Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wakati Madai yasiyofaa Yafanywapo

    Neno la kukatwa sasa ni hili: Je, mke ataona kuwa hana budi kukubali kwa urahisi madai ya mumewe akiona kuwa siyo kitu kingine ila tamaa mbaya tu za mwili zinazomtawala mumewe, na moyoni na akilini mwake akisadiki kuwa akifanya hivyo audhuru mwili wake, ambao Mungu amemwamuru kuutunza na kuuweka katika hali takatifu na ya neshima, kuuhifadhi kama dhabihu iliyo hai kwa Mungu?KN 155.3

    Upendo safi, mtakatifu haumwongozi mwanamke kutimiza shauku za mumewe na kupata hasara ya afya na uzima. Kama akiwa na upendo wa kweli na hekima, atafanya bidii kuigeuza nia yake na kuacha kuzitimiza tamaa mbaya za mwili na kuyaelekea mambo bora ya kiroho kwa kuyafikiri sana mafundisho ya dini yanayopendeza. Pengine italazimu kusisitiza mara nyingi kwa unyenyekevu na upendo, hata ikiwa ni kumchukiza, kwamba hawezi kuuharibu mwili wake kwa kukubali kutwaana kupita kiasi. Apaswa, kwa upole na moyo mzuri, kumkumbusha kuwa Mungu analo dai la kwanza na kuu kuliko mengine yote juu ya mwili wake mzima, na ya kuwa hawezi kulidharau dai hili, kwa sababu atatakiwa kutoa hesabu yake katika siku kuu ya Mungu.KN 155.4

    Kama atayazidisha mapenzi yake na kwa utakatifu na heshima kuhifadhi hali bora ya kumstahili mwanamke, aweza kufanya makuu kwa mvuto wake wa busara kumwadilisha mumewe pamoja naye mwenyewe, hivyo afanya kazi maradufu. Katika jamoo hili, ambalo ni gumu na la shida kulitimiza, hekima nyingi na uvumilivu hutakikana, pamoja na moyo wa adili na uhodari. Nguvu na neema vyaweza kupatikana kwa maombi. Upendo safi hauna budi kuwa kanuni itawalayo moyoni. Upendo kwa Mungu na upendo kwa mume peke yake waweza kuwa msingi bora wa matendo.KN 156.1

    Mke akikubali kutoa mwili wake na nia yake kutawaliwa na mumewe, akimwacha atende apendavyo kwa mambo yote, akiitoa dhamiri ya moyoni mwake, hesnima yake, hata hadhi yake, apoteza nafasi nzuri ya kujitahidi ambayo pengine ingekuwa na mvuto mwema ambao apaswa kuwa nao kumwinua mumewe awe na hali bora. Angeweza kuupunguza uakili wake, na mvuto wake utakasao ungeweza kutumiwa kwa njia ya kutakasa na kusafisha, ukimwongoza kukazana kwa bidii kuzitawala tamaa za mwili na kuwa mwenye moyo wa kupenda mambo ya kiroho, kusudi wapate pamoja kuwa washiriki wa tabia ya Mungu wakiwa wameuepuka uharibifu uliomo ulimwenguni kwa njia ya tamaa za mwili. Uwezo wa mvuto huweza kuwa kitu kikubwa cha kuiongoza nia ya mtu kwenye mambo bora, na kuyaacha mambo duni, kujifurahisha kwa tamaa mbaya za mwili, ambazo moyo usioongoka kwa kawaida kuyafuata. Kama mke akiona moyoni kuwa kusudi ampendeze mumewe hana budi kujidhili na kuwa na hali ya mumewe, wakati tamaa za mwili zikiwa msingi wa upendo wake na kanuni inayoyatawala matendo yake, humcnukiza Mungu; maana hautumii mvuto utakasao juu ya mumewe. Ikiwa anaona kuwa hana budi kushindwa na tamaa mbaya ya mumewe pasipo kusema neno lo lote la onyo, haufahamu wajibu wake kwa mumewe au kwa Mungu wake.KN 156.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents