; hivyo waweza kugeuza tabia zao na kubadilisha njia zao. Mungu kwa majaliwa yake huwaleta wanadamu mahali awezapo kupima uwezo wa tabia zao za moyoni na kudhihirisha makusudi ya matendo yao, kusudi wapate kukuza hali ya mambo mazuri ndani yao na kuachana na mabaya. Mungu apenda watumishi wake wajue matengenezo ya tabia za mioyo yao wenyewe. Ili kulitimiza hili, mara nyingi huruhusu moto wa mateso kuwashambulia kusudi wapate kusafishwa. “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, nave atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.” Malaki 3:2, 3. 114T 85;.KN 63.4

  Mungu huongoza watu wake mbele, hatua kwa hatua. Huwapandisna katika mambo yaliyokusudiwa kudhihirisha kitu kilicho moyoni. Wengine hustahimili jambo moja, na kushindwa kwa lingine. Wengine hustahimili jambo moja, na kushindwa kwa lingine. Wengine hustahimili jambo moja, na kushindwa kwa iingine. Katika kila jambo linalozidi hali yake moyo hupimwa na kujaribiwa zaidi kidogo. Kama wale wanaojiita watu wa Mungu wanaona mioyo yao inahitilafiana na kazi hii nyofu, hilo lingewasadikisha kuwa wanayo kazi ya kufanya ili kushinda, kama hawataki kutapikwa kutoka mdomoni mwa Mungu. 12IT 187; KN 64.1

  Mara tujuapo hali yetu ya kutoweza kuifanya kazi ya Mungu na kujitoa kuongozwa kwa hekima yake, Bwana aweza kufanya kazi pamoja nasi. Kama tutatoa moyoni kujipenda nafsi wenyewe bila kujali wengine, ataturuzuku mahitaji yetu yote. 137T 213;KN 64.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents