Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Tumbaku ni simu Itendayo Kazi Taratibu

    Tumbako ina sumu mbaya sana inayodhuru, ingawa inatenda kazi yake kwa siri polepole. Ingawa itumiwe kwa njia iwayo yote, inadhihirika kwa kuzidhoofisha nguvu za mwili; tumbaku ina madhara zaidi kwa sababu matokeo yake ni ya polepole sana, nayo ni vigumu kujulikana mwanzoni. Kwanza inaishtua mishipa ya fahamu, halafu inaipoozesha. Inaudhoofisha ubongo na kuutia bumbuazi. Mara nyingi hudhuru mishipa ya fahamu kwa nguvu zaidi ya vileo. Ni vigumu kufahamu hivi, na matokeo yake ni vigumu kuyaondoa kabisa mwilini. Kuitumia tumbaku kunaamsha kiu ya kutaka vileo, na kwa watu wengi inakuwa sababu ya mazoea mabaya ya kunywa pombe.KN 120.3

    Kuvuta tumbaku kunamletea mvutaji masumbufu na gharama nyingi, ni mazoea machafu yanayomnajisi mvutaji mwenyewe na kuwaudhi wengine. Madhara ya tumbaku kwa watoto na vijana hayaelezeki. Watoto wa kiume wanaanza kutumia tumbaku mapema wangali wadogo. Mazoea mabaya yanayofanywa namna nii, hasa wakati mwili na akili za mtoto zinapoweza kupatwa upesi na madhara yake, yanadhofisha nguvu za mwili, hudumaza mwili, hupoteza akili, na huharibu tabia ya mtu. 12MH 327-329;KN 120.4

    Hakuna tamaa ya asili ya kutaka tumbaku isipokuwa imerithishwa.KN 120.5

    Kwa kutumia majani ya chai na kahawa tamaa ya kutaka tumbaku hujengeka.KN 120.6

    Chakula kinachokolezwa viungo vikali vya chakula huunguza matumbo, huharibu damu, na kuvitayarishia njia vileo vikali zaidi. 13Te 56, 57;KN 120.7

    Kitoweo cha nyama kilichokolezwa kwa viungo vya chakula, chai na kahawa, vitu ambavyo mama wengine huwatia moyo watoto wao kuvitumia, huwatayarishia njia kuonea uchi vitu vinavyozimua nguvu mwilini, kama tumbaku. Kuvuta tumbaku hutia nguvu kiu ya pombe. 143T 488, 489;KN 120.8

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents