Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi ya Kupokea Karipio

  Wale ambao hukaripiwa na Roho wa Mungu haiwapasi kuondoka na kushindana na chombo hiki kiadilifu. Ni Mungu, wala si mwanadamu mkosaji, ambaye amesema ili kuwaokoa na uharibifu. Si jambo la kumpendeza mwanadamu kwa hali yake ya asili kupokea karipio, waia haiwezekani kwa moyo wa mwanadamu usioadilishwa na Roho wa Mungu, kufahamu lazima ya karipio au mbaraka uliokusudiwa kuletwa. Akili za movoni kupotoshwa. Maonyo ya dhamiri hudharauliwa, na sauti yake haisikiki wazi. Hupotewa kidogo kidogo na uwezo wa kupambanua baina ya mema na mabaya, mpaka awe na fahamu halisi za kusimama kwake mbele za Mungu. Huenda akawa anatimiza namna ya dini na kwa bidii kuyapata mafundisho yake, huku akiwa hana roho wake. Hali yake ndiyo ile iliyoelezwa na Shahidi aliye Mwaminifu: “Wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” Wakati Roho wa Mungu, kwa ujumbe wa karipio, asemapo kuwa hii ndiyo hali yake, hawezi kuona kuwa ujumbe huu ni kweli. Kwa hiyo, apaswa kulikataa onyo? La. Mungu ametoa ushuhuda wa kutosha, ili wote wapendao kufanya hivyo waridhike na tabia ya hizi shuhuda; na wakiisna kuzikiri kuwa zatoka kwa Mungu, ni wajibu wao kukubali lawama, ijapokuwa hawaoni wao wenyewe ubaya wa njia yao. Kama wangefahamu kabisa hali yao, kungekuwa na haja gani ya karipio? Kwa sababu hawaijui, Mungu kwa huruma huiweka mbele yao, kusudi wapate kutubu na kuongoka kabla ya kuchelewa sana. Wale wenye kulidharau onyo hili wataachwa katika upofu na kuendelea kujidanganya wenyewe; lakini wale ambayo hulitii, na wafanyao bidii kujitenga na dhambi na kuziacha ili kuwa na sifa njema zitakikanazo, watakuwa wakiufimgua mlango wa mioyo yao ili Mwokozi apate kuingia na kukaa nao. Wale amoao wanahusiana sana na Mungu ni wale ambao huijua sauti yake asemapo nao. Walio wa kirono huyapambanua mambo ya kiroho. Watu kama hao watashukuru kuwa Mungu ameonyesha makosa yao.KN 111.2

  Daudi alijifunza hekima kutoka kwa mambo Mungu aliyomtendea na akasujudu kwa unyenyekevu katika kurudiwa na Mwenyezi Mungu. Maelezo kamili ya hali yake hasa yaliyotolewa na nabii Nathani yalifanya Daudi kuzifahamu dhambi zake mwenyewe nayo yalimsaidia kuziacha. Akakubali mashauri mema kwa moyo mnyenyekevu na kujidhili mbele za Mungu. “Sheria ya Bwana,” asema, “ni kamilifu, huburudisha nafsi.” (Zaburi 19:7).KN 112.1

  “Kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa si wana wa halali.” (Waebrania 12:8) Bwana wetu amesema: “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi (Ufunuo 3:19). “Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.” (Waebrania 12:11). Ingawa marudi haya yawe makali, yameamuriwa kwa upendo wa Baba, “ili tuushiriki utakatifu wake . ‘ 115T 682, 683.KN 112.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents