Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuishi kwa Ujasiri Leo

  Neno la kweli la Mungu likipokewa moyoni laweza kuwahekimisha hata kuupata wokovu. Kwa kuliamini na kulitii mtapokea neema ya kuwatosha kwa kazi na shida za leo. Neema kwa ajili ya kesho hamuihitaji sasa. Yawapasa mwone moyoni kuwa mnawajibika na mambo ya leo tu. Shinda kwa leo; jikane nafsi kwa leo; kesha na kuomba kwa leo; pata ushindi kwa Mungu kwa leo. Hali za mambo yetu na mazingira yetu, mabadiliko ambayo kila siku hubainika pande zote kutuzunguka, na neno la Mungu lililoandikwa lenye kuona na kuthibitisha mambo yote-hayo hutosha kutufundisha wajibu wetu na kile kitupasacho kutenda, siku kwa siku. Badala ya kuyazuia mawazo ya moyo wako kuingia katika mkondo wa mafikara ambayo hayatakufaidia, yakupasa kuyachunguza Maandiko Matakatifu kila siku na kuzifanya kazi zile ambazo katika maisha ya kila siku zaweza sasa kuwa za kukuchosha, lakini ambazo hazina budi kutendwa na mtu fulani. 53T 333;KN 91.3

  Wengi huukazia macho uovu wa kutisha ulio kwa wingi pande zote kuwazunguka, ukafiri na udhaifu kila upande, nao nuongea juu ya mambo haya mpaka mioyo yao imejawa na huzuni na mashaka. Hutukuza kazi ya yule mdanganyifu mkuu ya mawazo ya moyoni na kutafakari mambo ya kukatisha tamaa yanayowapata maishani mwao, huku wakielekea kukosa kuuona uwezo wa Baba aliye mbinguni na upendo wake usio na kifani ndivyo Shetani apendavyo. Ni kosa kumfikiria yule adui wa haki kama mwenye uwezo mkuu, huku tukifikiria kidogo tu juu ya upendo wa Mungu na uwezo wake. Yatupasa kuzungumza habari za uwezo wa Kristo. Sisi wenyewe hatuwezi hata kidogo kujifungua kutoka mikononi mwa Shetani tulimoshikwa; lakini Mungu ameweka njia ya kuokoka.. Mwana wa Mungu anazo nguvu kutupigania, na “tunashinda, na zaidi ya kushinda kwa yeye aliyetupenda.”KN 91.4

  Hakuna nguvu za kiroho kwa ajili yetu katika kufikiria udhaifu na uasi wetu wa dini, na kulilia uwezo wa Shetani. Ukweli huu mkuu hauna budi kuimarishwa kama kanuni yenye nguvu mawazoni na mioyoni mwetu,manufaa ya dhabihu iliyotolewa kwa ajili yetu; kwamba Mungu aweza naye huokoa kabisa wote wanaomwendea wakiafikiana na masharti yaliyotajwa katika Neno lake. Kazi ni kuyaweka mapenzi yetu kando ya mapenzi ya Mungu. Ndipo kwa njia ya damu ya upatanisho, tunakuwa washiriki wa tabia ya Mungu; kwa njia ya Kristo tu watoto wa Mungu, nasi tunayo hakika kwamba Mungu atupenda, naam, kama alivyompenda Mwanawe. Tu hali moja na Yesu. Twatembea mahali Kristo atuongozapo; Anao uwezo kulifukuza giza ambalo Shetani hulitupa liifunge njia yetu, na penye giza na mambo ya kukatisha tamaa mwangaza wa utukufu wake hung’aa mioyoni mwetu.KN 92.1

  Ndugu na dada, kwa kumwangalia ndipo tunabadilika. Kwa kuutafakari upendo wa Mungu na wa Mwokozi wetu, kwa kuufikiria ukamilifu wa tabia ya Mungu na kudai haki ya Kristo kama haki yetu kwa imani, hauna budi kubadilishwa kuwa wenye sura ile ile. Basi, tusikusanye picha zote zisizopendeza-udhalimu na uovu na mambo ya kukatisha tamaa, yenye kuonyesha uwezo wa Shetanikuyakumbuka daima kuyazungumza na kuyalilia mpaka roho zetu zikatishwe tamaa. Roho ya mtu aliyekatishwa tamaa ni mwili wa giza, licha ya kujikosesha kuipokea nuru ya Mungu, hata huizuia isiwafikie wengine. Shetani hupenda kuona matokeo ya picha za ushindi wake, yakiwafanya wanadamu kuwa watu wasio na imani na kuwavunja moyo. 65T 741 -745;KN 92.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents