Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Waume Wawe Wenye Huruma

    Yawapasa waume kuwa waangalifu, wenye bidii, waaminifu, na wenye huruma. Wangeonyesha upendo na moyo wa huruma. Kama wakiyatimiza maneno ya Kristo, upendo wao hautakuwa hali mbaya ya kidunia, wa kuamsha tamaa za mwili, wenye kuleta uharibifu wa miili yao wenyewe na kuwaletea wake zao udhaifu na ugonjwa. Hawatatimiza tamaa mbaya za mwili huku wakiwaambia wake zao kwamba hawana budi kuwatii waume kwa kila jambo. Mume akiwa na tabia njema , usafi wa moyo, ubora wa akili apaswao kila Mkristo wa kweli kuwa nao, itadhihirika katika unyumba. Ikiwa anayo ile nia ya Kristo hatakuwa mharibifu wa mwili, bali atajawa na upendo wa kweli, akijitahidi kukifikia kipeo cha juu kabisa ndani ya Kristo.KN 154.5

    Hakuna mtu ampendaye kwa kweli mkewe atakayemkubalia awe mtumwa na mhudumiaji wa tamaa zake mbovu za mwili. Katika ustahimilivu wake hupoteza thamani aliyopata kuwa nayo machoni _pa mumewe. Humwona akidhoofu na kuwa na hali duni kwa kila jambo, na mara huanza kushuku kuwa (Mkewe) atakubali, bila kukaidi, kutendwa na mtu mwingine kama atendwavyo na mumewe mwenyewe. Huutilia shaka uaminifu na usafi wake, ulegevu wake, na hutafuta wengine wapya kuamsha na kuzidisha tamaa zake za mwili mbaya mno. Sheria ya Mungu hudharauliwa. Watu hawa ni wabaya kuliko wanyama wa mwitu; ni mashetani walio katika umbo la mwanadamu. Hawayafahamu mafundisho ya kweli yenye kuikuza hali na kuadilisha, wala upendo mtakatifu.KN 155.1

    Mke pia humwonea wivu memewe na kumshuku kuwa kama pakiwa na nafasi, kwa urahisi atamtongoza mwingine kama amfanyiavyo. Huona kuwa hatawaliwi na dnamiri ya moyoni au kicho cha Mungu; vizuuizi vyote hivi vitakatifu vimevunjwa na tamaa mbaya za mwili; mema yote kwa mume yamefanywa kuwa yenye kuzitimiza tamaa mbaya za kinyama.KN 155.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents