Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Yawapasa Wazazi Kupatana

    Watoto wana tabia za kutambua kwa upesi sana, na za upendo. Hupendezwa kwa urahisi na kukasirishwa kwa urahisi. Malezi mazuri ya upole kwa maneno na vitendo akina mama huweza kuwafungamanisha watoto wao na mioyo yao. Kuonyesha ukali na kuwadhulumu watoto ni makosa makubwa. Utawala imara usio wa hasira ni jambo muhimu kwa utii wa watu wa kila nyumba. Sema kile unachonuia kwa utulivu, kata shauri kwa busara, na kutimiza usemalo bila kwenda upande. 73T 532;KN 217.1

    Yawapasa wazazi wasisahau miaka yao ya utotoni, jinsi walivyokuwa wakikasirika walipolaumiwa na kukemewa bure. Yafaa wawe watoto tena katika maoni yao na kufahamu mioyoni mwao haja za watoto wao. Lakini, wakiwa imara, na wenye upendo pia, wangetaka utii kutoka kwa watoto wao. Neno la wazazi lingefuatwa kabisa. 81T 388;KN 217.2

    Kutokuwa imara katika utawala wa watu wa nyumbani ni jambo lenye madhara makubwa, kwa kweli ni baya karibu sawa na kutokuwa na utawala kabisa. Swali linaloulizwa kila mara ni ya kuwa, Mbona mara kwa mara watoto wa wazazi walio na dini ni wakaidi, wenye dharau, na waasi? Sababu ya hali hiyo hupatikana katika malezi ya nyumbani.KN 217.3

    Kama wazazi hawapatani, afadhali waondoke mbele ya watoto wao mpaka hapo watakapoweza kusikilizana.KN 217.4

    Ikiwa wazazi wanashirikiana katika kazi hiyo ya malezi, mtoto atafahamu kile anachotakiwa kufanya. Lakini kama baba, kwa neno au kwa mtazamo, huonyesha kuwa hakubaliani na malezi yatolewayo na mama; kama huona kuwa mama ni mkali mno na kudhani kwamba hana budi kumtuliza mtoto kwa kumbembeleza na kumwendekeza, mtoto huyo ataharibika. Atajifunza upesi kuwa aweza kufanya kama apandavyo. Wazazi wafanyao kosa hili kwa watoto, kuharibika kwa roho za watoto wao ni juu yao. 9AH 310-315;KN 217.5

    Wazazi wangejifunza kwanza kujitawala, ndipo wanaweza kuwatawala vizuri watoto wao. Kila wakati wanaposhindwa kujitawala, na kuanza kusema na kutenda mambo kwa pupa, hutenda dhambi kwa Mungu. Yafaa kwanza kujadiliana na watoto wao, wayadhihirishe makosa yao, wawaonyeshe dhambi yao, na kuwafanya waone huzuni kwamba licha ya kuwakosea wazazi wao, hata wametenda dhambi kwa Mungu. Mkiwa na moyo laini na uliojaa huruma na masikitiko kwa ajili ya watoto wenu wakosaji, ombeni pamoja nao kabla ya kuwarudi. Ndipo mkiwarudi hawatawachukia. Watawapenda. Wataona kuwa hamwapi adhabu kwa sababu wamewachukiza, wala kwa sababu mwataka kuonyesha chuki yenu juu yao; bali kwa kuwa ni wajibu, kwa ajili ya faida yao, kusudi wasiweze kuachwa kukua dhambini. 101T 398;KN 217.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents