Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mazoea ya Kujizuia na Kuwa na Kiasi

    Aha, laiti ningeweza kuwafahamisha wote wajibu wao kwa Mungu kutunza viungo vya akili na vya mwili na kuviweka katika hali bora kabisa wapate kumtumikia Mumbaji wao! Hebu mke aliye Mkristo ajizuie, kwa neno na kwa tendo pia, asiamshe tamaa za mwili za mumewe. Wengi hawana nguvu za kutupa ovyo kwa jambo hili Tokea utotoni mwao wamedhoofisha ubongo na kuufyonza mwili, kwa kutimiza tamaa mbaya za mwili bila ya kujizuia. Kujizuia na kuwa na kiasi yapasa liwe neno kubwa katika maisha yao ya ngono.KN 153.2

    Tuko chini ya wajibu mzito kwa Mungu kutunza roho iwe safl na mwili uwe wenye afya, kusudi tupate kuwanufaisha wanadamu wenzetu na kumtumikia Mungu kwa ukamilifu. Mtume amesema maneno haya ya onyo: “Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata makazitii tamaa zake.” Anatusukuma mbele kwa kutuambia kuwa “kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika vote.” Anawaonya wote wajiitao Wakristo kuitoa miili yao iwe “dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu.” Asema: “nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.”KN 153.3

    Upendo safi sio wenye kumchochea mwanamume kumfanya mkewe chombo cha kutumia kuiridhisha tamaa yake. Tamaa za mwili ndizo zenye kutimizwa bila kujizuia. Ni wachache kama nini wanaoonyesha upendo wao kwa njia ambayo imeelezwa na mtume: “Kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha (siyo kulinajisi)... bali liwe takatifu lisilo na mawaa.” Huu ni namna ya upendo utakiwao katika ndoa ambayo Mungu huihesabu kuwa takatifu. Upendo ni kanuni safi na takatifu, lakini tamaa mbaya haitakubali kujizuia wala haitatii ama kutawaliwa na akili ya moyoni. Haiyaoni matokeo ya baadaye, wala kuifikiri njia inayoifuata, na matokeo yake.KN 153.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents